Urusi: Serikali yatangaza kuzima intaneti ili kujilinda na maadui

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
559
1,000
Serikali ya Urusi chini ya Rais Vladimir Putin inajipanga kuzima mtandao wa intaneti kwa muda, na hivyo kujitoa kwenye mawasiliano na dunia kama sehemu ya majaribio yake ya kujikinga dhidi ya mashambulio ya kimtandao.


Zoezi hilo litafanya mawasiliano baina ya raia na mashirika ya Urusi kubaki ndani ya nchi badala ya ya kupitia njia za kawaida za kimtandao kimataifa.

Rasimu ya sheria ya kuruhusu mabadiliko ya kiufundi ili kuiwezesha nchi hiyo kuendesha mtandao wake wenyewe iliwasilishwa bungeni mwaka jana.

Jaribio hilo linatarajiwa kufanyika kabla ya tarehe mosi Aprili, lakini siku rasmi ya kuzimwa mtandao haijatajwa.

Mvurugano mkubwa

Rasimu hiyo ya sheria, iliyopewa jina la Programu ya Taifa ya Uchumi wa Kidijiti, inawataka watoa huduma za intaneti nchini Urusi kuwa na uwezo wa kuendelea na huduma zao hata pale ikitokea nchi za kigeni zikiamua kuitenga Urusi.

Nchi wanachama wa Nato na washirika wake wamekuwa wakitishia kuiwekea vikwazo vya kimtandao Urusi ambayo wanaituhumu kwa kufanya mashambulio ya kimtandao.

Njia mojawapo inayopangwa na Urusi katika kujilinda huko ni kutengeneza mfumo wake binafsi wa anuani za kimtandao ufahamikao kama DNS, waweze kupata mawasiliano hata pale watakapotengwa ama kujitenga.
Kwa sasa, kuna taasisi 12 zinzoshughulikia suala la utolewaj na matumizi ya anuani hizo na hakuna hata moja iliyopo Urusi.

Hata hivyo tayari kuna chapa nyingi za mfumo huo wa DNS nchini Urusi hali inayoonesha kuwa nchi hiyo inaweza kuendelea na shughuli zake za kimtandao hata ikitokea imetengwa leo.

Watoa huduma za intaneti wanatarajiwa kuelekeza mawasiliano yote yanayopita kwao kwenye vituo vya serikali kwenye zoezi hilo. Mawasiliano yote ya ndani ya Urusi yataruhusiwa kuendelea lakini yale yatokayo nje ya nci yataminywa.

Mwishowe, serikali ya Urusi itakuwa na ubavu kama wa China wa kupanga mawasiliano gani raia wake wapate kutoka nje ya nchi.

Vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa watoa huduma za intaneti nchini humo wanakubaliana na mabadiliko hayo lakini wanatofautiana kwenye namna gani utekelzwaji wake uwe. Wanaamini jaribio hilo litazaa "mvurugano mkubwa" kwa matumizi ya mtandao ya nchi hiyo, umeandika mtandao wa ZDNet.

Serikali ya Urusi inawapa fedha watoa huduma ya intaneti nchini humo ili kuboresha miundombinu yao kuendana na mipango yake ya baadae.

Hata hivyo, kuna uwezekano wa watu kuchupa mazuio hayo ya serikali kwa kutumia mitandao binafsi (VPNs) - ambayo hudanganya mahala kompyuta ama simu janja ilipo na hivyo vidhibiti kushindwa kuzizui kupata mawasiliano yaliyokatazwa.

Hata hivyo, baadhi ya nchi kama China zimekuwa wakali kwa wale wanaotumia tenkolojia hiyo. Ukikutwa unatumia ama kusambaza bila kibali teknolijia hiyo nchini China unaweza kutupwa jela.

Mara chache, nchi hujikuta zimejitoa kwenye mawasiliano ya intaneti kwa bahati mabaya - ilitokea hivyo mwaka 2018 nchini Mauritania kwa siku mbili baada ya nyaya ya chini ya bahari inayopeleka mawasiliano hayo kukatika. Meli ya kuvua samaki inasadikiwa kusababisha ajali hiyo.
 

Sela Son

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
745
1,000
Kwa miaka mingi warussi wamekuwa wakijitahidi kufanya yao y'allo tofauti na west..hii Ni ili kuhakikishs usalama wao hauko rehani..na ndio Mana Leo Wana kompyuta zao,,Wana madege yao na hata social networks zao..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
6,185
2,000
Uzuri ni pale wnaposema Serekali itatoa fedha kwa watoa huduma binafsi ili kujidhatiti! Wameonyesha dhamira ya kweli..... Urusi anaziba mianya yote iliyokua inawafanya wanyanyasike mbele ya US &EU kaanza kwenye Mster card na Visa card sasa kahamia kwenye internet!
 

Cicero

JF-Expert Member
Jan 20, 2016
2,919
2,000
Watu wenye akili hao. Nchi za Afrika ukiziwekea vikwazo tu basi umewamaliza…..sio Russia!
 

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,257
2,000
Watu wenye akili hao. Nchi za Afrika ukiziwekea vikwazo tu basi umewamaliza…..sio Russia!
Kuna vitu huwa havikwepeki acha uzembe wewe hizo ni propaganda tu za kisiasa like kutishia... dot com haikwepeki
 

Cicero

JF-Expert Member
Jan 20, 2016
2,919
2,000
Kuna vitu huwa havikwepeki acha uzembe wewe hizo ni propaganda tu za kisiasa like kutishia... dot com haikwepeki
Hujaelewa hoja. Urusi haizimi mtandao ila inajichomoa kwenye mtandao wa dunia na kujijengea mfumo wake pamoja na exchange point yake. Bado Warusi watakuwa wanaweza kuingia mtandaoni ila data zote zitapitia kwenye seva zilizoko Urusi. Huwezi kuelewa hivi vitu vinahitaji akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
5,671
2,000
Kwa miaka mingi warussi wamekuwa wakijitahidi kufanya yao y'allo tofauti na west..hii Ni ili kuhakikishs usalama wao hauko rehani..na ndio Mana Leo Wana kompyuta zao,,Wana madege yao na hata social networks zao..

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli mkuuu. Mmarekani bado anategemewa sana na dunia nzima
Mfano wa utegemezi wa kampuni izo ni:-
1. Coca cola
2. Email address (Gmail account, Yahoo account, rocket mail na nyingine
3. Facebook
4. WhatsApp
5. Twitter account
6. Kampuni za kuzalisha wazazi wa kuku wa Layers na broillers
7. Makkampuni ya dawa za binadamu
8. Mengine ongezeeeni
 

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,257
2,000
Hujaelewa hoja. Urusi haizimi mtandao ila inajichomoa kwenye mtandao wa dunia na kujijengea mfumo wake pamoja na exchange point yake. Bado Warusi watakuwa wanaweza kuingia mtandaoni ila data zote zitapitia kwenye seva zilizoko Urusi. Huwezi kuelewa hivi vitu vinahitaji akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndio unahitaji akili kuelewa hizi majigambo... Internet inavitu vingi na huwezi kuvitenganisha ukiingia umeingia wanadunia watakupata tu labda uzime... Mada ni Urusi inataka kujitenga na Internet wewe unaleta Ujinga mpya.
 

jazari

Member
Sep 9, 2018
73
125
Wewe ndio unahitaji akili kuelewa hizi majigambo... Internet inavitu vingi na huwezi kuvitenganisha ukiingia umeingia wanadunia watakupata tu labda uzime... Mada ni Urusi inataka kujitenga na Internet wewe unaleta Ujinga mpya.
Kasome tena Na utafakari!!! Kilicho semwa kuwa cio kwamba anajitenga na internet bl anataka kujitoa kwenye mfumo WA internet WA kidunia ili kulinda Usalama wake Na vile vile kuna vitisho vya vikwazo vya kimtandao kwaiyo kufikia mpk April watakua wana kamilisha mfumo wao wa internet ambao saver zote zitapitia urusi lkn kwa watu wake wataweza pata taarifa za dunia ht km watakua na vikwazo vya kimtandao kupitia Mfumo mazubuti DNS ambao taarifa zote za kimtandao za ndan ya urusi zitabakia urusi Na urusi itakua na mamlaka za taarifa kutoka nje zp zina faa kwa watu wake kuzipata kwaiyo atajitegemea mwenyewe kima mambo ya kimtandao

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom