Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,919
- 15,604
Hali ya corona nchini Marekani yaendelea kuwa tete. Visa vilivyothibitishwa hadi sasa ni zaidi ya 35,000 huku watu zaidi ya 450 wakiripotiwa kufa kwa corona.
Kumbukizi:
Mwanzoni mwa janga hili lilipokuwa likiikumba China, na wachina wakawa wapukutika, walitokea kundi la watu, wamatumbi wenzetu, wakawa wakifurahia kuwa China kachapwa corona na US, sasa tutamwona (China) si huwa anajifanya mbabe na taifa lenye nguvu kubwa duniani!
Bali watu hao wakaenda mbali na kusema US amewakomesha China, North Korea na Iran kwa kuwatengenezea corona sasa wapambane nayo.
Watu hawa tuliwaonya tukawaeleza corona haipigi nchi hizo tu, pia yapigaga nchi rafiki wa US, tukawawekea maelezo na rejea zake (sources) kuwa corona inapiga huko South Korea, Italy, na nchi nyingine za Ulaya (kipindi hiko Ulaya visa vipo vichache ktk nchi chace ndio, vilikuwa vyaanza kuripotiwa).
Bali baadae tukawaeleza corona ipo hata US, imeshaingia na wameripoti visa kadhaa (wakati ule walikuwa wagonjwa wachache, pasi na kifo chochote).
Wengi wa kundi hilo la wamatumbi wenzetu hawakuelewa...wao kwa kuwa tu China na Iran ndio wanashambuliwa zaidi na korona waliendelea kufurahi huku baadhi yao wakijitapa kuwa sisi waafrika korona haifui dafu, miili yetu iko ngangari.
Naam, muda ni mwalimu mzuri. Leo korona inawatesa hadi US. Wapendwa wao wapukutika. Mwanzoni Trump aliudogesha ugonjwa na kuufananisha na vijimafua tu. Ila sasa ni tofauti. Pia sisi wamatumbi tuliokuwa tukipiga tambo kubwa kuwa miili yetu corona haiambulii kitu, tumeanza kushuhudia visa vya korona kwa nchi kadhaa za Afrika, tena wamo wamatumbi wenzetu wanaougua.
Sasa twazungumza lugha moja; corona ni janga la dunia, haichagui haibagui utaifa.
Funzo:
Tusipende kufurahia majanga yawapatapo wenzetu, hata kama twawaona ni mahasimu wetu au (mahasimu) wa rafiki zetu.