Urusi salama ipo mikononi mwa ardhi ya Ukraine

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
URUSI SALAMA IPO MIKONONI MWA ARIDHI YA UKRAINE.

Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Tuesday- 7/05/2022
Marangu Mtoni, Kilimanjaro - Tanzania

Unataka kujua kwanini Urusi anaitaka Ukraine?, Ok twende pamoja...

Urusi na Ukraine wana historia moja toka mwanzo, historia yao inafanana kwa kila kitu, ni damu moja, jamii moja na kabila Moja, ni watoto wa baba mmoja, damu yao ni kutoka kwa babu yao Rurik of Ladoga.

Wote ni jamii ya Slavs kutoka Kabila la Varangian, asili yao ni eneo la Vistula, eneo hilo la Vistula ni eneo la mpaka wa Poland, Sweden na Finland ya sasa, zamani iliitwa Ladoga, baadae ikaitwa Rus, kisha ikaitwa Kievan Rus, baada ya mgawanyo mwaka 1550 ikazaliwa Russia na Ukraine lakini Ukraine hii ya sasa ilianza kuibuka baada ya mkataba wa "Riga", ntaeleza hili huko mbeleni.

Lakini kubwa la kuzingatia hapa ni kuwa kati ya Ukraine na Urusi nchi ya kale zaidi ni Ukraine, Ukraine ndio mama wa Urusi, Urusi katoka tumboni mwa Ukraine, mji wa Kyiv (Kiev) ndio mji mkuu wa kwanza kuanza kabla ya Moscow, Russia (Urusi) kazaliwa baada ya Ukraine ya awali (Kievan Rus) kuparaganyika, yani kuvunjika.

Historia ya Ukraine na mji wa Kyiv inaanza toka karne ya 7 huku Russia ya sasa ni zalio la mfalme Ivan the great, karne ya 14, hili ntalieleza huko mbeleni.

Hawa ni damu moja, jamii moja na aridhi waliotoka ni moja.

Wote umtambua Rurik of Ladoga kama mwasisi wa aridhi zao, wote wanachangia historia moja ambayo iligawika mwaka 1240 baada ya uvamizi wa Mongols, tutaliona hili kwa kina huko mbeleni.

Hivyo basi.....

Mwasisi wao ni kiongozi aliyeitwa Rurik of Ladoga, alikuwa ni chifu wa jamii ya Warangian ambaye mwaka wa 862 AD alivamia na kutawala kabila la Novgorod.

Akatanua himaya na kutawala eneo lote lilokaliwa na Slavs, huyu Rurik ndie anachukuliwa kama mwanzilishi wa nasaba ya Rurikid, iliyotawala himaya ya Ladoga, ambayo kwa sasa ndio zilipo nchi za Russia, Ukraine, Beralus, Poland, Estonia na ukanda wote wa Ulaya ya kati.

Rurik alianzisha dola ya Novgorod ambayo ndio baadae ilikuja kuitwa Kievan Rus, yani Ukraine na Russia ya sasa.

Kulingana na simulizi kutoka jamii za Radzivil na Hypati inaeleza kuwa miaka ya 862 mpaka 864, kikundi kikubwa cha wahaimiaji kutoka Sweden (viking) ya sasa waliweka makazi eneo la Ladoga wakiongozwa na Rurik, Rurik akaongoza vikosi kuvamia Novgorod, wakajenga ngome eneo hilo karibu na Mto Volkhov.

Rurik aliongoza uvamizi na kuteka maeneo yote kuzunguka mto Volkhov mpaka eneo la Volhynia, mfalme Rurik alisalia madarakani hadi mwaka wa 879 alipo fariki dunia.

Rurik of Ladoga alifariki kifo cha kitandani mwaka 879, kabla ajafariki Rurik alitoa wosia kuwa ufalme wake uende kwa rafiki yake Oleg, ambaye atatakiwa kumlea mwanae wa kiume Igor, kwa kuwa kipindi hicho mwanae Igor alikuwa bado mdogo sana.

Oleg alipochukua madaraka akahamisha mji mkuu kwenda Kiev (Kyiv) baada ya kufanya uvamizi na kuwashinda wenyeji na kuwaua watawala wa eneo hilo na kuanzisha himaya ya Kievan Rus, himaya hiyo ilitawala eneo hilo mpaka Igor alipokuwa mkubwa.

Igor the Old alichukua madaraka na kueneza utanuzi wa himaya ya Kievan Rus kuelekea kusini mwa mto Desna, yeye ndio alijenga ngome za kusini kuwadhibiti wafanya biashara wa Scandinavia kuvamia himaya yake, baada ya Igor the Old kufariki mwaka 945 ufalme na utawala ukaenda kwa mwanae Olga.

Huyu Olga ndio hufahamika kama Olga the Kiev, yeye ndio mwenye historia ya kuijenga jiji la Kyiv, ukifika kaskazini mwa jiji la Kiev kuna sanamu refu la mwanamama ambalo ndio refu kuliko sanamu zote kwenye jiji hilo, sanam lile huitwa saint Olga.

Baada ya kifo cha mfalme Olga madaraka yakarithiwa mwaka 925 na Sviatoslav the Brave, huyu alikuwa jemedari Mkuu wa Kiev, ni moja ya wafalme maarufu wa dola ya Kievan Rus, umaarufu wake unatokana na kushinda vita nyingi za mashariki na kusini mwa Ulaya ambazo zilisababisha kuanguka kwa mataifa makubwa mawili ya Ulaya wakati huo ya Dola ya mwanzo ya Bulgaria na Dola ya Khazaria na Dola ya Kwanza ya mashariki Slavic, hawa slav wa mashariki ndio eneo la Poland ya sasa.

Baada ya kifo cha Sviatoslav the Brave ufalme ukaenda kwa mfalme Yaropolk I Sviatoslavich, mwaka 972 ambae alitawala mpaka mwaka 978 kisha akarithiwa na Vladimir the great, huyu mama yake alikuwa ni kutoka Nordic.

Nordic ni jamii ya norsemen au watu wa Norse hawa walikuwa ni kundi la jamii ya Germanic ambao walizungumza lugha ya Kale ya Norse.

Huyu Vladimir the great aliongoza vita na kuteka eneo la Belarus hadi Bahari ya Baltic na kuimalisha mipaka dhidi ya uvamizi wa Wabulgaria, makabila ya Baltic na wahamiaji wa Mashariki.

Ni kipindi chake ukristo uliingia Kievan Rus, alipokea Ukristo kutoka himaya ya Byzantine iliyo eneza ukristo wa Orthodox na yeye kuwa mkristo wa kwanza, Vladimir alikuwa mkristo mwaka 988 na akaifanya dola ya Kievan Rus' kuwa ya Kikristo, kwasababu hiyo mpaka leo hujulikana kama Mtakatifu Vladimir.

Kisha mwaka 1015 madaraka yakaenda kwa Sviatopolk the Accursed ambae alitawala mpaka mwaka 1019, na mrithi wake akawa Yaroslav the Wise ambae husifiwa kuyaunganisha upya koo zilizoanza kuparaghanyika kufatia mpasuko uliofanywa na baba yake Sviatopolk ambae aliupata ufalme kwa kumuua kaka yake olega the order.

Dola ya Kievan Rus iliendelea mpaka uvamizi wa vikosi vya Mongol vilipo vamia mwaka 1240.

Kwaiyo.....

Kama nilivyosema huko awali ni kwamba, Mababu wa Urusi na Ukraine walikuwa sehemu ya jamii ya slavic iliyoitwa Kieven Rus, Ilianzishwa na mfalme na chifu wa pili Oleg katika karne ya tisa.

Faith Hillis, Profesa wa historia ya Urusi kutoka Chuo Kikuu cha Chicago, anasema kwamba eneo la bahari ya baltic na bahari nyeusi, ilipo sasa Ukraine, iliishi jamii ndogo ya Slavs karibu miaka elfu iliyopita.

Jamii hizi ziliamua kuungana na kuunda nchi mpya chini ya uongozi wa wafanyabiashara wa Scandinavia wanaosafiri kutoka Scandinavia kwenda Byzantium kupitia mto Nipro, Nchi hii mpya iliitwa Kieven Rus na mji mkuu wake ulikuwa unaitwa Kiev ambao ni mji mkuu wa Ukraine sasa, Watu hawa wa Slavic hawakuwa raia wa Ukraine wala Urusi, Pia ilijumuisha jamii zisizo za Kislavoni kama vile jamii za makabila ya Orguz, Mongolis, Waislamu wa Iraq na India na wayahudi."

Tuendeleee Sasa....

Karne ya 13, jamii ya Mongols walivamia Kieven Rus, uvamizi huo ulifanyika Mei 31, 1223, Majeshi ya Mongol ya Genghis Khan yakiongozwa na kamanda Subutai yaliwashinda majeshi ya Kievan Rus' kwenye Vita iliyo piganiwa kwenye Mto Kalka.

Vita hivi vilikuwa ushindi mkubwa kwa Mongols katika kudhibiti ulaya ya kati, katika vita hii askali wengi wa Rus walipoteza maisha huku Mongol ikipata hasara ndogo.

Idadi kubwa ya watu wa Slavic hapa iligawanywa katika sehemu tatu kubwa, baadae mgawanyo huu ulizaa Urusi, Ukraine na Belarus ya sasa.

Katika karne ya 14, wakati Mongols inaanguka kufatia kuibuka kwa Dola ya Ottoman iliyoanzishwa na Mfalme Osman Ghazi, mwana wa Etugrul bey kutoka ukoo wa Orguz Ghazi mwasisi wa kabila la Kay na jamii ya Celjuk, huyu Orguz Ghazi ndio mwasisi wa nchi za Türkeye, Turkistan, na Uzbekistan (ntaeleza habari zake siku za usoni inshallah)

Tureje kwenye hoja yetu, baada ya kuanguka kwa Mongoli kulikuwa na tishio jingine la uvamizi wa mji wa Kiev, Poland ilikuwa inajiandaa kupanua mipaka yake na uongozi wake ulikuwa mikononi mwa wakoloni wa kirumi, Kumbuka Poland ndio walae Slavs wa mashariki (eastern Slav).

Faith Hillis anasema, "Poland na Lithuania waliungana katika karne ya 16 na kufahamika kama Kingdom of Poland and the Grand Duchy of Lithuania walianza kueneza himaya yao kuelekea eneo la kusini.

Himaya hii ilikuwa mojawapo ya nchi kubwa zaidi na yenye watu wengi zaidi Ulaya karne ya 16 hadi 17, ilikuwa na takriban kilomita za mraba 1,000,000 (400,000 sq mi) na mpaka kufikia mwaka 1618 ilikuwa na idadi ya watu karibu milioni 12.

Kingdom of Poland and the Grand Duchy of Lithuania iliundwa tarehe 1 July 1569 chini ya Mfalme wa kwanza Sigismund II Augustus of the first.

Hivyo dola hii ikaivamia Kievan Rus na mji wa Kiev ukawa chini ya utawala wa Poland-Lithuania.

Historia ya Urusi na Ukraine iliingia katika sura mpya tena katika mwaka 1462 pale mfalme Ivan lll au Ivan the great alipo anza kuikomboa tena Kievan Rus, alifanikiwa kuunda himaya ya Russia ya mashariki (moscovy).

Jina Russia na Belarus yanatokana na jina la Rus (kutoka kwenye jina Kievan Rus) hivyo Ivan the great akapendekeza eneo la mashariki alilolikomboa liitwe Russia (kutoka neno "Rus"), ndio maana yeye huitwa Ivan the Russia, sababu ndio mkombozi wa Russia ya pili baada ya ile ya Rurik of Ladoga na Oleg kufutika.

Ivan aliijenga Rus mashariki (Russia) kutoka kwenye dola ya Novgorod iliyokuwa chini ya Poland na Lithuania, hatimae mwaka 1470 baada ya vita vingi na kupata ushindi kwenye ile vita ya mto shelon (Battle of Shelon River) iliyopiganwa eneo la Dvina ilipelekea Navgorodians kusalim amri mwaka 1471.

Mpaka mwaka 1480 maeneo yote ya Kiev, Crimea, Lithuania mashariki ilikuwa imeshachukuliwa na Ivan the great, hali hii ikamfanya kufanikiwa kuunda himaya mpya ya Rus mashariki (Russia), Ivan the great hufahamika kama ndio mfalme aliyeifufua tena Kievan Rus.

Hivyo.....

Faith Hillis anaelezea, "hii ilikuwa hatua kubwa ya mambo kuanza kugeuka ambapo majadiliano juu ya masuala ya utaifa yalianza na yanaendelea mpaka katika zama za sasa".

Katika karne ya 14 mpaka 18, ulikuwa wakati Urusi ilipounda himaya ya warusi ikijumuisha sehemu ya mashariki ya Ukraine.

Jina la Ukraine au Kievan ya mashariki ilikuwa ikiitwa Novorasia yaani Urusi mpya, Wakati huo huo, sehemu ya upande wa magharibi ilibaki kuwa chini ya Austria na kisha baadaye chini ya utawala wa nasaba wa himaya ya Austro-Hungarian.

Mfalme wa Urusi (Tsar Aleksei Mikhailovich) akalitoa kama zawadi jimbo la Volinskaya kwa Ukraine mnamo mwaka 1654, kimsingi majimbo yote ya Ukraine ya sasa yani kuanzia mashariki, magharibi na kusini ni mali ya Urusi.

Mfalme Mikhailovich alifanya hivyo ili kuongeza urafiki na kupunguza uadui na Kievan ya magharibi.

Mipaka ya Ukraine ya sasa ipo kwa mujibu wa mkataba wa mipaka wa "Pereiaslav Treaty" wa mwaka 1654 chini ya Mfalme Mikhailovich, Haya majimbo yote Ukraine ilikuwa ikimegewa kidogokidogo kutoka katika himaya ya Urusi kama zawadi hadi hapo Ukreni ilipofika leo.

Mfano wa majimbo hayo ni pamoja na majimbo ya Kharkovsk Oblast, Lugantsk, Donetsk, Dnepropetrovstk, Zaparozhsk, Herisontsk, Nikolaevsk na Odesk.

Hata mwaka 1922, Vladimir Ilyich Ulyanov Lenin alilitoa kama zawadi jimbo la Kharkovsk kwa Ukraine, pia Khrushev Nikita akalitoa kama zawadi jimbo la Krimea mnamo mwaka 1954 kwa Ukraine, huku Joseph Stalin akitoa majimbo manne ya magharibi yaliyopo mpakani mwa Polandi kama zawadi kwa Ukraine majimbo hayo ni Livivska, Zakarpatiska, Ivan Frankoftsk na Chernovitsk.

Lakini Pamoja na yote historia ya nchi hizi inatuonesha kuwa himaya ya dola ilianzia Kiev mji mkuu wa Ukraine ya sasa kwa zaidi ya miaka 1600 na kisha himaya ikarudi Moscow yani Russia mwaka 1500 kipindi cha mfalme Ivan the great.

Hii inamaana kwamba mji wa Kyiv (au Kiev) ni mkongwe kuliko Moscow, Kyiv ndio baba wa Moscow, kwasababu Kiev ndio ulikuwa mji mkuu wa himaya ya Kievan Rus', mji wa Kyiv unatajwa kuanzishwa mwaka 482 AD.

Simulizi za kale zinasema kwamba wakazi wa kwanza kuishi Kyiv ni watu wanne ambao ni, Kyi, Shchek na Khoryv, na dada yao Lybid, hawa ndio wakaazi wa kwanza kabisa kuishi mji huo ukiwa pori na kichaka, aifahamiki hasa walitokea wapi, japo simulizi hutaja kuwa walitokea Poland, watu hawa ndio walio anzisha jiji hilo.

Kimsingi jina Kyiv, linatokana na jina la mkaazi kiongozi wa kwanza mjini hapo ambae jina lake ni Kyi, aliyekuwa kaka mkubwa wa miongoni mwa wakaazi wanne wa kwanza kufika hapo.

Taratibu kwenye vilima vya Mto Dnipro, kulianza kupokea wageni wahamiaji kutoka jamii za Slavic kutafuta makazi, hatua kwa hatua mji ukakuwa na mfalme Oleg alipo hamishia makazi ya dola hapo ukaifanya Kyiv kuwa kitovu cha ustaarabu wa Slavic Mashariki, chini ya dola ya Kievan Rus' katika karne ya 10-12.

Hivyo Kyiv ni moyo wa historia ya Ukraine na Urusi, bila Kyiv hakuna historia ya Ukraine wala Urusi, ndio maana wao wote wawili huita Kyiv Mama mtakatifu.

Sasa unaweza kuona ni kwanini Putin anaitaka Ukraine kuliko sehemu yoyote ile kwenye ustawi wa masrahi yake.

Urusi hii ya sasa ilanza kustawi tena baada ya Ivan the great na kustawi zaidi Ulaya kipindi cha utawala wa mfalme Peter the great, huyu Mfalme Peter ndio mwenye mji maarufu wa St Petersburg, mji huu ulipewa jina hilo kurejelea heshima ya Peter the great.

Huyu Mfalme Peter the Great alikuwa mfalme wa Utawala wa Urusi kuanzia tarehe 7 Mei 1682 hadi kifo chake kilipotokea mnamo mwaka 1725, Chini ya utawala wake ndie aliyoifanya Urusi kukua kisasa na kuwa na nguvu barani Ulaya.

Peter the great alishinda vita nyingi, ni yeye aliye kamata bandari ya Azov na Bahari ya Baltic, ambayo inamilikiwa na Urusi mpaka leo, aliongoza mapinduzi ya kiuchumi ambayo yalibadilisha baadhi ya mifumo ya kijamii na kisiasa ya Urusi na kupelekea mifumo ya kisasa ya maisha ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kisayansi.

Ni yeye aliye anzisha taasisi nyingi za serikali ya Urusi zinazofanya kazi mpaka leo, yeye ndie aliye anzisha na kuendeleza jiji la Saint Petersburg, ambao alihamishia makao makuu ya utawala wake kutoka Moscow na kulifanya jiji la St Petersburg kuwa mji mkuu wa Urusi hadi 1917 serikali ya Bolsheviks ilipo hamia Moscow tena.

Chuo kikuu cha kwanza cha Urusi cha Saint Petersburg State University kilianzishwa mwaka mmoja tu kabla ya kifo chake yani mwaka 1724, pia chuo cha pili kuanzishwa Urusi cha Moscow State University kilianzishwa miaka 30 baada ya kifo chake, lakini ilikuwa ni ndoto yake kuwa na chuo kikubwa Ulaya, ndoto hiyo ikatimizwa na utawala wa binti yake Elizabeth.

Ok, Tuenderee Sasa....

Mvutano wa kujenga himaya barani Ulaya kati ya mataifa ya Ulaya ulisababisha kutokea vita vya dunia mwaka 1914, Miaka minne baadaye, wakati vita vilipomalizika, hakuna aliyebaki salama, si Austro-hungary wala himaya ya Warusi iliyonusurika na madhara ya vita ya kwanza ya dunia.

Baada ya vita vya kwanza vya dunia na mapinduzi ya Urusi mwaka 1917 yalibadilisha ramani ya bara zima la Ulaya, Ukraine wakaunda nchi yao huru, kutoka mikononi mwa kukaliwa na Russia, Poland na kukaliwa na Ottoman na ikawa ndio mwisho wa mkataba wa "Kolomak Articles" wa mwaka 1687.

Hatima ya Ukraine ilipatikana tarehe 10 June Mwaka 1917, kwa Ukraine Kupata uhuru na hatimae tarehe 20 January 1918 Ukraine ikawa Jamhuri ya ujamaa ya Soviet, kisha Mwaka 1921, "mkataba wa Riga" ulisainiwa ili kumaliza vita vya Poland-Soviet, ambapo baadhi ya maeneo ya Ukraine yakawa sehemu ya Poland, Czechslovakia na Romania.

Kisha Ukraine ikajiunga na Jamhuri ya Ujamaa ya Soviet ya Russia (USSR) iliyokuja kujulikana kama umoja wa Soviet.

Basi bwana....

Mwaka 1939, Hitler aliivamia Poland, iliyokuwa na kundi kubwa la raia wenye asili ya Ukraine, jambo hili lilipekekea vita ya Pili ya dunia kwa Urusi kuingia ili kuyadhibiti majeshi ya Hitler kuivamia Urusi.

Vita hiyo ndio chanzo cha migogoro inayoendelea mpaka sasa huko Ukraine na Russia, tutaliona hili hapo mbeleni.

Cha kuzingatia kwanza ni kwamba tarehe 24 august 1991, viongozi waaandamizi wa Urusi, Belarus na Ukraine walikutana huko Belarus, Pande zote tatu zilikubali kuondoka katika Umoja wa Sovieti wakasaini mkataba wa "Declaration of independence from Soviet Union".

Hivyo tarehe 24 August 1991, zikawa ndio zama za mwisho za Soviet.

Pamoja na Soviet union kuanguka bado uhasama baina Ukraine na Russia umekuwa ukiongezeka mpaka kufikia kuibuka kwa vita ya Russia kuamua kuivamia Ukraine.

Ni kwanini Urusi anaitaka Ukraine? Nini hasa Sababu ya Urusi hasa Putin kuamua kuivamia Ukraine? Ikizingatiwa kuwa ni ndugu wawili wa baba mmoja?

Swali hasa la kujiuliza hapa ni kwanini Urusi anaitaka Ukraine? Na kwanini anataka kuyarejesha majimbo ya Donbass (Donetsk na Luhansk) kwanza kabla ya kuidhibiti Ukraine kuelekea kuichukua mazima?

Kimsingi mgogoro huu umeibuliwa na kuchagizwa na kutanuka kwa NATO.

Yes, ni NATO, ambayo ndio imesababisha Urusi kurudi kuitaka tena Ukraine, yani kuvunja mkataba wa "Pereiaslav Treaty" wa mwaka 1654 ambao ndio hasa uliilinda Ukraine kuchukuliwa na kutawaliwa na Urusi.

Kama nilivyosema huku nyuma, Ukraine na Urusi ni nchi moja, zilizo gawanyika baada ya uvamizi wa Mongols, baada ya uvamizi ule kila nchi ikaamza kujijenga na kujiimalisha kivyake, yan Rus ya mashariki (Russia) ikajitanua kumuwin mwenzake Rus ya magharibi (Ukraine).

Matokeo yake ni kwamba Russia ilipata nguvu kuliko Ukraine na kuanza kuvamia Ukraine tena hasa kipindi cha Ivan the great, Ukraine haikuweza kudhibiti Russia mpaka ilipomezwa yote kupitia mkataba wa "Kolomak Articles" wa mwaka 1687 ulio ipa mamlaka Russia kumchukua ndugu yake Ukraine tena, nadhani nimeeleza kwa upana huko juu.

Sasa kinachoendelea sasa kwa Urusi kuitaka tena Ukraine ni baada ya utanuzi wa adui yake mkubwa Marekani kupitia mgongo wa NATO, ntaeleza hili mbeleni.

NATO ndio sababu ya hasira za Urusi kuitaka tena kuidhibiti Ukraine, Urusi hayuko tayari kuona akishindwa kudhibiti mipaka yake dhidi ya maadui zake, nadhani hii ni kanuni ya asili ya kijasusi katika usalama "Principal of nationality" au "interest de impera".

Kanuni hii hutumiwa na Marekani pia, mwaka 1848 Marekani ilifunga mkataba wa ulinzi na Mexico ulioitwa "Treaty of Guadalupe Hidalgo", mkataba huu ulimaliza vita baina ya Mexico na Marekani (Mexican-American War) ambapo vita ile ilipelekea Marekani kuchukua majimbo kadhaa ya Mexico ya Arizona, California, New Mexico, Texas, Florida, Nevada na sehemu ya jimbo la Utah.

Nje ya hilo pia mkataba huo uliitaka Mexico kutokaribisha nchi yoyote kuweka kituo cha kijeshi wala aridhi ya Mexico kutumika kama eneo la nchi nyingine kuendesha vita na Marekani, Marekani ana mkataba wa namna hii na nchi nyingi sana barani Amerika ya kusini.

Hivyo basi hata Urusi inazingatia sana hiyo kanuni ya "Principal of nationality" au "interest de impera"

Sasa turudi kwanini NATO ndio sababu...

Hii NATO hufahamika kama umoja wa kujihami wa nchi za magharibi, kwa kimombo hufahamika kama "The North Atlantic Treaty Organization", lakini pia hufahamika kama "North Atlantic Alliance".

Kimsingi NATO ni jumuia ya ushirikiano kijeshi baina ya nchi 27 za Ulaya na nchi 2 za Amerika ya kaskazini na nchi moja ya Ulaya ya kati, jumuia hii iliweka mkataba wa kusaidiana kijeshi iwapo nchi moja wapo itavamiwa na adui.

Jumuia hii ya NATO ilianzishwa mnamo tarehe 4 April 1949 kufatia kumalizika kwa vita ya pili ya dunia na kuibuka kwa vita baridi dhidi ya tishio la Umoja wa Usoviet USSR, hii Soviet Union ilikuwa tisho duniani dhidi ya mataifa ya kibepari huko Ulaya magharibi ambayo kiongozi wao ni Marekani.

Kufatia hilo wakaona waunde jumuia ya kujihami ili wawe salama, tutaliona hilo kwa undani zaidi.

Ok tutaanza hivi, Urusi mwaka 1982 mpaka mwaka 1984 wakati ile iliyoitwa Soviet Union ikielekea kuanguka Urusi iliwahi kutawaliwa na raisi aliyeitwa Yuri Andropov ambaye huyu bwana alikuwa bosi wa KGB kwa miaka 15 lakini bado hali ya nchi ilikuwa mbaya sana hasa kwenye mtikisiko wa kusambaratika na Uchumi.

Wakati Urusi inakaribia kuanguka miaka ya 1980 mwishoni na tisini mwanzoni kulikuwa na makubaliano baina ya Serikali ya Mikhaili Gorbachev na George Bush kwamba Urusi ingesitisha vita na kuzipa Uhuru nchi kama Poland, Latvia, Estonia, Ukraine na zinginezo ambazo zingependa kujitoa kwenye Jamhuri ya Kisovyeti.

Lakini Urusi ilisisitiza kuwa haya yangefanyika tu endapo Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO hautajitanua tu hata kwa Inchi moja wala Sentimeta moja kuelekea Ulaya Mashariki kwenye nchi ambazo bado zina maslahi na Urusi, zingatia neno "masrahi na Urusi"

Kwa bahati zaidi Mikhaili Gorbachev kwa kipindi hicho alikuwa akihudhuria kwenye vikao vya G7 mnamo siku za mwisho za Jamhuri ya Kisovieti na alikuwa akiomba mkopo kwa mataifa hayo ili kunusuru uchumi wa Urusi.

Lakini tofauti na Ufaransa hakuna taifa lililokubali kumpa mkopo wakati tayari alikuwa ameshakubali kufanya matakwa yao ya kuiuganisha Ujerumani kwa Kuvunja Ukuta wa Berlin.

Utawala wa William Jefferson Clinton (Bill Clinton) ulikiuka masharti na kuamua kufanya ubabe kwa kuanza kuitanua NATO kwa kasi kuielekea nchi ya Urusi ambayo ilikuwa imeshakubali kuweka silaha chini na kutafuta amani.

Unakumbuka walivyoanza kuilipua Yugoslavia ambayo kwenye Historia Warusi wanaichukulia kama ninjamii yao ya SLAVCS kama ndugu zao wa damu, na ikumbukwe kwamba chanzo cha vita ya kwanza ya dunia ni pale ambapo Urusi hakukubali kuona Ujerumani na AUSTRIA-HUNGARY wanaipa masharti nchi ya Serbia.

Ambapo mwaka 1914 Austria ilivyoitangazia vita Serbia kwa kushindwa kuwapelekea wauaji wa Arch-Duke Ferdinand basi Urusi chini ya Mfalme Nicholas Romanov waliitangazia vita Austria na yakatokea yaliyotokea mpaka mwaka 1917, vita ilipo koma.

Lakini William Jefferson Clinton na Madeline Albright waliipuuza hii historia na kuanza kuvunja makubaliano waliyowahi kufanya na Gorbachev kwenye mkataba uliofungwa December 1991, wa "Treaty of Final Settlement with Respect to Germany.

Pia February 1991 ulifungwa mkataba ulioitwa "Visegrad Declaration" ili kulinda makubaliano haya likaundwa Baraza la Ushirikiano la Atlantiki ya Kaskazini (NACC) mwaka wa 1991 huku USSR na nchi za zamani za Warsaw Pact zikiwa wanachama ili kuwezesha mazungumzo na kuimarisha uwazi kati ya Ulaya magharibi na Ulaya mashariki iliyoongozwa na Urusi.

Pia mwaka 1997 kukawepo mkataba uliolenga kuongeza urafiki na kupunguza uhasama baina ya Russia na NATO (Nato-Russia relationship) kupitia mkataba ulioitwa "Nato-Russia Founding Act" uliosainiwa mwaka 1997 kupitia mkutano wa Madrid (Madrid Summit).

Mikataba yote hii ilikuwa inasisitiza kuwa Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi yani NATO usijitanue hata kwa Inchi moja wala Sentimeta moja kuelekea Ulaya Mashariki kwenye nchi ambazo bado zina masrahi na Urusi, endelea kuzingatia neno "masrahi ya Urusi"

Mikataba yote hiyo haikuwa chochote, kwani mwaka 1999 nchi za Czech, Poland na Hungary zikajiunga na NATO kuwa wanachama waangalizi, na watu wengi walililamika sana akiwemo Gorbachev na Boris Yeltsin lakini Marekami wakawapuuza.

Warusi walichukulia hili kama Usaliti hasahasa pale ambapo NATO miaka ya 1990's ikiongozwa na Marekani iliamua kufanya uvamizi dhidi ya Jamhuri za Yugoslavia na kuanza kuilipua Kosovo ambayo ni sehemu yenye maslahi makubwa na Urusi pia ndiyo sehemu iliyomfanya Mrusi aingie kwenye Vita ya Kwanza ya dunia mwaka 1914.

Hili jambo la Marekani kuingia Kosovo lililalamikiwa sana na Urusi hadi kijarida cha National Interest walilaani kwa kusema kwamba haya yalikuwa ni makosa ya kiufundi kwa Utawala wa William, unaweza kujisomea mwenyewe hapa "How Bill Clinton Made America More Ambitious—and Dangerous"

George Bush Mdogo naye akaendelea kufanya ujinga, akaitoa Marekani kwenye mkataba wa ABM (Anti-Ballistic Missile Treaty 1972) na kuamua kutengeneza makombora ya masafa Marefu, Walipoulizwa na Urusi kuhusu hili wakasema na nyinyi tengenezeni kama mnaweza sisi hatuna tatizo.

Mwaka 2000 PENTAGON ilipeleka ripoti ya Uchambuzi wa Ulinzi kwa raisi George Bush kwamba serikali ya Urusi hasa jeshi lake lipo hoi, Nchi imechoka na rushwa, utawala mbovu, vita ya Chechenya na Ugaidi, Kama ikiendelea hivyo basi kufika mwaka 2004 Jeshi la Urusi na nchi inaweza isiwepo kabisa hapa duniani kwasababu itakuwa imeshasambaratika zaidi.

Serikali ya Marekani wakiongozwa na Media zao wakayaamini haya na kuanza kujifanyia wanayotaka hata kuikiuka protokali ya mkataba wa Minsk l na Minsk ll, Nyuma ya pazia Warusi kuona hivyo wakaanza kujipanga na kuungana hasa hasa baada ya kujua kwamba Marekani anataka kuwafutilia mbali ya uso wa dunia.

George Bush baada ya kuona Urusi imeanza kuwa na nguvu, Vita za Afghanistani na Iraq zimeenda vibaya na wakati huo huo Uchina anachuana naye sana kibiashara akachanganyikiwa hadi mwaka 2004 bila hata kufikiria madhara yake, akaamua kuziingiza nchi saba zilizo jirani na Urusi kwenye Umoja wa kujihami wa NATO.

Marekani akavuta mipaka zaidi baada ya kusogea karibu kabisa na Urusi kupitia Georgia mwaka 2008 na tunakumbuka wote nini ambacho Vladmir Putin alimfanya Mikhail Sakhasvilli ambaye alikuwa raisi wa Georgia.

Mjaluo wetu Barack Obama huyo naye akaingia kichwa kichwa huko Ukraine na Syria sehemu zenye maslahi makubwa ya Urusi, Kumbe hakujua kwamba anazidi kuwafanya Warusi wapate sababu ya kujijenga kijeshi, na kuamua kuanza kusuka mipango ya kuirekesha Ukraine zizini.

Ni kweli Urusi siyo taifa kubwa hapa duniani kiuchumi, lakini kafanyia kazi makosa yake, ikiwapo na kukubali kufuata mikataba yote bila kujua kuwa wenzake walilenga kummaliza.

Hivyo Vladmir Putin kufika hapa alipo pia ni Ujinga wa mataifa ya Ulaya umechangia kwa kiasi kikubwa na kusababisha Warusi wamuunge mkono Putin na kuona kama ni mwokozi wao kwa wakati kama huu.

Sasa unaweza kuona ni kwanini Urusi Kaamua kuingia kwenye vita ya akili na ulaya na Marekani huku ikienda mbele zaidi kuingia kwenye vita ya kimkakati na Ukraine, sababu kubwa ni NATO kukiuka mashariti na itifaki ya mkataba wa "Nato-Russia Founding Act", na ule wa Minsk yani "Minsk agreement" kwa mataifa ya Marekani na washirika wake kutokujitanua kwa kuidhibiti Urusi

Kinachofanyika sasa ni Urusi kuzuia yale mataifa yake ya zamani (USSR) kutokujiunga na NATO, maana Urusi anaamini kwamba kitendo cha Ukraine kujiunga na NATO ni kuwasogeza Maadui mlangoni, hivyo Putin anazuia makosa yaliyofanyika awali mpaka kupelekea kuvunjika kwa Soviet Union yasijirudie tena.

Ndio maana Moscow haiko Tayari kuona maeneo ya mipaka yake na nchi za ulaya kati haipotezi ushawishi wake, kwa kutambua hilo ndio maana kaamua kuzuia NATO kujipenyeza kwenye mataifa yote ya Ukraine, Lithuania, Belarus na ukanda mzima wa Urusi magharibi.

Ndio maana kwake Ukraine ni muhimu sana kwa masrahi ya usalama wake, Ukraine ni mama yake, kuiachia Ukraine mikononi mwa adui zake ni kuiua Urusi.

Hakuna Russia salama kama Ukraine itakuwa mikononi mwa adui zake, masrahi ya Urusi kwa Ukraine ni muhimu zaidi kuliko hata Moscow yenyewe zingatia neno "masrahi ya Urusi"

Urusi salama ipo mikononi mwa aridhi ya Ukraine, NARUDIA TENA ZINGATIA NENO "MASRAHI YA URUSI"

Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526 uungwe group la Maktaba Kuu kwa gharama ya Tsh 3000/=.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.

Maktaba Kuu.View attachment 2253544View attachment 2253547View attachment 2253545View attachment 2253548View attachment 2253546View attachment 2253549View attachment 2253550
a2ef5e9cb6fd099082ac51751929ed50.jpg
View attachment 2253551
FB_IMG_1654598251199.jpg
FB_IMG_1654598507878.jpg
800px-Coin_of_Vladimir_the_Great_(reverse).svg.jpg
FB_IMG_1654526377310.jpg
Varangian_routes.jpg
Muromian-map.jpg
800px-Location_of_Kyivan_Rus.jpg
%D0%92%D0%B0%D1%80%D1%8F%D0%B3%D0%B8.jpg
East_Slavic_tribes_peoples_8th_9th_century.jpg
 
URUSI SALAMA IPO MIKONONI MWA ARIDHI YA UKRAINE.

Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Tuesday- 7/05/2022
Marangu Mtoni, Kilimanjaro - Tanzania

Unataka kujua kwanini Urusi anaitaka Ukraine?, Ok twende pamoja...

Urusi na Ukraine wana historia moja toka mwanzo, historia yao inafanana kwa kila kitu, ni damu moja, jamii moja na kabila Moja, ni watoto wa baba mmoja, damu yao ni kutoka kwa babu yao Rurik of Ladoga.

Wote ni jamii ya Slavs kutoka Kabila la Varangian, asili yao ni eneo la Vistula, eneo hilo la Vistula ni eneo la mpaka wa Poland, Sweden na Finland ya sasa, zamani iliitwa Ladoga, baadae ikaitwa Rus, kisha ikaitwa Kievan Rus, baada ya mgawanyo mwaka 1550 ikazaliwa Russia na Ukraine lakini Ukraine hii ya sasa ilianza kuibuka baada ya mkataba wa "Riga", ntaeleza hili huko mbeleni.

Lakini kubwa la kuzingatia hapa ni kuwa kati ya Ukraine na Urusi nchi ya kale zaidi ni Ukraine, Ukraine ndio mama wa Urusi, Urusi katoka tumboni mwa Ukraine, mji wa Kyiv (Kiev) ndio mji mkuu wa kwanza kuanza kabla ya Moscow, Russia (Urusi) kazaliwa baada ya Ukraine ya awali (Kievan Rus) kuparaganyika, yani kuvunjika.

Historia ya Ukraine na mji wa Kyiv inaanza toka karne ya 7 huku Russia ya sasa ni zalio la mfalme Ivan the great, hili ntalieleza huko mbeleni.

Hawa ni damu moja, jamii moja na aridhi waliotoka ni moja.

Wote umtambua Rurik of Ladoga kama mwasisi wa aridhi zao, wote wanachangia historia moja ambayo iligawika mwaka 1240 baada ya uvamizi wa Mongols, tutaliona hili kwa kina huko mbeleni.

Hivyo basi.....

Mwasisi wao ni kiongozi aliyeitwa Rurik of Ladoga, alikuwa ni chifu wa jamii ya Warangian ambaye mwaka wa 862 AD alivamia na kutawala kabila la Novgorod.

Akatanua himaya na kutawala eneo lote lilokaliwa na Slavs, huyu Rurik ndie anachukuliwa kama mwanzilishi wa nasaba ya Rurikid, iliyotawala himaya ya Ladoga, ambayo kwa sasa ndio zilipo nchi za Russia, Ukraine, Beralus, Poland, Estonia na ukanda wote wa Ulaya ya kati.

Rurik alianzisha dola ya Novgorod ambayo ndio baadae ilikuja kuitwa Kievan Rus, yani Ukraine na Russia ya sasa.

Kulingana na simulizi kutoka jamii za Radzivil na Hypati inaeleza kuwa miaka ya 862 mpaka 864, kikundi kikubwa cha wahaimiaji kutoka Sweden (viking) ya sasa waliweka makazi eneo la Ladoga wakiongozwa na Rurik, Rurik akaongoza vikosi kuvamia Novgorod, wakajenga ngome eneo hilo karibu na Mto Volkhov.

Rurik aliongoza uvamizi na kuteka maeneo yote kuzunguka mto Volkhov mpaka eneo la Volhynia, mfalme Rurik alisalia madarakani hadi mwaka wa 879 alipo fariki dunia.

Rurik of Ladoga alifariki kifo cha kitandani mwaka 879, kabla ajafariki Rurik alitoa wosia kuwa ufalme wake uende kwa rafiki yake Oleg, ambaye atatakiwa kumlea mwanae wa kiume Igor, kwa kuwa kipindi hicho mwanae Igor alikuwa bado mdogo sana.

Oleg alipochukua madaraka akahamisha mji mkuu kwenda Kiev (Kyiv) baada ya kufanya uvamizi na kuwashinda wenyeji na kuwaua watawala wa eneo hilo na kuanzisha himaya ya Kievan Rus, himaya hiyo ilitawala eneo hilo mpaka Igor alipokuwa mkubwa.

Igor the Old alichukua madaraka na kueneza utanuzi wa himaya ya Kievan Rus kuelekea kusini mwa mto Desna, yeye ndio alijenga ngome za kusini kuwadhibiti wafanya biashara wa Scandinavia kuvamia himaya yake, baada ya Igor the Old kufariki mwaka 945 ufalme na utawala ukaenda kwa mwanae Olga.

Huyu Olga ndio hufahamika kama Olga the Kiev, yeye ndio mwenye historia ya kuijenga jiji la Kyiv, ukifika kaskazini mwa jiji la Kiev kuna sanamu refu la mwanamama ambalo ndio refu kuliko sanamu zote kwenye jiji hilo, sanam lile huitwa saint Olga.

Baada ya kifo cha mfalme Olga madaraka yakarithiwa mwaka 925 na Sviatoslav the Brave, huyu alikuwa jemedari Mkuu wa Kiev, ni moja ya wafalme maarufu wa dola ya Kievan Rus, umaarufu wake unatokana na kushinda vita nyingi za mashariki na kusini mwa Ulaya ambazo zilisababisha kuanguka kwa mataifa makubwa mawili ya Ulaya wakati huo ya Dola ya mwanzo ya Bulgaria na Dola ya Khazaria na Dola ya Kwanza ya mashariki Slavic, hawa slav wa mashariki ndio eneo la Poland ya sasa.

Baada ya kifo cha Sviatoslav the Brave ufalme ukaenda kwa mfalme Yaropolk I Sviatoslavich, mwaka 972 ambae alitawala mpaka mwaka 978 kisha akarithiwa na Vladimir the great, huyu mama yake alikuwa ni kutoka Nordic.

Nordic ni jamii ya norsemen au watu wa Norse hawa walikuwa ni kundi la jamii ya Germanic ambao walizungumza lugha ya Kale ya Norse.

Huyu Vladimir the great aliongoza vita na kuteka eneo la Belarus hadi Bahari ya Baltic na kuimalisha mipaka dhidi ya uvamizi wa Wabulgaria, makabila ya Baltic na wahamiaji wa Mashariki.

Ni kipindi chake ukristo uliingia Kievan Rus, alipokea Ukristo kutoka himaya ya Byzantine na Orthodox na yeye kuwa mkristo wa kwanza, Vladimir alikuwa mkristo mwaka 988 na akaifanya dola ya Kievan Rus' kuwa ya Kikristo, kwasababu hiyo mpaka leo hujulikana kama Mtakatifu Vladimir.

Kisha mwaka 1015 madaraka yakaenda kwa Sviatopolk the Accursed ambae alitawala mpaka mwaka 1019, na mrithi wake akawa Yaroslav the Wise ambae husifiwa kuyaunganisha upya koo zilizoanza kuparaghanyika kufatia mpasuko uliofanywa na baba yake Sviatopolk ambae aliupata ufalme kwa kumuua kaka yake olega the order.

Dola ya Kievan Rus iliendelea mpaka uvamizi wa vikosi vya Mongol vilipo vamia mwaka 1240.

Kwaiyo.....

Kama nilivyosema huko awali ni kwamba, Mababu wa Urusi na Ukraine walikuwa sehemu ya jamii ya slavic iliyoitwa Kieven Rus, Ilianzishwa na mfalme na chifu wa pili Oleg katika karne ya tisa.

Faith Hillis, Profesa wa historia ya Urusi kutoka Chuo Kikuu cha Chicago, anasema kwamba eneo la bahari ya baltic na bahari nyeusi, ilipo sasa Ukraine, iliishi jamii ndogo ya Slavs karibu miaka elfu iliyopita.

Jamii hizi ziliamua kuungana na kuunda nchi mpya chini ya uongozi wa wafanyabiashara wa Scandinavia wanaosafiri kutoka Scandinavia kwenda Byzantium kupitia mto Nipro, Nchi hii mpya iliitwa Kieven Rus na mji mkuu wake ulikuwa unaitwa Kiev ambao ni mji mkuu wa Ukraine sasa, Watu hawa wa Slavic hawakuwa raia wa Ukraine wala Urusi, Pia ilijumuisha jamii zisizo za Kislavoni kama vile jamii za makabila ya Orguz, Mongolis, Waislamu wa Iraq na India na wayahudi."

Tuendeleee Sasa....

Karne ya 13, jamii ya Mongols walivamia Kieven Rus, uvamizi huo ulifanyika Mei 31, 1223, Majeshi ya Mongol ya Genghis Khan yakiongozwa na kamanda Subutai yaliwashinda majeshi ya Kievan Rus' kwenye Vita iliyo piganywa kwenye Mto Kalka.

Vita hivi vilikuwa ushindi mkubwa kwa Mongols katika kudhibiti ulaya ya kati, katika vita hii askali wengi wa Rus walipoteza maisha huku Mongol ikipata hasa ndogo.

Idadi kubwa ya watu wa Slavic hapa iligawanywa katika sehemu tatu kubwa, baadae mgawanyo huu ulizaa Urusi, Ukraine na Belarus ya sasa.

Katika karne ya 14, wakati Mongols inaanguka kufatia kuibuka kwa Dola ya Ottoman iliyoanzishwa na Mfalme Osman Ghazi, mwana wa Etugrul bey kutoka ukoo wa Orguz Ghazi mwasisi wa kabila la Kay na jamii ya Celjuk, huyu Orguz Ghazi ndio mwasisi wa nchi za Türkeye, Turkistan, na Uzbekistan (ntaeleza habari zake siku za usoni inshallah)

Tureje kwenye hoja yetu, baada ya kuanguka kwa Mongoli kulikuwa na tishio jingine la uvamizi wa mji wa Kiev, Poland ilikuwa inajiandaa kupanua mipaka yake na uongozi wake ulikuwa mikononi mwa wakoloni wa kirumi, Kumbuka Poland ndio walae Slavs wa mashariki (eastern Slav).

Faith Hillis anasema, "Poland na Lithuania waliungana katika karne ya 16 na kufahamika kama Kingdom of Poland and the Grand Duchy of Lithuania walianza kueneza himaya yao kuelekea eneo la kusini.

Himaya hii ilikuwa mojawapo ya nchi kubwa zaidi na yenye watu wengi zaidi Ulaya karne ya 16 hadi 17, ilikuwa na takriban kilomita za mraba 1,000,000 (400,000 sq mi) na mpaka kufikia mwaka 1618 ilikuwa na idadi ya watu karibu milioni 12.

Kingdom of Poland and the Grand Duchy of Lithuania iliundwa tarehe 1 July 1569 chini ya Mfalme wa kwanza Sigismund II Augustus of the first.

Hivyo dola hii ikaivamia Kievan Rus na mji wa Kiev ukawa chini ya utawala wa Poland-Lithuania.

Historia ya Urusi na Ukraine iliingia katika sura mpya tena katika mwaka 1462 pale mfalme Ivan lll au Ivan the great alipo anza kuikomboa tena Kievan Rus, alifanikiwa kuunda himaya ya Russia ya mashariki (moscovy).

Jina Russia na Belarus yanatokana na jina la Rus (kutoka kwenye jina Kievan Rus) hivyo Ivan the great akapendekeza eneo la mashariki alilolikomboa liitwe Russia (kutoka neno "Rus"), ndio maana yeye huitwa Ivan the Russia, sababu ndio mkombozi wa Russia ya pili baada ya ile ya Rurik of Ladoga na Oleg kufutika.

Ivan aliijenga Rus mashariki (Russia) kutoka kwenye dola ya Novgorod iliyokuwa chini ya Poland na Lithuania, hatimae mwaka 1470 baada ya vita vingi na kupata ushindi kwenye ile vita ya mto shelon (Battle of Shelon River) iliyopiganwa eneo la Dvina ilipelekea Navgorodians kusalim amri mwaka 1471.

Mpaka mwaka 1480 maeneo yote ya Kiev, Crimea, Lithuania mashariki ilikuwa imeshachukuliwa na Ivan the great, hali hii ikamfanya kufanikiwa kuunda himaya mpya ya Rus mashariki (Russia), Ivan the great hufahamika kama ndio mfalme aliyeifufua tena Kievan Rus.

Hivyo.....

Faith Hillis anaelezea, "hii ilikuwa hatua kubwa ya mambo kuanza kugeuka ambapo majadiliano juu ya masuala ya utaifa yalianza na yanaendelea mpaka katika zama za sasa".

Katika karne ya 14 mpaka 18, ulikuwa wakati Urusi ilipounda himaya ya warusi ikijumuisha sehemu ya mashariki ya Ukraine.

Jina la Ukraine au Kievan ya mashariki ilikuwa ikiitwa Novorasia yaani Urusi mpya, Wakati huo huo, sehemu ya upande wa magharibi ilibaki kuwa chini ya Austria na kisha baadaye chini ya utawala wa nasaba wa himaya ya Austro-Hungarian.

Mfalme wa Urusi (Tsar Aleksei Mikhailovich) akalitoa kama zawadi jimbo la Volinskaya kwa Ukraine mnamo mwaka 1654, kimsingi majimbo yote ya Ukraine ya sasa yani kuanzia mashariki, magharibi na kusini ni mali ya Urusi.

Mfalme Mikhailovich alifanya hivyo ili kuongeza urafiki na kupunguza uadui na Kievan ya magharibi.

Mipaka ya Ukraine ya sasa ipo kwa mujibu wa mkataba wa mipaka wa "Pereiaslav Treaty" wa mwaka 1654 chini ya Mfalme Mikhailovich, Haya majimbo yote Ukraine ilikuwa ikimegewa kidogokidogo kutoka katika himaya ya Urusi kama zawadi hadi hapo Ukreni ilipofika leo.

Mfano wa majimbo hayo ni pamoja na majimbo ya Kharkovsk Oblast, Lugantsk, Donetsk, Dnepropetrovstk, Zaparozhsk, Herisontsk, Nikolaevsk na Odesk.

Hata mwaka 1922, Vladimir Ilyich Ulyanov Lenin alilitoa kama zawadi jimbo la Kharkovsk kwa Ukraine, pia Khrushev Nikita akalitoa kama zawadi jimbo la Krimea mnamo mwaka 1954 kwa Ukraine, huku Joseph Stalin akitoa majimbo manne ya magharibi yaliyopo mpakani mwa Polandi kama zawadi kwa Ukraine majimbo hayo ni Livivska, Zakarpatiska, Ivan Frankoftsk na Chernovitsk.

Lakini Pamoja na yote historia ya nchi hizi inatuonesha kuwa himaya ya dola ilianzia Kiev mji mkuu wa Ukraine ya sasa kwa zaidi ya miaka 1600 na kisha himaya ikarudi Moscow yani Russia mwaka 1500 kipindi cha mfalme Ivan the great.

Hii inamaana kwamba mji wa Kyiv (au Kiev) ni mkongwe kuliko Moscow, Kyiv ndio baba wa Moscow, kwasababu Kiev ndio ulikuwa mji mkuu wa himaya ya Kievan Rus', mji wa Kyiv unatajwa kuanzishwa mwaka 482 AD.

Simulizi za kale zinasema kwamba wakazi wa kwanza kuishi Kyiv ni watu wanne ambao ni, Kyi, Shchek na Khoryv, na dada yao Lybid, hawa ndio wakaazi wa kwanza kabisa kuishi mji huo ukiwa pori na kichaka, aifahamiki hasa walitokea wapi, japo simulizi hutaja kuwa walitokea Poland, watu hawa ndio walio anzisha jiji hilo.

Kimsingi jina Kyiv, linatokana na jina la mkaazi kiongozi wa kwanza mjini hapo ambae jina lake ni Kyi, aliyekuwa kaka mkubwa wa miongoni mwa wakaazi wanne wa kwanza kufika hapo.

Taratibu kwenye vilima vya Mto Dnipro, kulianza kupokea wageni wahamiaji kutoka jamii za Slavic kutafuta makazi, hatua kwa hatua mji ukakuwa na mfalme Oleg alipo hamishia makazi ya dola hapo ukaifanya Kyiv kuwa kitovu cha ustaarabu wa Slavic Mashariki, chini ya dola ya Kievan Rus' katika karne ya 10-12.

Hivyo Kyiv ni moyo wa historia ya Ukraine na Urusi, bila Kyiv hakuna historia ya Ukraine wala Urusi, ndio maana wao wote wa wawili huita Kyiv Mama takatifu.

Sasa unaweza kuona ni kwanini Putin anaitaka Ukraine kuliko sehemu yoyote ile kwenye ustawi wa masrahi yake.

Urusi hii ya sasa ilanza kustawi tena baada ya Ivan the great na kustawi zaidi Ulaya kipindi cha utawala wa mfalme Peter the great, huyu Mfalme Peter ndio mwenye mji maarufu wa St Petersburg, mji huu ulipewa jina hilo kurejelea heshima ya Peter the great.

Huyu Mfalme Peter the Great alikuwa mfalme wa Utawala wa Urusi kuanzia tarehe 7 Mei 1682 hadi kifo chake kilipotokea mnamo mwaka 1725, Chini ya utawala wake ndie aliyoifanya Urusi kukua kisasa na kuwa na nguvu barani Ulaya.

Peter the great alishinda vita nyingi, ni yeye aliye kamata bandari ya Azov na Bahari ya Baltic, ambayo inamilikiwa na Urusi mpaka leo, aliongoza mapinduzi ya kiuchumi ambayo yalibadilisha baadhi ya mifumo ya kijamii na kisiasa ya Urusi na kupelekea mifumo ya kisasa ya maisha ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kisayansi.

Ni yeye aliye anzisha taasisi nyingi za serikali ya Urusi zinazofanya kazi mpaka leo, yeye ndie aliye anzisha na kuendeleza jiji la Saint Petersburg, ambao alihamishia makao makuu ya utawala wake kutoka Moscow na kulifanya jiji la St Petersburg kuwa mji mkuu wa Urusi hadi 1917 serikali ya Bolsheviks ilipo hamia Moscow tena.

Chuo kikuu cha kwanza cha Urusi cha Saint Petersburg State University kilianzishwa mwaka mmoja tu kabla ya kifo chake yani mwaka 1724, pia chuo cha pili kuanzishwa Urusi cha Moscow State University kilianzishwa miaka 30 baada ya kifo chake, lakini ilikuwa ni ndoto yake kuwa na chuo kikubwa Ulaya, ndoto hiyo ikatimizwa na utawala wa binti yake Elizabeth.

Ok, Tuenderee Sasa....

Mvutano wa kujenga himaya barani Ulaya kati ya mataifa ya Ulaya ulisababisha kutokea vita vya dunia mwaka 1914, Miaka minne baadaye, wakati vita vilipomalizika, hakuna aliyebaki salama, si Austro-hungary wala himaya ya Warusi iliyonusurika na madhara ya vita ya kwanza ya dunia.

Baada ya vita vya kwanza vya dunia na mapinduzi ya Urusi mwaka 1917 yalibadilisha ramani ya bara zima la Ulaya, Ukraine wakaunda nchi yao huru, kutoka mikononi mwa kukaliwa na Russia, Poland na kukaliwa na Ottoman na ikawa ndio mwisho wa mkataba wa "Kolomak Articles" wa mwaka 1687.

Hatima ya Ukraine ilipatikana tarehe 10 June Mwaka 1917, kwa Ukraine Kupata uhuru na hatimae tarehe 20 January 1918 Ukraine ikawa Jamhuri ya ujamaa ya Soviet, kisha Mwaka 1921, "mkataba wa Riga" ulisainiwa ili kumaliza vita vya Poland-Soviet, ambapo baadhi ya maeneo ya Ukraine yakawa sehemu ya Poland, Czechslovakia na Romania.

Kisha Ukraine ikajiunga na Jamhuri ya Ujamaa ya Soviet ya Russia (USSR) zilikuja kwenye umoja wa Soviet.

Basi bwana....

Mwaka 1939, Hitler aliivamia Poland, iliyokuwa na kundi kubwa la raia wenye asili ya Ukraine, jambo hili lilipekekea vita ya Pili ya dunia kwa Urusi kuingia ili kuyadhibiti majeshi ya Hitler kuivamia Urusi.

Vita hiyo ndio chanzo cha migogoro inayoendelea mpaka sasa huko Ukraine na Russia, tutaliona hili hapo mbeleni.

Cha kuzingatia kwanza ni kwamba tarehe 24 august 1991, viongozi waaandamizi wa Urusi, Belarus na Ukraine walikutana huko Belarus, Pande zote tatu zilikubali kuondoka katika Umoja wa Sovieti wakasaini mkataba wa "Declaration of independence from Soviet Union".

Hivyo tarehe 24 August 1991, zikawa ndio zama za mwisho za Soviet.

Pamoja na Soviet union kuanguka bado uhasama baina Ukraine na Russia umekuwa ukiongezeka mpaka kufikia kuibuka kwa vita ya Russia kuamua kuivamia Ukraine.

Ni kwanini Urusi anaitaka Ukraine? Nini hasa Sababu ya Urusi hasa Putin kuamua kuivamia Ukraine? Ikizingatiwa kuwa ni ndugu wawili wa baba mmoja?

Swali hasa la kujiuliza hapa ni kwanini Urusi anaitaka Ukraine? Na kwanini anataka kuyarejesha majimbo ya Donbass (Donetsk na Luhansk) kwanza kabla ya kudhibiti Ukraine kuelekea kuichukua mazima?

Kimsingi mgogoro huu umeibuliwa na kuchagizwa na kutanuka kwa NATO.

Yes, ni NATO, ambayo ndio imesababisha Urusi kurudi kuitaka tena Ukraine, yani kuvunja mkataba wa "Pereiaslav Treaty" wa mwaka 1654 ambao ndio hasa uliilinda Ukraine kuchukuliwa na kutawaliwa na Urusi.

Kama nilivyosema huku nyuma, Ukraine na Urusi ni nchi moja, zilizo gawanyika baada ya uvamizi wa Mongols, baada ya uvamizi ule kila nchi ikaamza kujijenga na kujiimalisha kivyake, yan Rus ya mashariki (Russia) ikajitanua kumuwin mwenzake Rus ya magharibi (Ukraine).

Matokeo yake ni kwamba Russia ilipata nguvu kuliko Ukraine na kuanza kuvamia Ukraine tena hasa kipindi cha Ivan the great, Ukraine haikuweza kudhibiti Russia mpaka ilipomezwa yote kupitia mkataba wa "Kolomak Articles" wa mwaka 1687 ulio ipa mamlaka Russia kumchukua ndugu yake Ukraine tena, nadhani nimeeleza kwa upana huko juu.

Sasa kinachoendelea sasa kwa Urusi kuitaka tena Ukraine ni baada ya utanuzi wa adui yake mkubwa Marekani kupitia mngongo wa NATO, ntaeleza hili mbeleni.

NATO ndio sababu ya hasira za Urusi kuitaka tena kudhibiti Ukraine, Urusi hayuko tayari kudhibiti mipaka yake na maadui zake, nadhani hii ni kanuni ya asili ya kijasusi katika usalama "Principal of nationality" au "interest de impera".

Kanuni hii hutumiwa na Marekani pia, mwaka 1848 Marekani ilifunga mkataba wa ulinzi na Mexico ulioitwa "Treaty of Guadalupe Hidalgo", mkataba huu ulimaliza vita baina ya Mexico na Marekani (Mexican-American War) ambapo vita ilipelekea Marekani kuchukua majimbo kadhaa ya Mexico ya Arizona, California, New Mexico, Texas, Florida, Nevada na sehemu ya jimbo la Utah.

Nje ya hilo pia mkataba huo uliitaka Mexico kutokaribisha nchi yoyote kuweka kituo cha kijeshi wala aridhi ya Mexico kutumika kama eneo la nchi nyingine kuendesha vita na Marekani, Marekani ana mkataba wa namna hii na nchi nyingi bara la America ya kusini.

Hivyo basi hata Urusi inazingatia sana hiyo kanuni ya "Principal of nationality" au "interest de impera"

Sasa turudi kwanini NATO ndio sababu...

Hii NATO hufahamika kama umoja wa kujihami wa nchi za magharibi, kwa kimombo hufahamika kama "The North Atlantic Treaty Organization", lakini pia hufahamika kama "North Atlantic Alliance".

Kimsingi NATO ni jumuia ya ushirikiano kijeshi baina ya nchi 27 za Ulaya na nchi 2 za Amerika ya kaskazini na nchi moja ya Ulaya ya kati, jumuia hii iliweka mkataba wa kusaidiana kijeshi iwapo nchi moja wapo itavamiwa na adui.

Jumuia hii ya NATO ilianzishwa mnamo tarehe 4 April 1949 kufatia kumalizika kwa vita ya pili ya dunia na kuibuka kwa vita baridi dhidi ya tishio la Umoja wa Usoviet USSR, hii Soviet Union ilikuwa tisho duniani dhidi ya mataifa ya kibepari huko Ulaya magharibi ambayo kiongozi wao ni Marekani.

Kufatia hilo wakaona waunde jumuia ya kujihami ili wawe salama, tutaliona hilo kwa undani zaidi.

Ok tutaanza hivi, Urusi mwaka 1982 mpaka mwaka 1984 wakati ile iliyoitwa Soviet Union ikielekea kuanguka Urusi iliwahi kutawaliwa na raisi aliyeitwa Yuri Andropov ambaye huyu bwana alikuwa bosi wa KGB kwa miaka 15 lakini bado hali ya nchi ilikuwa mbaya sana hasa kwenye mtikisiko wa kusambaratika na Uchumi.

Wakati Urusi inakaribia kuanguka miaka ya 1980 mwishoni na tisini mwanzoni kulikuwa na makubaliano baina ya Serikali ya Mikhaili Gorbachev na George Bush kwamba Urusi ingesitisha vita na kuzipa Uhuru nchi kama Poland, Latvia, Estonia, Ukraine na zinginezo ambazo zingependa kujitoa kwenye Jamhuri ya Kisovyeti.

Lakini Urusi ilisisitiza kuwa haya yangefanyika tu endapo Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO hautajitanua tu hata kwa Inchi moja wala Sentimeta moja kuelekea Ulaya Mashariki kwenye nchi ambazo bado zina maslahi na Urusi, zingatia neno "masrahi na Urusi"

Kwa bahati zaidi Mikhaili Gorbachev kwa kipindi hicho alikuwa akihudhuria kwenye vikao vya G7 mnamo siku za mwisho za Jamhuri ya Kisovieti na alikuwa akiomba mkopo kwa mataifa hayo ili kunusuru uchumi wa Urusi.

Lakini tofauti na Ufaransa hakuna taifa lililokubali kumpa mkopo wakati tayari alikuwa ameshakubali kufanya matakwa yao ya kuiuganisha Ujerumani kwa Kuvunja Ukuta wa Berlin.

Utawala wa William Jefferson Clinton (Bill Clinton) ulikiuka masharti na kuamua kufanya ubabe kwa kuanza kuitanua NATO kwa kasi kuielekea nchi ya Urusi ambayo ilikuwa imeshakubali kuweka silaha chini na kutafuta amani.

Unakumbuka walivyoanza kuilipua Yugoslavia ambayo kwenye Historia Warusi wanaichukulia kama ninjamii yao ya SLAVCS kama ndugu zao wa damu, na ikumbukwe kwamba chanzo cha vita ya kwanza ya dunia ni pale ambapo Urusi hakukubali kuona Ujerumani na AUSTRIA-HUNGARY wanaipa masharti nchi ya Serbia.

Ambapo mwaka 1914 Austria ilivyoitangazia vita Serbia kwa kushindwa kuwapelekea wauaji wa Arch-Duke Ferdinand basi Urusi chini ya Mfalme Nicholas Romanov waliitangazia vita Austria na yakatokea yaliyotokea mpaka mwaka 1917, vita ilipo koma.

Lakini William Jefferson Clinton na Madeline Albright waliipuuza hii historia na kuanza kuvunja makubaliano waliyowahi kufanya na Gorbachev kwenye mkataba uliofungwa December 1991, wa "Treaty of Final Settlement with Respect to Germany.

Pia February 1991 ulifungwa mkataba ulioitwa "Visegrad Declaration" ili kulinda makubaliano haya likaundwa Baraza la Ushirikiano la Atlantiki ya Kaskazini (NACC) mwaka wa 1991 huku USSR na nchi za zamani za Warsaw Pact zikiwa wanachama ili kuwezesha mazungumzo na kuimarisha uwazi kati ya Ulaya magharibi na Ulaya mashariki iliyoongozwa na Urusi.

Pia mwaka 1997 kukawepo mkataba ulilenga kuongeza urafiki na kupunguza uhasama baina ya Russia na NATO (Nato-Russia relationship) kupitia mkataba ulioitwa "Nato-Russia Founding Act" uliosainiwa mwaka 1997 kupitia mkutano wa Madrid (Madrid Summit).

Mikataba yote hii ilikuwa inasisitiza kuwa Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi yani NATO usijitanua hata kwa Inchi moja wala Sentimeta moja kuelekea Ulaya Mashariki kwenye nchi ambazo bado zina masrahi na Urusi, endelea kuzingatia neno "masrahi ya Urusi"

Mikataba yote hiyo haikuwa chochote, kwani mwaka 1999 nchi za Czech, Poland na Hungary zikajiunga na NATO kuwa wanachama waangalizi, na watu wengi walililamika sana akiwemo Gorbachev na Boris Yeltsin lakini Marekami wakawapuuza.

Warusi walichukulia hili kama Usaliti hasahasa pale ambapo NATO miaka ya 1990's ikiongozwa na Marekani iliamua kufanya uvamizi dhidi ya Jamhuri za Yugoslavia na kuanza kuilipua Kosovo ambayo ni sehemu yenye maslahi makubwa na Urusi pia ndiyo sehemu iliyomfanya Mrusi aingie kwenye Vita ya Kwanza ya dunia mwaka 1914.

Hili jambo la Marekani kuingia Kosovo lililalamikiwa sana na Urusi hadi kijarida cha National Interest walilaani kwa kusema kwamba haya yalikuwa ni makosa ya kiufundi kwa Utawala wa William, unaweza kujisomea mwenyewe hapa "How Bill Clinton Made America More Ambitious—and Dangerous"

George Bush Mdogo naye akaendelea kufanya ujinga, akaitoa Marekani kwenye mkataba wa ABM (Anti-Ballistic Missile Treaty 1972) na kuamua kutengeneza makombora ya masafa Marefu, Walipoulizwa na Urusi kuhusu hili wakasema na nyinyi tengenezeni kama mnaweza sisi hatuna tatizo.

Mwaka 2000 PENTAGON ilipeleka ripoti ya Uchambuzi wa Ulinzi kwa raisi George Bush kwamba serikali ya Urusi hasa jeshi lake lipo hoi, Nchi imechoka na rushwa, utawala mbovu, vita ya Chechenya na Ugaidi, Kama ikiendelea hivyo basi kufika mwaka 2004 Jeshi la Urusi na nchi inaweza isiwepo kabisa hapa duniani kwasababu itakuwa imeshasambaratika zaidi.

Serikali ya Marekani wakiongozwa na Media zao wakayaamini haya na kuanza kujifanyia wanayotaka hata kuikiuka protokali ya mkataba wa Minsk l na Minsk ll, Nyuma ya pazia Warusi kuona hivyo wakaanza kujipanga na kuungana hasa hasa baada ya kujua kwamba Marekani anataka kuwafutilia mbali ya uso wa dunia.

George Bush baada ya kuona Urusi imeanza kuwa na nguvu, Vita za Afghanistani na Iraq zimeenda vibaya na wakati huo huo Uchina anachuana naye sana kibiashara akachanganyikiwa hadi mwaka 2004 bila hata kufikiria madhara yake, akaamua kuziingiza nchi saba zilizo jirani na Urusi kwenye Umoja wa kujihami wa NATO.

Marekani akavuta mipaka zaidi baada ya kusogea karibu kabisa na Urusi kupitia Georgia mwaka 2008 na tunakumbuka wote nini ambacho Vladmir Putin alimfanya Mikhail Sakhasvilli ambaye alikuwa raisi wa Georgia.

Mjaluo wetu Barack Obama huyo naye akaingia kichwa kichwa huko Ukraine na Syria sehemu zenye maslahi makubwa ya Urusi, Kumbe hakujua kwamba anazidi kuwafanya Warusi wapate sababu ya kujijenga kijeshi, na kuamua kuanza kusuka mipango ya kuirekesha Ukraine zizini.

Ni kweli Urusi siyo taifa kubwa hapa duniani kiuchumi, lakini kafanyia kazi makosa yake, kiwapo na kukubali kufuata mikataba yote bila kuja wenzio walilenga kummaliza.

Hivyo Vladmir Putin kufika hapa alipo pia ni Ujinga wa mataifa ya Ulaya umechangia kwa kiasi kikubwa na kusababisha Warusi wamuunge mkono Putin na kuona kama ni mwokozi wao kwa wakati kama huu.

Sasa unaweza kuona ni kwanini Urusi Kaamua kuingia kwenye vita ya akili na ulaya na Marekani huku ikienda mbele zaidi kuingia kwenye vita ya kimkakati na Ukraine, sababu kubwa ni NATO kukiuka mashariti na itifaki ya mkatabat wa "Nato-Russia Founding Act", na ule wa Minsk yani "Minsk agreement" kwa mataifa ya Marekani kujitanua kwa kuidhibiti Urusi

Kinachofanyika sasa ni Urusi kuzuia yale mataifa yake ya zamani (USSR) kutokujiunga na NATO, maana Urusi anaamini kwamba kitendo cha Ukraine kujiunga na NATO ni kuwasogeza Maadui mlangoni, hivyo Putin anazuia makosa yaliyofanyika awali mpaka kupelekea kuvunjika kwa Soviet Union yasijirudie tena.

Ndio maana Moscow haiko Tayari kuona maeneo ya mipaka yake na nchi za ulaya kati haipotezi ushawishi wake, kwa kutambua hilo ndio maana kaamua kuzuia NATO kujipenyeza kwenye mataifa yote ya Ukraine, Lithuania, Belarus na ukanda mzima wa Urusi magharibi.

Ndio maana kwake Ukraine ni muhimu sana kwa masrahi ya usalama wake, Ukraine ni mama yake, kuiachia Ukraine mikononi mwa adui zake ni kuiua Urusi.

Hakuna Russia salama kama Ukraine itakuwa mikononi mwa adui zake, masrahi ya Urusi kwa Ukraine ni muhimu zaidi kuliko hata Moscow yenyewe zingatia neno "masrahi ya Urusi"

Urusi salama ipo mikononi mwa aridhi ya Ukraine, NARUDIA TENA ZINGATIA NENO "MASRAHI YA URUSI"

Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526 uungwe group la Maktaba Kuu kwa gharama ya Tsh 3000/=.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.View attachment 2253544View attachment 2253547View attachment 2253545View attachment 2253548View attachment 2253546View attachment 2253549View attachment 2253550
 
Mwaka 1939, Hitler aliivamia Poland, iliyokuwa na kundi kubwa la raia wenye asili ya Ukraine, jambo hili lilipekekea vita ya Pili ya dunia kwa Urusi kuingia ili kuyadhibiti majeshi ya Hitler kuivamia Urusi.

Comred hapa zungumza ukweli Mkuu Poland iligawanywa baada ya mkataba wa Siri kati ya Stalin na Hitler kugawana Ulaya Mashariki.

Msharika wa kwanza wa katika kuanza vita ya Dunia ya pili ni Urusi

Urusi hakuingia sababu hiyo hiyo kuyadhibiti majeshi ya Hitler. Poland basi kumbuka KATYN Massacre ambapo majeshi ya Soviet yaliwauwa Maafisa wa jeshi na WA Serikali ili iikalie Poland Sasa atawauaje Ndugu zake kama kweli alikua na Nia ya kuwatetea?

Usipotoshe Historia wewe ni Scholar mzuri sana katika Historia hutakiwi kuwa bias katika uandishi wako
 
Mkuu kuna mengi sana yapo nyuma ya pazia kuhusu hilo, ntaeleza huko mbeleni.... Kwa haraka utadhania hivyo usemavyo
 
Mwaka 1939, Hitler aliivamia Poland, iliyokuwa na kundi kubwa la raia wenye asili ya Ukraine, jambo hili lilipekekea vita ya Pili ya dunia kwa Urusi kuingia ili kuyadhibiti majeshi ya Hitler kuivamia Urusi.

Comred hapa zungumza ukweli Mkuu Poland iligawanywa baada ya mkataba wa Siri kati ya Stalin na Hitler kugawana Ulaya Mashariki.

Msharika wa kwanza wa katika kuanza vita ya Dunia ya pili ni Urusi

Urusi hakuingia sababu hiyo hiyo kuyadhibiti majeshi ya Hitler. Poland basi kumbuka KATYN Massacre ambapo majeshi ya Soviet yaliwauwa Maafisa wa jeshi na WA Serikali ili iikalie Poland Sasa atawauaje Ndugu zake kama kweli alikua na Nia ya kuwatetea?

Usipotoshe Historia wewe ni Scholar mzuri sana katika Historia hutakiwi kuwa bias katika uandishi wako
Kajitahidi kuandika vizuri lakini shida imekuja kwenye mahaba ya uislamu wake kwa Rusia .Maana wengi wao wanaamini Rusia anawaoenda waislamu kitu ambacho ni uongo kwa Sababu wakimbizi wa mashariki ya kati Huwa wanaenda Ulaya na Marekani na sio Urusi,.
 
Wanaenda Marekani na ulaya kwa sababu wao ndio wenye haki ya kuwapokea maana Marekani na Ulaya ndio wanaoenda kuzichafua nchi zile so hakuna atakaebeba mzigo ispokua wao waliochafua, sasa Russia anahusikaje na wakimbizi ?? Wataenda hukohuko kueneza Uislam maana Mwenyezi Mungu huwaga anaanza kulipa hapahapa duniani
 
Back
Top Bottom