Urusi: Korea Kaskazini inataka kuhakikishiwa usalama wake na Marekani

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,415
9,557
Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi,Sergei Lavrov,amesema kwamba Korea Kaskazini ipo tayari kufanya mazungumzo moja kwa moja na Marekani kuhusiana na mpango wake wa nyuklia.Hayo yalielezwa na Lavrov alipokutana na waziri mwenzake wa mashauriano ya kigeni wa Marekani,Rex Tillerson huko Vienna.

"Korea Kaskazini inataka mazungumzo na Marekani lakini inahitaji kuhakikishiwa usalama wake na ikulu ya Marekani.Tupo tayari kuunga mkono hilo na kushiriki katika mazungumzo hayo",alisema Lavrov.

Hayo yamejiri baada ya maafisa wa ngazi za juu wa Urusi kwenda Pyongyang kufanya majadiliano na wale wenzao wa NK.

Mapema mwezi huu Korea Kaskazini ilifanya majaribio ya kombora lake la masafa marefu(ICBM),Hwasong-15 lenye uwezo wa kufika Washington,New York na miji mingine ya Marekani huku Marekani na Korea Kusini wakifanya mazoezi makubwa ya kijeshi ya Anga yenye lengo la kujiweka tayari kushambulia maeneo ya silaha za nyuklia za Pyongyang.

Korea Kaskazini inataka kutambuliwa na Marekani kama Taifa lenye nguvu za kinyuklia huku Marekani ikisema kamwe haitaitambua nchi hiyo kama Taifa la kinyuklia ambapo Rais wa Marekani alipokutana na washauri wake wa Mambo ya usalama alisema kwamba tatizo la Korea Kaskazini litadhibitiwa ipasavyo.

China na Urusi zinasema majadiliano ndo njia pekee ya kutatua mgogoro huo huku ikisisitiza sera yake ya 'double freeze' ambapo NK iache kufanya majaribio yake ya makombora na Marekani iache kufanya mazoezi ya kijeshi na SK, Marekani imekataa mpango huu kwa kusema kwamba ina haki ya kufanya mazoezi ya kijeshi na washirika wake huku ikisisitiza kwamba muda wa mazungumzo na Korea Kaskazini unakaribia ukomo.

THE GUARDIAN & ARRIRANG NEWS
 
Nahisi alidhani baada ya kufanya icbm test US wangeufyata kumbe ndo kwanza katia petroli kwenye moto.Naona kaka yake Urusi kamwambia dogo akitulize.
Aliyekutangulia kuiona siku sio wa kubeza, Nk hana historia katika vita yoyote kubwa, hivyo naona anataka kuingia msitu mgeni kwake, japo silaha zake pia sio za kubeza lakini "avaaye asijifu kushinda avuaye)
 
N.Korea ,, ukiangalia kwaumakin ,,utagundua , Kim ameamua kuwaweka jamaa kimtego ,,, huyu bwana angekua nalengo lamazungumzo angekua keshafanya muda .

Putin na bwana Xi ,, shida yetu hatutaki THAAD systems + mazoezi ya kijeshi milangon mwetu.

Hapo wamarekan , niether wakubali hayo mashariti au wakatae ,,alafu kajamaa kaendelee na vitu vyake .

Huku urusi na uchina wakisema * US haikuwa tayari yenyewe *.
 
Back
Top Bottom