KWELI Urusi yaanza mazoezi ya kutumia silaha za nyuklia, Aprili 20, 2022

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Urusi yaanza mazoezi ya kutumia makombora ya nyuklia ni saa chache baada USA kukubali kuipatia Ukraine makombora ya masafa marefu.

FUN908QWIAAuSO4.jpg
 
Tunachokijua
Bado mapigano ya kivita baina ya taifa la Ukraine na Urusi yanaendelea kushika kasi kila uchwao. Mataifa mbalimbali duniani yameendelea kujitokeza kuiunga mkono nchi ya Ukraine kwa kuipa misaada mbalimbali ikiwamo misaada ya silaha.

Je, ni kweli Urusi yaanza mazoezi ya kutumia silaha za nyuklia?
JamiiForums imefatila taarifa hii kutoka katika vyanzo vinavyoaminika na kubaini kuwa baada ya Marekani kupitisha azimio la kuisaidia Ukraine silaha, Serikali ya Urusi ilitangaza kuanza mazoezi ya matumizi ya mabomu ya nyuklia Aprili 20, 2022 kwa kuonesha uwezo wao baada ya taarifa kuwa taifa la Marekani kutaka kuisaidia roketi za kisasa jeshi la Ukraine ili kupambana na Urusi.

Mazoezi hayo yanahusisha makombora ya Balestiki ya Yars, ambayo ni kizazi kipya cha kombora kilichojaribiwa kwa mara ya kwanza mnamo 2007.

Jeshi la Urusi linasema kuwa mazoezi hayo yanayofanyika katika Mkoa wa Ivanovo karibu na Moscow yanahusisha wafanyakazi wa huduma 1,000 na zaidi ya magari 100.

Makombora hayatarushwa. Mazoezi hayo yanajumuisha doria, kuweka mifumo ya makombora na kuwalinda kutokana na mashambulizi.

Urusi na Ukraine zilianza kupigana Februari 2022 ambapo Urusi iliita suala hilo kama 'Operation Crimea'.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imetangaza kuanza kwa mazoezi ya kijeshi ya kile kinachoitwa Kikosi cha Makombora, Mazoezi hayo yalitangazwa saa kadhaa baada ya Marekani kusema kuwa itawapa Waukraine mifumo ya hali ya juu ya roketi, ingawa taarifa ya jeshi la Urusi kwa vyombo vya habari haikurejelea habari kutoka Washington.

Hivyo, kutokana na vyanzo hivi taarifa hii ni ya ukweli.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom