US na EU wakifuata mkondo wa China kwa nchi za Afrika, hali itakuwaje?

Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
7,051
12,560
Tunajua sera za China kwa nchi za Africa,concern yake ni fursa ya kukuza uchumi wake kwa kupata tenda kubwa kubwa za ujenzi na soko la uhakika la bidhaa zake!Taifa hili huwa halijihusishi na mambo mengine kabisa yanayotokea kwenye mataifa ya Africa ilimradi yeye anafanya biashara!Kwa msimamo huo,taifa hili limekuwa role model wa baadhi ya watu na kumuona kama rafiki wa kweli!

Kwa mantiki nikawaza, vipi kama US na nchi za Ulaya zikifuata mkondo wa China?Kwamba na wao wajali tu maslahi yao ya kibiashara bila kuingilia wala kujishughulisha na mambo yanayotokea ndani ya nchi husika!Muwe na amani au msiwe na amani wao wawe kimya na kuendelea kufanya biashara!Muwe na demokrasia au msiwe na demokrasia wao wasijali na waendelee na mishe zao!Pia wasitoe misaada kama ambavyo china hatoi!

Je,hali ya amani na uchumi kwa nchi hizi za Africa itakuwaje?Kwa aina ya viongozi wa africa,siasa zitakuwaje?
 
Mkuu, swali lako limejikoroga sana....
Yaani naona hoja zinazo takiwa kujibiwa kwa hoja, ni nyingi kuliko swali (hapo kwenye umaliziaji)
Anyway......
Ebu ngoja atakae uelewa afike kwanza, pengine nami nitaanza kuelewa hata kidogo
 
Rahisi tu,unaweza jibu katika nyanja tatu tu!Hali ya kisiasa,kiuchumi na kisiasa!
Fikiri leo Tanzania iambiwe sasa uko huru kufanya chochote na hakuna wa kukuuliza,hakuna sanction zozote!
Uamue utawale milele,ni wewe na wananchi wako!Uamue kutunga sheria kali,ni wewe na wananchi wako!Yaani chochote utakachoamua ni juu yako na wananchi wako!
Sasa ndio swali,madhara yake ni nini hasa kwa aina ya viongozi tulionao Africa?
 
Okay......
Jibu ni kwamba, ikitokea ikawa hivyo basi sisi tutakufa tu maana hatutokua na namna (mfano ni matajiri/wafanyabiashara walivyo kubali nyanyasika kwasababu tu hawakua na namna tena ya kuondoka/pakukimbilia).
Baada ya hapo watoto wetu wataanza kuona utawala ni wahovyo na kisha wataanza kuhama na kwenda kutafuta makazi kwenye nchi zingine (mfano ni Somalia/Nigeria).
Kisha kizazi chetu cha tatu kitachoshwa na hali hii ya manyanyaso na kitakua kimepata historia mbaya ya mababu zao ambao ni sisi, then kwakua watakua wamesha kata tamaa na mbele yao ni giza, hapo wataanzisha vuguvugu la harakati za kujikomboa kutokan ana uonevu huu (mfano Libya/Iraq).
Then baada ya hapo nchi zitagawanyika na patatokea majimbo kujitenga na tawala za kifalme/koo zitarejea.
 
Back
Top Bottom