Urusi yaijibu Marekani kwa kuwatimua wanadiplomasia wake

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Urusi imewataka wanadiplomasia 10 wa Marekani kuondoka nchini humo katika hatua ya kulipiza kisasi baada ya Marekani kuwafukuza wanadiplomasia 10 wa Urusi kwa madai ya udukuzi na kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka uliopita.

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema John Sullivan, ambaye ni balozi wa Marekani nchini Urusi, anapaswa kurudi nyumbani katika kile walichosema ni kwa mashauriano zaidi.

Kupitia taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema huu ni wakati wa Marekani kuonyesha ukomavu wake wa kiakili na kugeuza mkondo wao wa kugombana.

Taarifa hiyo imeongeza kusema kuwa ina uwezo wa kuiumiza zaidi Marekani kuichumi na kupunguza idadi ya wanadiplomasia wa Marekani nchini Urusi hadi 300, japo kwa sasa haitachukua hatua hiyo.

Uamuzi wa Urusi, ukiwa sehemu ya mpango mpana wa kulipiza kisasi, uliidhinishwa na Rais Vladimir Putin kama jibu kwa Marekani baada ya serikali ya Joe Biden kuiwekea vikwazo Urusi.

Hata hivyo licha ya Moscow kujibu kwa haraka na kuweka hatua ambazo zinanuia kupunguza ushawishi wa Marekani nchini Urusi, Urusi imeacha mwanya wa mazungumzo uliopendekezwa na Rais Joe Biden aliyetaka kufanyika mkutano kati yake na Putin ili kujadili masuala kadhaa.

Marekani imeituhumu Urusi kwa udukuzi na kuingilia uchaguzi wake
Marekani imesema vikwazo ilivyoiwekea Urusi ni jibu lake kwa Urusi baada ya Moscow kuingilia uchaguzi wa mwaka jana wa Marekani, kufanya udukuzi, na kuitishia Ukraine pamoja na vitendo vyengine.

Hata hivyo, Urusi imekanusha madai yote dhidi yake.

Vile vile, Ikulu ya Kremlin imesema Rais Putin bado hajaamua iwapo atashiriki katika mkutano wa kujadili athari za mabadiliko ya tabia nchi unaoongozwa na Marekani wiki ijayo.

Kremlin pia imeongeza kusema, itakuwa vigumu kuandaa kwa haraka mkutano wa kilele baina ya Putin na Biden.

Msemaji wa Ikulu Dmitry Peskov alisema jana Ijumaa kuwa Putin kwa muda mrefu amezungumzia juu ya umuhimu wa kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya Marekani na Urusi.

Peskov alisema "Ni vizuri kuwa viongozi hao wawili wamekubaliana juu ya hili." Hata hivyo, msemaji huyo ameshtumu vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani, akisema "uraibu wa vikwazo vya Marekani haukubaliki."

Uhusiano kati ya Urusi na Marekani umetetereka katika siku za hivi karibuni baada ya Rais Biden kusema kuwa anadhani Putin ni "muuaji" na Moscow kujibu kwa kumuita nyumbani balozi wake anayehudumu nchini Marekani mnamo mwezi Machi. Balozi huyo bado hajarudi Marekani karibu mwezi mmoja baadaye.
 
Taarifa hiyo imeongeza kusema kuwa ina uwezo wa kuiumiza zaidi Marekani kuichumi na kupunguza idadi ya wanadiplomasia wa Marekani nchini Urusi hadi 300, japo kwa sasa haitachukua hatua hiyo.
 
Sawa dada. Jifunze kuandika maneno ya lugha ya kiswahili kwa ufasaha maana hauna tofauti na mtoto anayesoma chekechea au darasa la kwanza. Tunapoelekea lugha ya kiswahili itapoteza hadhi yake kwasababu ya kuwepo kwa watu wajinga wasiojua kuandika maneno ya lugha ya kiswahili kwa ufasaha.
Utakuta huyu naye anaitwa mama. Inashangaza sana
Akili ✔
Akiliiiiiii ❌
Ndiyo ✔
Ndio ❌
Hapo ndio unaona umetumia akiliiiiii
😀 😀😀 vituko haviishi duniani.
 
Ninachokiona hapa ni Marekani kuzidi kuonekana kuwa si chochote kwa Urusi na kupoteza ile heshima yake ya maamuzi duniani. Urusi ilimzuia kumpindua Assad,ikamzuia kumpindua rais wa Venezuela, ikatwaa Crimea kwa nguvu bila Marekani kupenda leo hii kalipizwa sawa suala lakufukuza wanadiplomasia. Biden angeachana na Mambo ambayo yanaendelea kuipotezea heshima nchi yake.
 
Sawa dada. Jifunze kuandika maneno ya lugha ya kiswahili kwa ufasaha maana hauna tofauti na mtoto anayesoma chekechea au darasa la kwanza. Tunapoelekea lugha ya kiswahili itapoteza hadhi yake kwasababu ya kuwepo kwa watu wajinga wasiojua kuandika maneno ya lugha ya kiswahili kwa ufasaha.
Utakuta huyu naye anaitwa mama. Inashangaza sana
Akili ✔
Akiliiiiiii ❌
Ndiyo ✔
Ndio ❌
Ina sasa unaanza kuwa mwalio.
Hivi unajua tofauti ya Ndiyo na Ndio!?
Ndiyo ni jibu, kwa kingereza inatwa YES.
Ndio kwa kingereza THAT.

Jifunze kiswahili kijana.
 
Sawa dada. Jifunze kuandika maneno ya lugha ya kiswahili kwa ufasaha maana hauna tofauti na mtoto anayesoma chekechea au darasa la kwanza. Tunapoelekea lugha ya kiswahili itapoteza hadhi yake kwasababu ya kuwepo kwa watu wajinga wasiojua kuandika maneno ya lugha ya kiswahili kwa ufasaha.
Utakuta huyu naye anaitwa mama. Inashangaza sana
Akili ✔
Akiliiiiiii ❌
Ndiyo ✔
Ndio ❌
Vilevile ninaendelea kukufundisha kiswahili.
Je, unakua Thamathali za semi.
Hapa tunaongelea Tanakali Sauti.
Hilo neno akiliiii! Ni tanakali sauti.
Umenielewa!?
 
Back
Top Bottom