Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Mzimu wa Kolelo

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
1,485
2,000
.habar za majukumu ndugu zangu....husiken na kichwa cha habar hapo juu....nimekuwa nikisumbuliwa na u.t.i ya mara kwa mara au naweza nikasema u.t.i sugu sababu haisikii kabisa dawa.

sasa naomba mwenye kujua dawa hasa napenda iwe ya asili anisaidie maana dawa za kizungu nimemaliza karibu zote lakin tatizo bado linaendele.

Natanguliza shukran zangu...cc mziz mkavuhakuna U.T.I sugu bali ni Usugu wa dawa
na una deal na mwanamke/wanawake Wenye fangasi SUGU

tumia dawa hii AMOXICILILINE na CLAVULATE
mwambie akupe dozi ya UK kwa siku 10
ukimaliza kaa siku 5 au wiki kisha
tumida dawa hii CITAL syrup ili kufrash masalia ya bacteria

baada ya hapo kaa miezi miwili usitombe ili kupona kabisa Athari zilizotokana na mashambulio ya mfumo wa mkojo

na ukitaka kumrudia demu/mke wako mpe dozi ya siku tano na antifungal cream ajipake kunako wiki nzima
akisha maliza dozi akae mwenzi ndio uanze kumcheda
na baada ya kupona acha kutombatomba malaya ndio unampelekea mwenzio FUNGA ambao wanakuletea athali wewe


ukifanya masihara FIGO zitafail shauri yako
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,606
2,000
.habar za majukumu ndugu zangu....husiken na kichwa cha habar hapo juu....nimekuwa nikisumbuliwa na u.t.i ya mara kwa mara au naweza nikasema u.t.i sugu sababu haisikii kabisa dawa.

sasa naomba mwenye kujua dawa hasa napenda iwe ya asili anisaidie maana dawa za kizungu nimemaliza karibu zote lakin tatizo bado linaendele.

Natanguliza shukran zangu...cc mziz mkavu
Mkuu pole kwa maradhi yako ya UTI Sugu isiyo sikia dawa za Hospitali nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia maradhi yako uguwa pole.
 

_pjc_

Member
Aug 25, 2019
68
95
UGONJWA WA UTI
Kwanza kabisa kirefu cha cha herufi UTI ni URINARY TRACT INFECTION ikimaanisha ni maambukizi yanayotokana na bacteria kwenye njia ya mkojo.

Kwa ujumla njia ya mkojo inaanzia kwenye mrija wa mkojo kwa mwanaume na mwanamke. Mrija huu unajulikana kama URETHRA na ukishapata maambukizi ugonjwa sehemu hii unaitwa URETHRITIS. Njia ya mkojo inayofuata baada ya urethra ni BLADDER yaani kibofu. Wanawake wanakua na urethra fupi 4cm kulinganisha na wanaume 25cm hivo hali hiyo hupelekea wanawake kupata UTI kwa urahisi zaidi ukilinganisha na wanaume. Kibofu kikipata maambukizi ugonjwa unajulikana kama CYCITITIS. Baada ya kibofu inafuata mirija miwili inayo kwenda kwenye figo mbili. Mirija hii inaitwa ureters na ikishaambukizwa inajulikana kama URETITIS.Na mwisho wa njia ya mkojo ni figo mbili yaani kidneys na hizi figo zikishaambukizwa ugonjwa unajulikana kama NEPHRITIS.

2 VISABABISHI
Visabibishi vya ugonjwa huu huambatana na chanzo cha tatizo katika mojawapo ya sehemu husika.
-Ugonjwa wa sukari hufanya kiwango cha sukari kuwa kikubwa kwenye damu kwa vile mafigo kazi yake ni kuchuja damu hivyo ni kusema sukari huingia kwa wingi kiasi cha kusababisha vidudu bakteria kuzaliana kwa wingi kwenye figo au kibofu cha mkojo kusababisha maambukizi.
-Madawa /sumu huchubua utando wa njia ya mkojo na kusababisha bacteria kuzaliana
-Matatizo ya vijiwe kwenye figo/ mirija ya mkojo, kibofu, hufanya msongomano wa mkojo na Vijidudu huzaliana.

-Maradhi ya Tunda Prostate gland huvimba na kufunga njia ya mkojo matokeo yake kuuzuia na kuuweka mkojo mda mrefu kwenye kibofu mpaka bacteria kuzaliana.

-Tendo la ndoa, sexual intercouse unapata vijidudu moja kwa moja kutoka kwa mwanamke mwenye uambukizo

-Kujichua, tendo hili mara nyingi watu hutumia mafuta au sabuni ambazo huwa zina kemikali zinazopenya kwenye mrija wa mkojo huwasha na kusababisha vidonda ambayo bacteria hukua na kazaliana

-Usafi, aidha kwa kujikamua sana baada kukojoa, kutawaza maji machafu kutokuwa na hali ya unadhifu, huko chini kuna vijidudu ambavyo huishi baina ya njia ya haja kubwa na makorodani kutokana na hali ya ujoto humea vizuri na hupata nafasi ya kukuingia kwenye mirija kama utakuwa huna tabia ya kuwapunguza kwa usafi

DALILI
Dalili za UTI zinaonekana kulingana na aina ya maambukizi, lakini dalili kuu kwa watoto na watu wazima zinafanana, zifuatazo ni dalili za UTI kulingana na aina ya maambukizi;

-Maumivu wakati wa kukojoa na pengine kutoka uchafu au usaha kwenye njia ya mkojo.

-Urethritis dalili zake ni kupata maumivu wakati wa kukojoa

-Cystitis dalili zake ni kupata maumivu ya tumbo chini ya kitovu na saa nyingine
kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu.

-Pyelonephritis dalili zake ni Homa, kichwakuuma, kichefuchefu, kutapika,
maumivu ya tumbo sehemu za pembeni na mgongo kuuma.

MADHARA
-Hatari kubwa ya kukaa na UTI kwa mda mrefu bila kutibiwa husababisha bacteria kusambaa kutoka kwenye kubofu hadi kwenye figo. Bakteria hawa huwe ku athiri utendaji kazi wa figo kitu ambacho ni hatari sana kwa watu wenye matatizo ya figo.
-Pia kuna uwezekano mdogo wa bacteria hawa kuingia kwenye mfumo wa damu iwapo hali itatokea huweza kusababisha athari katika viungo vingine.
-Hatari ya mama mjamzito kuwa na UTI huweza kumpelekea kujifungua kabla ya wakati au kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo.

Kwa ushauri zaidi wa kitabibu na namna ya kuondoa shida hii wasiliana nasi kupitia +255715059944

IMG_0553.jpg
 

_pjc_

Member
Aug 25, 2019
68
95
No hapana kichocho ni ugonjwa mwingine kabisa

Yes swali zuri,
Kichocho kwa kitaalamu “schistosomiasis” yenyewe husababishwa na mdudu aitwae schistosoma haematobium ambae ni tofauti kabisa na vijidudu vinavyosababisha UTI kama nilivyovitaja hapo juu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom