Uroho wa Madaraka wa CCM (CHAMA CHA MAJIPU)

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Niseme Kwa Maneno Machache, Iliniwia Vigumu sana siku za Mwanzo Kuwaaminisha Watanzania Kuwa CCM Hawakushinda Uchaguzi wa Urais Bali Waliupora.

Mwenye Macho Haambiwi Tazama.
1)Walichofanya Dodoma Kwenye Uchaguzi wa Kumpata Mgombea Ni Ushahidi Kuwa CCM aka (CHAMA CHA MAJIPU) Ni hapa Mizegwe tu hapa ni Wizi Tu, Hapa Hadaa tu Hapa Ni Kupora!
2)Walichofanya Wakati wa Uchaguzi (a) Kupora Computer za Taasisi Tatu tofauti. ITC ya Ukawa, ICT ya Kituo cha Haki za Binaadamu, Computer za Umoja wa Asasi za Kiraia. Ilikuwa Ni kufuta Ushahidi wa Wizi.
3)Walichofanya Zanzibar Kufuta Ushindi wa CUF na Uhuni wa Kuwachomeka kwa lazima Wagombea wa CUF hata baada ya Kukataa kushiriki, "Uchaguzi" haramu wa Marudio.
4)Juhudi Kubwa walizofanya za Kuleta wajumbe haramu kwenye Manispaa za Dar ili washende Umeya
5)Juhudi Kubwa za Kuvuruga na Upora Ushindi wa Ukawa ambao Upo wazi wa Meya wa Jiji.

Watanzania Tunahitaji Ushahidi wa Namna Gani Kujua CCM huwa hawashindi chaguzi bali wanaiba na Kupora ushindi. Na Pale inaposhindikana Kimizengwe wanatumia hata Polisi na Majeshi. IT IS A SHAME!
 
Muda si mrefu mtakubaliana na Donald Trump. Ile thread yake ya maneno machafu aliyotoa kwa voongozi wa Africa watu humu walilaani sana. Sasa nadhani mnaona na kumuelewa Trump alikuwa anamaanisha nini.

Waafrica tunahitaji kutawaliwa tena kwa mara ya pili.
 
Sijui wanachama wa ccm huwa wanajisikiaje. Hivi kuna busara gani ya kuwepo kwa chaguzi za vyama vingi huku chama kingine kikijihami kwa kutumia risasi na mabomu? Kwanini tume za uchaguzi zinazojitanabaisha kuwa huru zinapenda kuburuzwa? Au zinalipa fadhila kwa walioziteua? Uhuru wao uko kuwaruhusu polisi kuwa bised au ni mimi sielewi? Tena zinaongozwa na majaji wenye heshima na nikisema majaji hawa wanazitia doa kazi zao bora walizokwisha kuzifanya nakosea? Hebu nao tuwaone kuwa hawakuwahi kutoa hukumu za haki basi kwa kuruhusu figisu kwenye vyombo wanavyoviongoza sasa.
 
Back
Top Bottom