Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,775
- 3,610
Young_Master,
Hapo kwenye bluu, panaenda kinyume na shule yangu ya Microbiology. Unaweza ukanifafanulia? inawezekana shule yangu ipo outdated....
Nimekuelewa ,kwanza tuanze na kuanika nguo za ndani nje.kuna bacteria mmoja anaitwa staphylococcus saprophyticus huyu mdudu anapenda kuishi kwenye udongo au vumbi, sasa unapoanika chupi nje kama ikidondoka chini au ikipitiwa na vumbi yule bacteria anaweza kuingia ndani ya hiyo chupi na ukija kuivaa unahatari ya kupata U.T.I.
Hivyo kiafya inashauriwa kuwa ukianika chupi nje ni vizuri uifunikie na kitambaa chepesi kinachopitisha mwanga.Pia kwa upande wa maji kwenye maji machafu kuna bacteria anayeitwa Salmonella Typhi,huyu mdudu ni maarufu kwa kusababisha ugonjwa wa Typhoid pia inasemekana kuwa huyu mdudu anauwezo wa kusababisha ugonjwa wa U.T.I kama akiingia katika mfumo wa mkojo lakini hii ni mara chache sana kutokea.
Nazani umenielewa.