US Police Reform Bill

jollyman91

Member
Sep 21, 2021
69
29
Bipartisan negotiations in the US senate over a police reform bill have collapsed. The piece of legislation would have banned chokeholds and limited immunity for officers and would have set national policing standards.
 
Kwa kingereza hiko Haji mtu kukoment si utaniambia
kuna bill walioweka kwa ajili ya kupunguza nguvu za askari marekani ila imefeli . yaani askari kila anachokifanya hana kuhukumiwa. ni sawa tu na sheria za kule zinasaidia
 
Nachopendea wenzetu ni wamestaarabika na viongozi wengi wana hekima.

Magereza yao yanalenga kurekebisha tabia Siyo kuadhibu...
Umungu mtu haupo kwa sababu kila mtu anajua mtu ni nini... mtu asili yake ni nini!!

Mara ngapi Africa mfungwa analazw hospitali kwa upungufu wa sukari mwilini( Hypoglycemia?). Ni mateso, hawali... sijajua kama hawa watu wanapata hata milo miwili per day!!!

Wafungwa wengi wanauguzwa hospitali Africa shida zao ni sukari ya chini na kukosa haja kubwa... sasa mtu hauli utajisaidia nini msalani???

Malcom aliibukia gerezani...

Bongo ni mfungwa yupi anatoka anaakili ya maisha... anatoka ana falsafa yoyote nzuri ya kumpa muongozo maishani .

Tuna Punitive prisons badala ya corrective ones..
Uhitaji wa viongozi wanaoheshimu utu( mtu) hata kama mkosefu ni mkubwa...

Viongozi wakipewa madaraka tuu yanawapanda kichwani wanawehuka... wanalose Perspective... Viongozi wetu wanaamini Hisia zao Ndo uhalisia... Yani anavyoona basi ni sahihi..

Mpaka sasa Polisi kwetu ni jeshi badala ya idara... polisi... National police force... nguvu tu...

Hiyo force inatakiwa iondolewe tubaki na the national police...

Kuna mambo mengi kwenye mfumo wetu yanahitaji kufumuliwa kabisa...

Ubaya watu wanaaamini mifumo Inatoka kwa Mungu... hapana. Na baadhi ya watu huwatia hofu wenzao wakiwaaminisha ni afadhali kuendelea mifumo mibovu iliyopo kuliko kuibadilisha...
Hapa nakubali “ The fear of change is real”

Lakini watu waliostaarabika huembrace change... rejoicing in change instead of an everlasting order.

Mifumo yote ya maisha tunayoishi imewekwa na watu... na watu ndiyo wanoweza kuivunja... kama hekima iliyotumika kuweka mfumo fulani itaonekana ina upungufu sehemu ni lazima ibadilishwe... hakuna mtu aliyekamili... na maisha yanabadilika...

Kuna mtu aliwahi kusema “ the only thing that is permanent is change “

Ndiyo Rais wa kwanza aliweka mifumo fulani mizuri... hii haina maaana watu wataishi na hiyo mifumo miaka 500 ijayo... tunakosa broad Perspective... tunaishi kileoleo sana... unakuta upartisan ni mwingi kupindukia...

Let us Try thinking long term...na tuweke mifumo ambayo hata vitukuu vya wajukuu wetu leo wanaweza kuibadilisha wakiona inamapungufu...

Lengo la mifumo ni kuregulate maisha ya watu... siyo kukandamiza watu.

Viongozi wanaogopa kuvunja mifumo mibovu iliyopo kulinda vyama... lakini time is the best teacher... kile ambacho mnatesa/mnaua watu leo kwa ajili yake kinaweza kuangushwa kirahisi watu wakashangaa.... kipindi ambacho wewe haupo... ushajiozea na madhambi yako ya kutesa/ kuua watu... kipindi hiko uliona unatetea taifa au kiongozi mkuu au tumbo lako...

Ubaya ni kwamba, Few people think long term...
And worse enough they are in power.... those in power are not bold enough to accept change...


Tunahitaji watu wanoona miaka 300 mbele... kipindi ambacho wao na watoto wao na wajukuu hawapo....

Sehemu uliyojenga leo kwa kuhangaika au ukagombana na watu miaka 300 au chini ijayo inaweza kuwa barabara au stendi au sehemu ya halmashauri ya kuzikia ....ni jinsi gani vitu vinarudi kwenye uhalisia ukifikilia in terms of decades, centuries or millennia...

Tunahitaji watu walioko serious kujenga mifumo imara lakini ambayo ipo flexible kwenye kubadilishwa kuendana na wakati... mifumo ambayo Hakuna Mtu atakaeonekana yu zaidi ya wengine...

“What we have learned as a nation is the danger of putting trust in a single man instead of the people “ Mamady Doumbouya, leader of the Guinea Military Coup.
 
Back
Top Bottom