Serikali imefanya jambo jema la kuwaondoa watumishi hewa kwenye Payroll, Hongera kwa hilo. Japo sijasikia hatua stahiki kwa waliowaweka au kuwabeba. Pia waliochukua pesa hizo wamefanywa nini?
Nirudi kwenye mada, Rais akitumbua vyeti feki nchi itatikisika. Sio kwamba natisha au natania hili ni janga. Atafungua milango miwili tu atakachokikuta humo ndani, he he hee atarudi Chato kula ugali na sato mapumzikoni. Hembu aende JWTZ, TANAPA, MAGEREZA, POLISI na AFYA upande wa manesi, kada za chini yaani certificate, diploma atajionea.
Kwa kuwa Rais wangu mpendwa ulisema hutafukua makaburi hata hili la vyeti feki Sio makaburi tu Bali ni Jehanamu ya watumishi wengi wa umma ukilivalia njuga. Nusu tutaondoka hata Mimi huenda nitakuwemo.
Ukiamua kusamehe samehe wote mkuu, usibague baadhi ya idara zingine ukaziacha utaleta nanung'uniko watakao kumbwa na kokoro hili wakubali matokeo, hata walivyokula vinatosha japo nina imani vibaka, wezi, majangili, majambazi, malaya, makahaba na matapeli watajaa mtaani ukilitekekeza hili Rais wangu. Najua unahekima sana kaa na wazee kadhaa unao waamini ili wakushauri namna bora ya kutumbua jipu hili, liko pabaya linahitaji umakini mkubwa.