USAFI na MAZINGIRA KTK AWAMU YA NNE

waziri kalala

Member
Sep 2, 2008
14
0
HIVI ni UFISADI pia unaochangia baadhi ya miji yetu na hasa jiji la Kibiashara Dar es salaam kudorora kwa uchafu kila sehemu.

NI siri gani aliyoitumia Bw. au ni Dk sikuhizi Fredrick Sumaye angalau kulifanya jiji likaanza kuwa na tabia ya usafi. Halafu baada ya kuondoka yeye hali imerudia palepale kama sio mbaya zaidi?

Pengine Mawaziri wakuu baada yake wana shughuli nyingi zaidi. Sawa. Je huyo anayeitwa Waziri wa Mazingira mbona sijawahi kumsikia achilia mbali kumuona kwenye TV akishughulika kuhaha huku na huko na kuona kama makampuni ya ajabu ajabu yaliyopewa tenda za kusafisha jiji na kusomba taka zinawatendea haki wakazi wa jiji hili.

Inavyoelekea ni kuwa mengi ya makampuni yenye tenda ya KUZOA TAKA kwanza hayana ajenda ya usafi bali kutajirika haraka haraka.

Makampuni hayo hayana vifaa kabisa na vifaa walivyo navyo sio hatari tu kwa wafanyakazi wao bali pia kwa jamii inayohudumiwa.

Hivi kweli hatuwezi kupata wawekezaji wenye vifaa na mitambo ya kubadili taka kuwa kitu kinachofaa kutumika.

Ninajua kuna makampuni kadhaa toka Norway hadi Seychelles ambayo yana uwezo wa kuwekeza katika biashara ya ukokotaji taka na kuzigeuza kuwa mbolea, karatasi, maboksi, chupa na kadhalika lakini hayapati ushirikiano wa kuridhisha toka kwa wakubwa kwa kuwa wawekezaji hawataki kutoa kitu kidogo au kuwafanya wakuu wawe madairekta kwenye kampuni hizo!

HIVI kweli karibu miaka 50 baada ya Uhuru Watanzania tunashindwa kuachana kabisa na tatizo la taka.

Waziri na watu wake hata wameshindwa kuanzisha kampeni ya TUNZA MJI AU JIJI LAKO kwa kutumia redio, televisheni na magazeti ya walipa kodi?

Au sampuli ya watu TBC iliyowamulika katika Wizara ya Miundombinu ndio wamo humu pia. Jamaa wana vitambi wanaburudika na airconditioner lakini hawajui wala hawataki kuwa na lugha nzuri kwa waandishi wa habari tena wa serikali?
Ndio maana migomo TRL haiwezi ikaisha eti?

NIULIZE swali moja hivi Waziri wa Mazingira anahesabu anafanya kazi kwa kwenda na kujificha kwenye chumba chake makao makuu ya wizara au hapo alipo akiburudishwa na kiyoyozi akahesabu kweli yumo kazini?

Hebu tuchambueni jamani hili tuwasaidie ndugu zetu hawa. Kuna wizara bwana kama vile ya fedha ikitoka tu unaibiwa!

Lakini kuna Wizara zingine ukikaa ofisini wallahi unadanganywa na hakuna kitakachofanyika.

Akili ni nywele kila mtu ana zake. Labda kama ni mkuu wa nchi au Waziri Mkuu tu ndiye anayweza kuanzisha tena upya kampeni ya usafi jijini au kufuatilia magari mabovu yanayochafua jiji badala ya kusomba taka na wahudumu wenye lugha chafu kuliko ya makuli!

Nibarikiwe, na nyie mbarikiwe. Hakika tunahitaji baraka na ufunuo ili tuondokane na uziwi na upofu unaotuzuia kutenda yale yanayopaswa kutendwa kwa kudhani sio wewe au sio mimi bali ni yule. Wakati na yule naye anadhania vivyo hivyo!
 
Back
Top Bottom