Urusi Yawafanyia 'Kitu Mbaya' Mabalozi wa Marekani na Uingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urusi Yawafanyia 'Kitu Mbaya' Mabalozi wa Marekani na Uingereza

Discussion in 'International Forum' started by Saint Ivuga, Aug 11, 2009.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,407
  Trophy Points: 280
  Baada ya mwanadiplomasia wa ubalozi wa Uingereza nchini Urusi kunaswa kwenye mtego wa warusi akijivinjari na makahaba wawili wa Urusi na video yake kuanikwa magazetini mwezi uliopita, safari hii zamu imekuwa kwa mwanadiplomasia wa Marekani ambaye naye amenaswa akijiachia na mmoja wa makahaba wa nchini Urusi. Mwanadiplomasia wa ubalozi wa Marekani nchini Urusi, Kyle Hatcher amenasa kwenye mtego wa warusi na video yake wakati akifanya mapenzi na kahaba wa Urusi iliyochukuliwa kisiri imeanikwa kwenye magazeti karibia yote ya nchini Urusi.

  Mwanadiplomasia huyo ambaye hivi sasa ameingia matatani akiwa na kazi ya kujielezea vizuri kwa mkewe, amedaiwa na magazeti ya Urusi kuwa ni jasusi wa siri wa CIA.

  Mwezi uliopita, mwanadiplomasia wa Uingereza aliyekuwa akifanya kazi kwenye ubalozi wa Uingereza nchini Urusi, James Hudson, alinyang'anywa wadhifa wake na kurudishwa Uingereza na wizara ya mambo ya nje ya Uingereza baada ya mwanadiplomasia huyo naye kunasa kwenye mtego wa Warusi na video yake wakati akifanya mapenzi na makahaba wawili kuanikwa kwenye magazeti ya Urusi.

  Katika video ya mwanadiplomasia wa Marekani yenye dakika nne na sekunde 11 inamuonyesha Kyle mwenye umri wa miaka 35 akifanya mapenzi na mwanamke mmoja raia wa Urusi.

  Video hiyo inamuonyesha Kyle akiwapigia simu wanawake watatu wa Urusi na kupanga kukutana nao kwenye chumba kimoja.

  Kyle ili kujilinda na mitego ya warusi anaonekana akikifanyia uchunguzi chumba hicho kugundua kama kina kamera ya siri.

  Hata hivyo Kyle alishindwa kuigundua kamera ya siri iliyowekwa kwenye chumba hicho na matokeo yake mchezo mzima wa 'malavidavi' ulinaswa na kamera hiyo.

  Magazeti ya kila siku ya nchini Urusi karibia yote yaliandika habari ya video hiyo yakiwa na vichwa vya habari vya kumponda mwanadiplomasia huyo.

  Ubalozi wa Marekani nchini Urusi haujasema chochote kuhusiana na video hiyo na haijulikani kama Kyle ataendelea na kazi au atarudishwa Marekani.
  source nifahamishe
   
 2. D

  Darwin JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hahaaa thought for a moment it may have been Bill Clint ---- AGAIN!
  Sorry, Bill! Ahem!
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Tit for tat!

  Hakuna aliye mkamilifu..ni vema tu watu wakaheshimiana!
   
Loading...