Urusi yakataa ombi la Irani kuuziwa mfumo wa ulinzi wa makombora wa S-400

Najua watu wenye chuki na uislam watanasibisha hili na uislam.ilhal hao watu wana maslahi Yao ya kidunia.
Lakin kumkatalia Iran kutokupata huo mfumo wa ulinzi wa s-400 hakumfanyi yey kuwa Dhaifu Iran still are greatest kashindwa Bush akisaidiwa na Saddam Hussein kuiangusha Hajem ataweza trump na putin aah wapi
Urusi Yakataa Ombi La Irani Kuuziwa Mfumo Wa Ulinzi Wa Makombora Wa S-400

Urusi
imekataa ombi la Irani kuuziwa mfumo wa ulinzi wa anga wa S-400, kukiwa na wasiwasi kuwa uuziwaji huo ungeweza kuongezeka zaidi mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati.

View attachment 1112962

Ombi hilo lilikataliwa na Rais Vladimir Putin, kwa kile kinachoelezwa kuwa, kwa kukubali ombi hilo la Irani huenda kungechochea zaidi mivutano na migogoro katika eneo la Mashariki ya Kati. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alitembelea Moscow Mei 7.

Mauzo ya mifumo hii ya Makombora yamekuwa na utata katika Mashariki ya Kati huku Uturuki, mwanachama wa NATO na mshirika wa Marekani, akihatarisha hatua za adhabu za utawala wa Trump kwa kukubali kununua mitambo hiyo.

View attachment 1112997
Rais wa Urusi, Vladimir Putin akiendesha mkutano wa kijeshi wa maswala ya anga huko Sochi, Urusi, Mei 15, 2019. (Reuters)

Mgomo wa Urusi kwa ombi la Irani unaonesha uwiano wa kinguvu katika Ghuba ya Uajemi, ambako kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya Jamhuri ya Kiislamu kwa upande mmoja, na Umoja wa Mataifa na washirika wake wa Ghuba ya Uarabu kwa upande mwingine. Rais Donald Trump alikubali mwezi huu kutuma majeshi zaidi katika eneo hilo ikiwa ni baada ya Marekani kudai Irani kuhusika kwenye mashambulizi ya mitambo ya mafuta ya Saudia pamoja na meli nne.

Viongozi wa Irani wamekana kuhusika kwa Irani katika mashambulizi hayo.

Kuimarisha Uhusiano

Urusi na Irani wamekuwa na uhusiano wa karibu wa kisiasa na kijeshi katika miaka ya hivi karibuni, ingawa kuna ishara kwamba Moscow inatafuta kupunguza hatua za Iran katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwa ni kutafuta kulinda uhusiano wake na mamlaka nyingine za kikanda kama Saudi Arabia na Israeli.

"Uimarishaji wowote wa kweli au wa kufikirika wa Irani unaweza kusababisha ongezeko - ikiwa Urusi imeikatalia Irani ombi kama hilo, inamaanisha kuwa Urusi inataka kuendelea kufanya kazi katika mahusiano na Saudi Arabia, Israeli na kuweka fursa ya mazungumzo na Trump," Ruslan Pukhov, mkuu wa Kituo cha Uchambuzi wa Mikakati na Teknolojia huko Moscow, alisema. "Ikiwa Urusi itaamua kuipatia Irani Mifumo ya S-400, itakuwa changamoto moja kwa moja kwa Saudi Arabia na Israeli, hivyo itakuwa kinyume na maslahi ya kitaifa ya Urusi."

Urusi ni mojawapo ya nchi zinazotetea mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 na Irani, ambapo Marekani iliachana nao mwaka jana kabla ya kurejesha vikwazo vya kiuchumi kwa Irani. Nchi hizo mbili pia zilimsaidia Rais wa Syria Bashar al-Assad kurejesha udhibiti wa maeneo karibia yote ya Syria baada ya miaka minane ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilisababisha mamia ya maelfu ya watu kupoteza maisha.

S-400 ni Mfumo wa Makombora wa Ulinzi wa Anga ambao unauwezo wa kulenga shabaha katika umbali wa hadi kilomita 400 (maili 249).

Chanzo: The Moscow Times::Russia Rejected Iran S-400 Missile Request Amid Gulf Tension
 
Usiropoke we mtoa usingizin hv historia ya wahajem unaifuatilia vzur.
Hv unajua kilichomfanya Bush aishindwe Iran.
Km hawawez mbona wana wana inteligensia wao wa kutengeneza nuclear weapons embu nenda kisom usiishi kwa kasumba kijana
Watu acheni propaganda. Iran hana uwezo wa kutengeneza silaha yenye kiwango kama hicho.

Haya mambo ya technology yanaendana zaidi na kipawa cha asili "Nature Talent" na kwa mantiki hiyo Iran wana "Capacity Limitation". Ingekuwa rahisi hivyo basi hata sisi tungezitengeneza hata pale Morogoro au Mbeya.
 
Jinga ww, sisi unatufananisha na Iran, urusi amewezaje kama binadamu, then wengine washindwe dada angu
Usiende mbali muulize North korea kwa kijogoo kim wale wanatengeneza makombora tofaut tofaut had ya nuclear wale nao wana capacity limitation.tena makombora yake mpk trump yanamtetemesha mwambie asiishi kwa kasumba huyo
 
hivi humu jf hakuna wairan watupatie maoni yao kuhusu hii issue ya makombora maana naona sisi wabongo tunadanganyana tu
 
Waislam humu hali ngumu leo, mrusi kamkatalia Muislam kumuuzia S-400 basi roho zimewaumaa kama ni haki yenu vile.. Haaa, Mrusi na Mu Israel ni kitu kimoja, don't waste your time even to think
Mashoga humu leo wanasherehekea
 
Sasa wanataka kununua kumbe uwezo wa kutengeneza wanao. Watakuwa ni majuha wakutupwa.
Sasa wewe ndo huna akili hivi hujawah kuona nchi ikizuiwa au kunyimwa kitu fulani wanakaa chini wanawaza watafanyaje???mwisho wa siku wanapata mbadala???
 
Watu acheni propaganda. Iran hana uwezo wa kutengeneza silaha yenye kiwango kama hicho.

Haya mambo ya technology yanaendana zaidi na kipawa cha asili "Nature Talent" na kwa mantiki hiyo Iran wana "Capacity Limitation". Ingekuwa rahisi hivyo basi hata sisi tungezitengeneza hata pale Morogoro au Mbeya.
Wewe ni zero kbs iran mifumo mingi ya ulinzi katengeneza mwenyewe hebu pita hapa
 
Putin kahofia maisha yake, kwani Israel ingemfanya kitu hajawahi ona yeye binafsi, Netanyahu alienda Moscow na kumwambia ukiwauzia Iran S-400 jua umetangaza vita vikuu na Israel, na Putin akabaki kutoa macho tu, anajua Israel ni nani.. Maana S-300 waliouziwa Syria inapigwa na kuchakazwa kila siku na Israel AirForce wanaichezea kama toy vile yaani, tokea S-300 iende Syria imebakia kama sanamu la maonyesho tu.. Syria wanashangaa tu..!!
Kwa taarifa yako hiyo ni fake news hata urusi wamekanusha
 
Putin kahofia maisha yake, kwani Israel ingemfanya kitu hajawahi ona yeye binafsi, Netanyahu alienda Moscow na kumwambia ukiwauzia Iran S-400 jua umetangaza vita vikuu na Israel, na Putin akabaki kutoa macho tu, anajua Israel ni nani.. Maana S-300 waliouziwa Syria inapigwa na kuchakazwa kila siku na Israel AirForce wanaichezea kama toy vile yaani, tokea S-300 iende Syria imebakia kama sanamu la maonyesho tu😅😅.. Syria wanashangaa tu..!!
ACHA UMBEA WEWE
 
Tanzañia tuna nunua hii
18556417_1179114118882411_4531944084065002948_n.jpeg
 
Mbona nchi nyingi tu zinanunua silaha wakati uwezo wa kutengeneza wanao. Hata israel wana air defense za mmarekani wakati wao wanaweza kutengeneza za kwao.
wanaotengeneza Silaha duniani za first class ni only russia na america...na sababu ni kwamba wao ndio waliibuka washindi wa WW2 baada ya kumuangusha Hitler. ukiacha hao wababe wawili wengine bado wanajaribu...kama Iran ndo bado kabisa yeye kajiweka kipropaganda zaidi...military technology sio kitu cha kulala na kuamka...ni investment ya muda mrefu
 
Putin kahofia maisha yake, kwani Israel ingemfanya kitu hajawahi ona yeye binafsi, Netanyahu alienda Moscow na kumwambia ukiwauzia Iran S-400 jua umetangaza vita vikuu na Israel, na Putin akabaki kutoa macho tu, anajua Israel ni nani.. Maana S-300 waliouziwa Syria inapigwa na kuchakazwa kila siku na Israel AirForce wanaichezea kama toy vile yaani, tokea S-300 iende Syria imebakia kama sanamu la maonyesho tu.. Syria wanashangaa tu..!!
Israel wa kuwatisha warusi?
 
Putin kahofia maisha yake, kwani Israel ingemfanya kitu hajawahi ona yeye binafsi, Netanyahu alienda Moscow na kumwambia ukiwauzia Iran S-400 jua umetangaza vita vikuu na Israel, na Putin akabaki kutoa macho tu, anajua Israel ni nani.. Maana S-300 waliouziwa Syria inapigwa na kuchakazwa kila siku na Israel AirForce wanaichezea kama toy vile yaani, tokea S-300 iende Syria imebakia kama sanamu la maonyesho tu😅😅.. Syria wanashangaa tu..!!

Wayahudi ni nguzo muhimu ktk viwanda vya silaha vya Urusi na US. Kwa asili ya myahudi hawezi acha kusapoti taifa lake, hivyo Israel wako well informed na technologia za silaha, warusi na wamarekani wanajua, na ndio maana wana makubaliano yao wanayoyajua wao.

Mrusi isingekuwa rahisi kudai hawezi kwenda kinyume na maslahi yake!
 
wanaotengeneza Silaha duniani za first class ni only russia na america...na sababu ni kwamba wao ndio waliibuka washindi wa WW2 baada ya kumuangusha Hitler. ukiacha hao wababe wawili wengine bado wanajaribu...kama Iran ndo bado kabisa yeye kajiweka kipropaganda zaidi...military technology sio kitu cha kulala na kuamka...ni investment ya muda mrefu
Germany, uk, ufaransa, italy na nchi nyingi tu zinauwezo wa kutengeneza silaha yotote wanayotaka ila hawajawekeza sana kwenye majeshi yao kama us na russia. Russia wenyewe kuna technology nyingi tu ambazo bado hajazifikia nchi za ulaya. Mfano russia walikua wanataka kununua aircraft carrier mbili kutoka ufaransa ila baada ya vikwazo vya Ukraine wakauziwa misri. Usa wenyewe wananunua silaha kutoka israel. Kuna nchi zinanunua silah hata kama uwezo wa kutengeneza wanao wanao.
 
Usiropoke we mtoa usingizin hv historia ya wahajem unaifuatilia vzur.
Hv unajua kilichomfanya Bush aishindwe Iran.
Km hawawez mbona wana wana inteligensia wao wa kutengeneza nuclear weapons embu nenda kisom usiishi kwa kasumba kijana
Usually, comments based on religious fanaticism will not make you reason objectively.
 
Back
Top Bottom