Inawezekana kabisa kuwa kuna sababu nyinginezo zilizofanya uchumi wa marekani uyumbe, ila mimi nadhani kuwa hamu ya wamarekani ya kuwa na serikali inayozuia abortion rights na gay marriage ndizo zilizolifikisha taifa hili hapa. Serikali hii ya sasa iliingia madarakani kwa kete hiyo na ndiyo imevuruga uchumi huu kutoka kwenye budget ya sulplus hadi kuwa budget ya deficit.
Hebu nipeni pole ndugu zanguni. Nilikuwa na stocks 850 za benki moja inaitwa New Century nilizokuwa nimenunua kwa dola 20 kila moja. Stocks zile zikafanya vizuri sana na kukua hadi dola 120 na kitu. Kuelekea mwishoni mwa spring semester, nikawa buzy na mambo ya shule nikawa mzembe wa kushindwa kuangalia mwenendo wa stock kwa siku nne mfulilizo. Siku ya tano nikakuta stock zile zimeanguka kutoka dola 120 hadi dola 5. Nikadhani ni shock tu, kesho yake nikakuta stock zimebaki dola mbili tu. Wakati huo swala la subprime lending likawa hot issue sana na kwa uchungu nikashsindwa kuuza stock zile. Leo hii stock zile zina thamani ya senti 0.01!!!!
...acha tuu,hapa nilipo kichwa kinazunguka naogopa hata kuchungulia portfolio yangu,najua 70%(networth) is gone since monday,na hili mortgage kila nikiamka linaelekea south,hii crisis imepiga pabaya sana...wabongo nyumbani msifikiri mko safe ngojeni ianze kuwachapa sawasawa huko ndio mtatia akili na soon mtaipata tuu maana naona wengine naona mmefurahi!