Urusi yakataa kushirikiana na Taliban kuwaua wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,566
Kremlin nayo yapinga madai ya New York Times kuhusu mauaji ya wanajeshi wa Marekani huko Afghanistan
Jun 30, 2020 02:29 UTC
Dmitry Peskov
Dmitry Peskov
Msemaji wa Ikulu ya Rais wa Russia, Kremlin, amesema kuwa madai yaliyotolewa na gazeti la New York Time kwamba Moscow imeshirikiana na wapiganaji wa kundi la Taliban kuwaua wanajeshi wa Marekani huko Afghanistan ni ya uongo.

Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari mjini Moscow kwamba madai hayo yaliyotolewa katika ripoti ya gazeti la New York Times hayajawahi kujadiliwa katika mazungumzo ya Rais Vladimir Putin na mwenzake wa Marekani, Donald Trump.

Peskov ameeleza kusikitishwa na tabia na gazeti hilo la Marekani katika miaka ya hivi karibuni ya kukimbilia kuandika ripoti za uongo na kusisitiza kuwa, suala hilo linashusha chini hadhi ya chombo hicho cha habari.

Ijumaa iliyopita gazeti la New York Times lilidai kuwa timu isiyojulikana ya maajenti wa jeshi la Russia ililihamasisha kundi la Taliban kuwaua wanajeshi wa muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani nchini Afghanistan.

Wanajeshi wengi wa Marekani wameuawa nchini Afghanistan
Ripoti iliyoandikwa na gazeti la gazeti hilo imedai kuwa, Russia ilitoa kitita cha fedha kwa wapiganaji wa kundi la Taliban na kuwahamasisha kuwashambulia na kuwaua askari wa nchi za Magharibi wakiwemo wanajeshi wa Marekani na Uingereza huko Afghanistan.

Mwaka 2001 Marekani na waitifaki wake walituma vikosi vya jeshi katika ardhi ya Afghanistan kwa kisiingizio cha kukabiliana na ugaidi na kurejesha amani nchini humo. Hata hivyo tangu wakati huo uzalishaji wa dawa za kulevya umeongezeka sana nchini Afghanistan na machafuko na mashambulizi ya kigaidi vinaendelea kuchukua roho za makumi ya maelfu ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo licha ya kuwepo maelfu ya majeshi ya nchi za Magharibi nchini Afghanistan.
 
Karibu wananchi milioni 30 wa Russia ni masikini wa kutupwa lkn hali yao hiyo: is not Kremlin's source for concern...!!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom