Urusi yaionya Nato isijaribu kufanya uchikozi wowote

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,566
Russia yaionya NATO isijaribu kufanya chokochoko zozote dhidi yake

Russia yaionya NATO isijaribu kufanya chokochoko zozote dhidi yake
Baraza la Usalama wa Taifa la Russia limelionya Shirika la Kijeshi la NATO lisijaribu kuanzisha chokochoko zozote katika eneo la maji linalopakana na nchi hiyo.

Baraza la Usalama la Russia limesema, nchi wanachama wa NATO zinatumia vyombo vyao vya majeshi ya majini kama wenzo wa kuishinikiza Russia na kuanzisha chokochoko dhidi ya nchi hiyo na likaongeza kuwa, Moscow itatumia mbinu kali kabisa kutoa jibu dhidi ya chokochoko na hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi yake.

Bahari Nyeusi ndilo eneo kuu la makabiliano kati ya Russia na Magharibi.

Vikosi vya wanamaji vya shirika la kijeshi la NATO vinaendelea kuwepo muda wote katika eneo la maji ya Bahari Nyeusi; na kila mwaka hufanya mazoezi mbali mbali ya kijeshi kwenye pwani za Georgia na Ukraine huku Russia ikitazamwa na kuchukuliwa kama adui wa asili.

Katika miaka ya karibuni, na kwa kutoa kisingizio kwamba Moscow inatoa vitisho dhidi Magharibi, NATO imepanua mno wigo wa kuwepo kwake karibu na ardhi ya Russia na maeneo yanayopakana na nchi hiyo.

Uhusiano wa Magharibi na Russia umeharibika tangu mwaka 2014 katika nyuga nne za kupanuka kwa ushawishi na satua ya NATO na hasa Marekani katika maeneo ya karibu na Russia na mashariki ya Ulaya, mgogoro wa Ukraine, Bahari ya Baltiki na kuhusiana na kadhia ya Syria.../
4by379bea58a761woup_800C450.jpg
 
With a poor economy, Russia is a paper tiger 🐅 and it cannot endure a protracted combat with the tenacious Nato.
May be you are a toddler other wise tell your NATO fans to touch the bear's whisk, NATO was formed as a military coalition vs Russia. If Russia is that feeble as you have stressed why military and economic powers like USA, Canada, Japan, Europe etc made a military coalition vs her? Wazungu wote wanatambua kuwa Russian powerful kantri lakini wewe wa kwa mfuga mbwa ndo unaona Urusi dhaifu pole sana.
 
With a poor economy, Russia is a paper tiger 🐅 and it cannot endure a protracted combat with the tenacious Nato.
Are you sure? Can America really launch a war against Russia or even China?
 
Back
Top Bottom