Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Sina kwa sasa,ila madukani zipo.Inauzwa 300 tu mkuu.
Boksi lake linaendana sana na BAKING POWDER angalia usije changanya mafile
Ndo maana nikakuomba picha maana naweza kununua hata juisi kola..😂
Inauzwa maduka ya dawa au.?
 
Wanawake wanasumbuliwa na fungus na UTI sugu miaka hii sana.

Ukiwauliza wanachojua kusinguzia ni kwamba vyoo sijui vichafu. Sasa unajiuliza mbona miaka ya nyuma mama zetu, dada zetu, shangazi zetu hawakuwa wakiteseka na haya matatizo.

Jibu ni very simple, ni mabadiliko ya mfumo wa maisha ambayo yanadisturb balance ya hormones mwili na kusababisha mwili kutokana na ulaji usiozingatia mahitaji ya mwili kuzalisha acid kwa wingi, na acid inapozidi mwilini tegemea mrundikano wa magonjwa kadha wa kadha both kwa wanaume na wanawake.

Matatizo mengine ambayo hatujafuatilia ni Halitosis, hemorrhoids, stomach bloating, choo kuwa kigumu na kuwa na harufu kali sana, vidonda vya tumbo, macho kuwasha, maumivu ya kichwa, uchovu usioeleweka, kukosa hamu ya kula, hasira na moods swings, ngozi kukosa mng'ao wa asili bila kujali ni rangi gani unayo, nywele, harufu kali ya jasho, rashes, mate kuwa mazito na ya povu povu, tonsils stones, kidney stones, etc matatizo yapo mengi sana yanayokuja na hiyo hali.

Ukienda hospital utapewa midawa tu miaka nenda rudi but hii haitasaidia utachosha tu figo na ini na kuudhofisha moyo wako. Dawa ni kubadili diet yako ya chakula na kuupa mwili muda wa kupumzika. Acheni kula junk food (fast food na mavyakula ya kusindikwa viwandani) tumia healthy food.

Diet yako inatakiwa kuwa at least 50% mboga za majani na vegetables na the rest utagawanya katika makundi ya vyakula yaliyosalia.

UTI ni miongoni tu mwa magonjwa hayo ambapo huambukizwa kwa kutokea ndani yaani yale maji maji ya ukeni kuwa na tindi kali ambayo huwa ni mbolea nzuri kupata bakteria.

Wanawake punguzeni kunywa vinywaji vya kiwandani kama soda bia juice na maji haya ya chupa ya dukani. Yana kiwango kikubwa cha kemikali ambacho hujaza mwili wako na supply ya chemicals taka zinazoufanya mwili kuwa acidic zaidi.

Kunyweni maji ya kuchemsha ya nyumbani. Kama ikilazimu sana uko mbali na nyumbani ndipo utumie hayo ya dukani tena tazama sana brand za kununua. Tumia kilimanjaro, hill water au umekosa kabisa basi tumia Canadian pure. Ila haya mengine siwezi kukupa guarantee hata kidogo. Maana kwanza ukiyaweka ndani kwenye chombo baada ya kuyafungua ukija yanusa yanatoa harufu kama yamewekwa dawa..... Kuweni makini especially nyie maslayqueen mnaojikuta wa mjini sana pumbavu nyie.....

Tumieni maji yale ya kuchemsha home, unachemsha unaweka katika friji ukitoka unaeza nunua chupa special zile za maji ya lita kuanzia 2 au unachukua hata chupa hizi za maji ya dukani unatia maji yako safi kabisa unakunywa.

Yale maji faida yake hayana kemikali. Kuchemsha maji husaidia kuya neutralize yasiwe na effects mbaya kwenye mwili wako. Nawasisitiza kunywa sana juice za kutengeneza hizi fresh za nyumbani, sio hayo majuice ya kununua.....

Soda ziepukeni kabisa akina dada, soda na bia, contents zake huwa zinawafanya vibaya ninyi hamjui tu. Wanawake salad na matunda iwe sehemu ya lunch yenu muda mwingi.

Nawaambia haya yote sababu nimeshafanya sana utafiti nimegundua mahospitalini humu tunakwenda kupoteza pesa tu.

Daktari mzuri unapokwenda hospital na ugonjwa atakufunza namna ya kuukomesha, sio kukupa dawa zikupe ahuweni kesho urejee tena akupe zingine.

Zingatieni sana. Kwa maswali zaidi niulizeni tu hapa nitawaelekeza. Shemeji /wifi yenu alikuwa anasumbuliwa na mambo mengi sana ya hivyo, nilimuweka under special watch na diet. Haikuwa rahisi kunipa ushirikiano sababu sote tunajua wanawake wanavyopenda ubishi wa kitoto. Ila baada ya muda alikubali na kufuata maelekezo hivi sasa ninavyoongea ameona improvements kubwa sana na anafanya maelekezo yangu amesahau kabisa UTI. Na ameona tofauti amechangamka sana.....
 
Kaone tutoke huku tusije haribu Uzi wa watu maana naona umeanza vichokozi vipiganishi..
Screenshot_2020-11-01-17-21-08-1.png

Hiyo yenye chapa ya simba ndio Bicarbonate of soda .Hiyo nyingine ni baking powder
 
Wanawake wanasumbuliwa na fungus na UTI sugu miaka hii sana.

Ukiwauliza wanachojua kusinguzia ni kwamba vyoo sijui vichafu. Sasa unajiuliza mbona miaka ya nyuma mama zetu, dada zetu, shangazi zetu hawakuwa wakiteseka na haya matatizo...
Naam ushauri mzuri sana, kinga ni bora kuliko tiba.
 
Dugu yangu ana UTI sugu, ametumia dawa za aina mbalimbali ikiwemo sindano lakini bado UTI ipo mwilini mwake, je wajuzi wa tiba ni kweli hakuna ufumbuzi wa tatizo hilo?
 
Dugu yangu ana UTI sugu, ametumia dawa za aina mbalimbali ikiwemo sindano lakini bado UTI ipo mwilini mwake, je wajuzi wa tiba ni kweli hakuna ufumbuzi wa tatizo hilo?
Hakuna kitu kinaitwa UTI sugu kwenye tasinia ya udaktari!

Kwanza umejua je ni UTI?
definition yako ya usugu ni ipi?
Maana wadudu wanaosababisha huo ugonjwa hakuna organism hata mmoja analeta magonjwa sugu, sasa wewe tafsiri yako ya usugu ni ipi labda ni lugha ya mtaani?
Hapa wengi ndo mnapojikuta mnamezeshwa madawa bila hata kuelewa
 
Hakuna kitu kinaitwa UTI sugu kwenye tasinia ya udaktari!

Kwanza umejua je ni UTI?
definition yako ya usugu ni ipi?
Maana wadudu wanaosababisha huo ugonjwa hakuna organism hata mmoja analeta magonjwa sugu, sasa wewe tafsiri yako ya usugu ni ipi labda ni lugha ya mtaani?
Hapa wengi ndo mnapojikuta mnamezeshwa madawa bila hata kuelewa
Tupe ufumbuzi wa tatizo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom