Rais wa Matajiri
JF-Expert Member
- Sep 14, 2018
- 1,475
- 607
Kuna watu wanapenda kudharau watu toka Mataifa yaliyoendelea kama Marekani na mengineyo kwa kuwaita eti wao ni "Mabeberu " kitu ambacho sichema kwa ustawi wa nchi na kwanchi zinazotuletea biashara na ajira kama hizi kuwaita "Mabeberu " japo hii sio hoja yangu wacha twende kwenye hoja.
Marekani ni nchi iliyowekeza Tanzania karibu maratatu ya Jumla ya kiasi ilichowekeza Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi,hadi mwaka 2019 Jumla ya uwekezaji wa Marekani kwa Tanzania ulifikia US$1.5BL sawa na TZS 3.45Trilioni ikifuatiwa na Kenya US$353M, Uganda $42M, Rwanda $11M na Burundi US$1M uwekezaji huu wa,Kenya, Uganda,Rwanda na Burundi ni sawa na Jumla ya $407M au TZS 936.1BL.
Baraza la Biashara Africa Mashariki The East African Business Council ( EABC ) tayari limesaini makubaliano (MoU) na Kituo cha Kibiashara cha Africa na Dunia cha The Africa Global Chamber of Commerce (AGCC) ili kuuvuta zaidi uwekeji wa Marekani uje kwa wingi Ukanda huu wa Africa ya Mashariki.
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipambanua kujali na kuthamini kila mwekezaji awe wa nje au wandani kwani sekta binafsi kwa mujibu wa taarifa za TPSF zinaonesha Sekta binafsi kwa Tanzania inabeba zaidi ya 90% ya ajira zote Tanzania,Lakini inachangia 80% ya mapato yote ya Serikali na inabeba 60% ya uwekezaji wote wa nchi.
Tangu Rais Samia aingie madarakani majarida mbalimbali yamekuwa yakiitaja Tanzania kama Sehemu salama zaidi ya kuwekeza kwa mwaka 2021 ikiwa kwenye nafasi ya kumi bora pamoja na Kenya na Rwanda pengine hii ndio inasukuma zaidi kusainiwa kwa hii MoU kati ya AGCC na EABC itakayofungua milango kwa Wamarekani wanaomiliki 25% ya Uchumi wote wa Dunia ambayo ulifikia US$ 84.54Ttrilioni mwaka 2020 kutiririka Africa Mashariki hasahasa Tanzania kwaajili ya kuwekeza zaidi,endelea kujisomea hapo chini..