US: Corona inapamba moto, Walioambukizwa zaidi ya 35000, Vifo zaidi ya 450

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Dec 27, 2019
443
1,000
Hali ya corona nchini Marekani yaendelea kuwa tete. Visa vilivyothibitishwa hadi sasa ni zaidi ya 35,000 huku watu zaidi ya 450 wakiripotiwa kufa kwa corona.

Kumbukizi:
Mwanzoni mwa janga hili lilipokuwa likiikumba China, na wachina wakawa wapukutika, walitokea kundi la watu, wamatumbi wenzetu, wakawa wakifurahia kuwa China kachapwa corona na US, sasa tutamwona (China) si huwa anajifanya mbabe na taifa lenye nguvu kubwa duniani!

Bali watu hao wakaenda mbali na kusema US amewakomesha China, North Korea na Iran kwa kuwatengenezea corona sasa wapambane nayo.

Watu hawa tuliwaonya tukawaeleza corona haipigi nchi hizo tu, pia yapigaga nchi rafiki wa US, tukawawekea maelezo na rejea zake (sources) kuwa corona inapiga huko South Korea, Italy, na nchi nyingine za Ulaya (kipindi hiko Ulaya visa vipo vichache ktk nchi chace ndio, vilikuwa vyaanza kuripotiwa).

Bali baadae tukawaeleza corona ipo hata US, imeshaingia na wameripoti visa kadhaa (wakati ule walikuwa wagonjwa wachache, pasi na kifo chochote).

Wengi wa kundi hilo la wamatumbi wenzetu hawakuelewa...wao kwa kuwa tu China na Iran ndio wanashambuliwa zaidi na korona waliendelea kufurahi huku baadhi yao wakijitapa kuwa sisi waafrika korona haifui dafu, miili yetu iko ngangari.

Naam, muda ni mwalimu mzuri. Leo korona inawatesa hadi US. Wapendwa wao wapukutika. Mwanzoni Trump aliudogesha ugonjwa na kuufananisha na vijimafua tu. Ila sasa ni tofauti. Pia sisi wamatumbi tuliokuwa tukipiga tambo kubwa kuwa miili yetu corona haiambulii kitu, tumeanza kushuhudia visa vya korona kwa nchi kadhaa za Afrika, tena wamo wamatumbi wenzetu wanaougua.
Sasa twazungumza lugha moja; corona ni janga la dunia, haichagui haibagui utaifa.

Funzo:
Tusipende kufurahia majanga yawapatapo wenzetu, hata kama twawaona ni mahasimu wetu au (mahasimu) wa rafiki zetu.
2020-03-23 08.58.14.jpg
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,387
2,000
... uko sahihi; kuna wamatumbi na wasio wamatumbi pia akiwamo yule mhubiri wa Iraq na wengineo bila aibu wala haya eti coronavirus ni adhabu toka kwa Allah kuiadhibu China kwa kuwatesa watu wa Uighur (jimbo mojawapo la uchina) kwa sababu ya dini yao!
 
Latrice

JF-Expert Member
Jan 30, 2020
2,138

Uzi wake huyu ni wakinafki tu

Kumbukizi:
Mwanzoni mwa janga hili lilipokuwa likiikumba China, na wachina wakawa wapukutika, walitokea kundi la watu, wamatumbi wenzetu, wakawa wakifurahia kuwa China kachapwa corona na US, sasa tutamwona (China) si huwa anajifanya mbabe na taifa lenye nguvu kubwa duniani!
 
Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
8,371
2,000
Hali ya corona nchini Marekani yaendelea kuwa tete. Visa vilivyothibitishwa hadi sasa ni zaidi ya 35,000 huku watu zaidi ya 450 wakiripotiwa kufa kwa corona.

Kumbukizi:
Mwanzoni mwa janga hili lilipokuwa likiikumba China, na wachina wakawa wapukutika, walitokea kundi la watu, wamatumbi wenzetu, wakawa wakifurahia kuwa China kachapwa corona na US, sasa tutamwona (China) si huwa anajifanya mbabe na taifa lenye nguvu kubwa duniani!

Bali watu hao wakaenda mbali na kusema US amewakomesha China, North Korea na Iran kwa kuwatengenezea corona sasa wapambane nayo.

Watu hawa tuliwaonya tukawaeleza corona haipigi nchi hizo tu, pia yapigaga nchi rafiki wa US, tukawawekea maelezo na rejea zake (sources) kuwa corona inapiga huko South Korea, Italy, na nchi nyingine za Ulaya (kipindi hiko Ulaya visa vipo vichache ktk nchi chace ndio, vilikuwa vyaanza kuripotiwa).

Bali baadae tukawaeleza corona ipo hata US, imeshaingia na wameripoti visa kadhaa (wakati ule walikuwa wagonjwa wachache, pasi na kifo chochote).

Wengi wa kundi hilo la wamatumbi wenzetu hawakuelewa...wao kwa kuwa tu China na Iran ndio wanashambuliwa zaidi na korona waliendelea kufurahi huku baadhi yao wakijitapa kuwa sisi waafrika korona haifui dafu, miili yetu iko ngangari.

Naam, muda ni mwalimu mzuri. Leo korona inawatesa hadi US. Wapendwa wao wapukutika. Mwanzoni Trump aliudogesha ugonjwa na kuufananisha na vijimafua tu. Ila sasa ni tofauti. Pia sisi wamatumbi tuliokuwa tukipiga tambo kubwa kuwa miili yetu corona haiambulii kitu, tumeanza kushuhudia visa vya korona kwa nchi kadhaa za Afrika, tena wamo wamatumbi wenzetu wanaougua.
Sasa twazungumza lugha moja; corona ni janga la dunia, haichagui haibagui utaifa.

Funzo:
Tusipende kufurahia majanga yawapatapo wenzetu, hata kama twawaona ni mahasimu wetu au (mahasimu) wa rafiki zetu.
View attachment 1396708
Trump alikuwa akiwadhihaki Wachina na kuponda utawala wao namna ulivyokuwa unapambana na Corona, USA sasa analia vifaa hakuna vya kutosha, vitanda vya wagonjwa mahututi havitoshi wao ubabe wao huwa ni wa kwenda kuiba rasilimali kwenye nchi zingine
 
babumapunda

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
4,605
2,000
tuchape kazi....watanzania chapeni kazi mjenge uchumi wenu hii corona sisi hitatusumbua
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom