US TECHNOLOGY: How to Spot A liar!

Apr 27, 2006
26,588
10,374
Few things are easier than telling a lie, and few things are harder than spotting one when it is told to us. We have been trying to suss out liars ever since Cain fibbed to God about murdering Abel. God was not fooled, hearing the blood of Abel cring out from the land, the rest of us do not have such divine lie-detection gifts!

But that doesn't mean we are not trying! Quitely over the past five years, the US Dept. of Defense have dramaticcaly stepped up the hunt, millions of dollars are believed to have been poured into lie-detection techniques as diverse as infrared imagers to study the eyes, scanners to peer into the brain, sensors to spot liars from a distance, and analysist trained to scrutinize the unconscious facial flutters that often accompany a falsehood!

Wazee mnasemaje, je bongo tunahitaji hiiitechnology kama ipo?
 
Inawezekana vitu kama hivi vikakubalika hapa kwetu as long as haitatofautisha samaki wakubwa kwa wadogo.
 
Mzee ES
Kwa hapa Bongo, huhitaji hiyo teknolojia kwani "liars" wa Bongo wanadanganya mpaka mpumbavu anaona kabisa huo ni uongo.

Miaka michache nilifanya kazi kuchunguza wizi wa fedha kwenye benki moja na haikunichukua hata masaa kadhaa kabla sijaona uongo.

Wabongo ni rahisi mno kudanganywa na kudanganyika.
 
Habari zenu waheshimiwa

Hili swala ni interesting sana kwa sababu la kwamba lipo hapo toka enzi. Uongo hautaacha kuwepo so long as binaadamu anaexist. Ninge omba kabla hatuja tafuta tiba ya uongo na jinsi ya kuweka wazi uongo tufafanue uongo maanake kuna wongo wa kila aina. Kwa mfano:
1.kuna uongo wa watu binafsi ambaye mtu anamdaganya:
A) mwenzake kwa sababu kadhaa, anaweza kua huyo muongo ana umwa na anadanganya tu.
B) Mtu anamdanganya mwanae au mkewe

2. Uongo wa kidini
3. Uongo wa mashirika ya habari
4. Uongo wa Kisiasa
4. Uongo wa takwimu
5. uongo wa kitamaduni
Uongo na uwongo, na wapo wanaosema uongo kwa kuendelza uongo kwa sababu ni kazi yao.
Kuna uongo ambae leo ni uongo lakini kesho ni ukweli au leo ni ukweli kesho uongo.

Nategemea sija wachanganya lakini hebu tufafanue ni uongo wa aina gani tunazungumzia? Na ni mategemo gani ambayo tunayo kwa kupata chombo cha kushika waongo?
 
Bora hii ije kuliko ya ujanja wa kutengeneza Mvua ya Lowasa duh !! tutaweza kuwabana wez wa kalamu na kuingia mikataba ya uongo
 
Tatizo la mabingwa wa uongo, ni pale wanapodanganya hadi wao wenyewe wanaamini wanasema kweli!! Mfano mzuri ni ule wa Clinton.." I did not have sexual relationship with that woman.. miss Lewinsky" didn't you believe that until the blue dress came to light!!

Kwa sisi wabongo, kuna uongo ambao unatolewa kwa jina la serikali au chama, na kwa sababu hiyo tunauamini na kuuita ukweli. Rais JK alipozungumza Mwanza na kusema kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa silaha haramu zinasafirishwa kupitia Tanzania, CCM, Bunge na jumuiya kadhaa za kiraia ziliamini na kukubali!!

Kwa muda mrefu tumeambiwa kuwa sisi ni Masikini.. na kwa bahati mbaya tumeamini na tunaishi kama masikini!! Wakati wanaojua sisi ni matajiri wanakujwa na kujichotea mali zetu huku sisi tukibakia kuomba omba!!

Hiki kinanikumbusha kile kisa cha watoto wawili, yule mdogo alimuendea baba yake na kumlaghai ili ampatie pesa kiasi kadhaa, mzee alimsikiliza kwa makini na bila kujua anadanganywa basi alimkubalia. Yule mkubwa alipokutana na mdogo wake na kushangaa jinsi gani aliweza kupata fedha kwa baba yao ambao ni bahili sana, yule mdogo alijibu kwa ufupi tu "Nilimfunga kamba"

Yule mkubwa kwa utaahira wake, akaamua kwenda "kumfunga kamba baba yake". Marehemu aliacha mke na watoto wawili!!!
 
Back
Top Bottom