Kagosi DJ
Member
- May 5, 2020
- 19
- 69
Akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa bunge uliopewa jina la "Russia-Africa in a Multipolar World", Raisi Putin alitangaza kuwa Urusi imefuta madeni ambayo nchi hiyo inayadai baadhi ya mataifa ya Afrika yanayofikia zaidi ya Dola bilioni 20.
Vladmir Putin pia amesema kuwa kuimarika kwa uhusiano kati ya Urusi na nchi za Afrika ni lengo lake kuu, hii imetiwa chachu na vikwazo alivyowekewa na Mataifa ya Magharibi kwa kile kinacho endelea nchini Ukraine.
Mataifa ya Afrika yatarajie neema zaidi hasa kwa kipindi hiki ambacho mahusiano baina ya Kremlin na White House si mazuri. Marekani na washirika wake hawatokuwa tayali kuona ushawishi wao unapungua Barani Afrika. Hivyo mengi yanaweza kutokea yenye manufaa kwa Bara la Afrika.