Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Wakubwa hachana na madawa ya madukani, tumia mchai chai, chemsha kama chai usichanganye na chochote, weka tu sukari, kunywa asubuhi na jioni, kwa kifupi ifanye kama chai yako, malaria, UTI, na magonjwa mengine utayasikia kwa jirani
Wakuu tofautisheni mkojo mchafu na UTI. Mkojo mchafu kweli unatibika na mchaichai, mpapai, kitunguu swaumu nk. Lakini UTI ni bakteria. Huwezi kumuua bakteria kwa mchaichai. Tutofautishe vitu hivyo....
 
Inawezekana kujinunulia dawa hovyo na kwenda dispensary za uchochoroni ndio shida yako...
Ushauri:
1. Nenda hospitali kubwa kuanzia ngazi ya wilaya uonane na wataalamu
2. Omba wakufanyie culture &sensitivity ya huo mkojo
3. Piga ultrasound ya figo, kibofu, ureters ili kuonekane kama kuna shida pia
4. Warudie vipimo routine kama urinalysis, etc
 
Inawezekana kujinunulia dawa hovyo na kwenda dispensary za uchochoroni ndio shida yako...
Ushauri:
1. Nenda hospitali kubwa kuanzia ngazi ya wilaya uonane na wataalamu
2. Omba wakufanyie culture &sensitivity ya huo mkojo
3. Piga ultrasound ya figo, kibofu, ureters ili kuonekane kama kuna shida pia
4. Warudie vipimo routine kama urinalysis, etc
Mh! Uwe vizuri financially. Siku hizi afya zimekua mitaji ya watu.
 
FANYA MTINDI NDIO KINYWAJI CHAKO!IKIWEZEKANA KUNYWA KAMA UMETUMWA NA KIJIJI!
UTI UTAISKIA KOROMIJE!
 
Nimekuelewa vizur sana lakini hujanipa kipimo cha hyo dawa kama ni kijiko,glass au jagi
Uwe na msimamo
mm nimeandikiwa Cefuroxime 500mg lkn wapi!
Tumia nitrofurantoin mkuu(1*4) ... Na chagua moja dawa za kienyeji au za kizungu..."usichanganye"..kikubwa zingatia ushauri wa kufanya culture and sensitivity.. Ukiweza fanya hiyo ultra-sound ya kibofu,figo..kikubwa zingatia ushauri dakitari kutoka hospitali inayoeleweka..
 
Habari za kazi wakuu
Natanguliza shukrani kwa mungu kwa kutupa nafasi ya kuwa hai na kukutana kwa ajili ya mijadala mbalimbali kwenye uwanja huu.

Niende moja kwa moja kwenye point...

Nasumbuliwa sana na ugonjwa wa UTI(Urine Track Infection) na kiukwel nimetumia dawa nyingi sana na kwa kufuata masharti husika ya dawa, lakini kila ninapomaliza dose nikikaa siku kujisikilizia ili nikapime tena naanza kuhisi dalili za uwepo wa ugonjwa huu na mara nirudipo hospital kwa ajili ya vipimo ungojwa huwa bado upo na madaktari huamua kunibadilishia dozi.

Nimebadilishiwa dozi nyingi mpaka sindano lakini sijapona na huu ni mwez wa tatu sasa tangu ugonjwa huu uanze kunisumbua.

Ni matumaini yangu nitapata msaada japo wa mawazo na dawa nzur ya kutumia ili kutibu ugonjwa huu ambao sasa umekuwa sugu.Naomba msaada wenu kwa hili tatzo wakuu na mungu atawabariki.


Pole sana ndugu yangu. Sijajua ni wa jinsia gani lakini ilimradi umelileta inaweza kusaidia wengine hasa wadada. Wadada/ wamama wengi wanapata shida hii mara kwa mara bila kujua chanzo. Wengine husingizia vyoo vichafu lakini kuna sababu moja wengi hawaijui. Wadada wengi wakioga wanapenda kujisafisha kwa sabuni sehemu za uke tena kwa kuingiza povu na vidole na kujisugua kuhakikisha usafi. Hili ni kosa kubwa. Sehemu za siri za mwanamke kwanza zina mdomo ambao uko wazi muda wote, pili zina bacteria ambao kazi yao ni kushambulia bakteria yeyote toka nje kuingia ukeni. Hawa wako kwa kila mwanamke. Kwa hiyo unapotumia povu la sabuni kusafisha ukeni unawaua hao bacteria kwa sababu sabuni nyingi zina kemikali. Hivyo unabaki bila ulinzi wowote na ndio maana asilimia kubwa ya akina mama wana tatizo la kujirudiarudia la U.T.I. Kuepuka hilo unapooga tumia sabuni sehemu zingine lakini usitumie huko ikulu. Tumia maji tu kujisafisha vizuri na hutakuwa na hilo tatizo tena.
 
Nenda hospitali nzuri,ushatumia antibiotics nyingi na hili limaweza likawa tatzo,ufanye kipimo cha culture and sensitivity ili ijulikane dawa gani inafaa Kwa aina ya bacteria ulionao!!
 
Kama kweli unasumbuliwa na hilo tatizo, fanya kipimo cha Urine Culture and sensitivity, kitakusaidia ila binafsi naamini kwa sasa msemo wa dawa fulani inatibu kila bacteria asababishaye magonjwa ni uwongo kwani level ya resitance kwenye antibiotic ipo juu hasa e.coli wasababishao urinary tract infection
 
U.T.I ni nini (kwa hisani ya saad ebr)
(U.T.I) MAAMBUKIZI YA NJIA YA MKOJO (URINARY TRACT INFECTIONS -UTIs)
Neno U.T.I si geni masikioni mwa wengi, kwani ni wengi leo utawasikia “naumwa U.T.I”. Japo si wote hulitumia kisahihi. Wengine wana tatizo ambalo ni tofauti na U.T.I, lakini anaweza akaenda hata duka la dawa na kuomba apatiwe dawa za U.T.I. Leo nimeona tubadilishane elimu juu ya hili tatizo, angalau kila mmoja awe na uelewa U.T.I ni nini hasa, inasababisha na nini, na ni jinsi gani anaweza kujikinga.
U.T.Is, ni kifupisho cha Urinary Tract Infections, ambayo kwa lugha yetu ni maambukizi ya njia ya mkojo. Kama linavyojieleza, kwamba maambukizi ni lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo ndipo tunaita ni U.T.I, na si pengine popote. Una uchafu unatoka ukeni, hiyo ni kitu kingine tofauti nk. Tunapozungumzia njia ya mkojo, ni kutoka eneo la nje hadi kwenye kibofu, na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo.
Kama maambukizi yako eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo(ikihusisha na figo pia), inaitwa Lower Urinary Tract Infect. Na ikihusisha eneo la juu ya kibofu, inaitwa Upper Urinary Tract Infection.
Tatizo hili huwapata wote, wanaume na wanawake. Lakini huwapata zaidi wanawake kutokana na tofauti za kimaumbile. Hii ni kwa sababu kuu mbili, i)njia ya haja ndogo ya mwanamke iko jirani zaidi na njia ya haja kubwa ambapo vijidudu vingi visababishao U.T.I ndipo vinapoishi, ii) mrija wa mkojo (urethra) wa mwanamke ni mfupi ukilinganisha na wa mwanaume, hivyo kufanya iwe rahisi kwa maambukizi kufika kwenye kibofu kwa mwanamke kuliko kwa mwanaume.
Visababishi
Tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bacteria ambao makazi yao ya kawaida utumbo mpana, na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa, mfano Escherichia coli na wengineo. Pia, linaweza likasababisha na ‘fungus’ na visababishi vingine, japo ni mara chache sana.
Vihatarishi na Njia ya Maambukizi
a)Kwa wanawake
• Kujamiiana –hii huweza kuamisha bacteria walio kwenye uume moja kwa moja, ama watokanao na maambukizi ya ukeni kuingia moja kwa moja njia ya mkojo
• Kuchezea ama kuchezewa na mikono michafu maeneo ya uke kunaweza kusababisha maambukizi
• Njia mbaya ya kujisafisha baada ya haja kubwa au ndogo inaweza kuhamisha bacteria walio ktk njia ya haja kubwa na kuingia njia ya mkojo
• Matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambao huua bacteria wa asili wa eneo la uke na kukaribisha bacteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi
Vifuatavyo pia vinaweza vikachangia
• Ujauzito –mara nyingi hushusha kinga ya mwili ya mjamzito
• Upungufu wa homon ya ya kike Oestrogen husababisha bacteria wasababishao U.T.I kuzaliana kirahisi
b)Kwa wanaume
• Matatizo ya tezi ya kiume(prostate) mabapo husababisha mrija wa mkojo kuziba, ama kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bacteria kujenga makazi
• Kutotahiriwa, ambapo nyama ya mbele inaweza kuhifadhi bacteria wasababishao U.T.I
• Kujamiiana kinyume cha maumbile huingiza kirahisi bacteria walio njia ya haja kubwa kwenye njia ya mkojo
• Kujamiiana bila kinga na mwanamke ambaye ana maambukizi ukeni
• Kuwa na VVU ambapo hupunguza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi
c)Kwa wote
• Kutokunywa maji na vinyaji kwa wingi –kunywa maji mengi husababisha mkojo kuzalishwa kwa wingi, na kukojoa mara kwa mara na hivyo kusafisha njia ya mkojo
• Kuwekewa mirija inayosaidia kutoa mkojo nje inaweza pia kukaribisha maambukizi
• Matatizo ya figo na mengine kwenye njia ya mkojo yanayoweza kuziba njia ya mkojo
• Kisukari ambapo hudhoosha kinga ya mwili na pia kuharibu mfumo wa figo wa uchujaji
Dalili za U.T.I
a) Kwa eneo la chini la njia ya mkojo
i. Hali ya kujisikia kutaka kukojoa muda wote
ii. Maumivu, au hali ya kujisikia kuchoma choma wakati wa kukojoa
iii. Kukojoa mara kwa mara na mara zote mkojo ni mdogo
iv. Mkojo unaweza kuonekana una ukungu, na mara nyingine unatoa harufu kali
v. Maumivu ya nyonga kwa wanawake
vi. Maumivu ya rektamu(rectum) kwa wanaume
vii. Na mara nyingine damu kwenye mkojo
b) Kwa eneo la juu la njia ya mkojo
i. Maumivu ya tumbo(hasa eneo la juu kwa pembeni –chini ya mbavu)
ii. Homa kali
iii. Kutetemeka na kujihisi baridi
iv. Kichefuchefu na /au kutapika
Vipimo na matibabu
Mara nyingi kipimo cha mkojo kinaweza kuonyesha tatizo.
Matibabu ni antibiotic baada ya daktari kubaini tatizo
Madhala yatokanayo na U.T.I isipopata tiba sahihi
• Inaweza ikasababisha maambukizi makubwa ya figo(pyenephritis) ambayo yanaweza kusababisha uharibifu wa kudumu wa figo na hivyo kutishia maisha
• Kwa wajawazito inaweza kuhatarisha maisha ya wote mama, na motto aliye tumboni
• Bakteria wanaweza kuingia mfumo wa damu na kusababisha ama kwenda kusababisha madhala mengine
• Inaweza kusababisha shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji wa kazi mbovu wa figo
Tiba mbadala nyumbani kabla ya kumwona daktari
Unaweza kutibu, ama kupunguza tatizo nyumbani kabla ya kumwona daktari pale uonapo dalili ya awali ya U.T.I, ambayo ni maumivu na kuchomachoma wakaji wa kukojoa. Fanya yafuatayo
i. Kunywa maji mengi hasa saa 24 za kwanza baada ya kuona dalili. Hii itasaidia kuzalisha mkojo kwa wingi na kusafisha njia ya mkojo
ii. Kojoa mara kwa mara na hakikisha ni hadi mkojo unaisha ili kibofu kiwe tupu
iii. Kwa maumivu ya mlango wa mkojo, oga na kuosha kwa maji ya moto, kutapunguza maumivu
Njia za Kujikinga na U.T.I
Kunywa maji na vinywaji kwa wingi kila siku. Hii itakusaidia ukojoe mara kwa mara na kutoruhusu bacteria kujenga makazi kwenye njia ya mkojo
Kojoa kila ujisikiapo mkojo na usiubane kwa muda mrefu
Kwa wanawake
Nenda ukakojoe mara tu umalizapo tendo la kujamiiana. Hii itasaidia kutoruhusu bacteria kuingia na kujenga makazi kwenye njia ya mkojo.
Badili pedi mara kwa mara uwapo hedhini
Epuka kujisafisha ukeni na maji yarukayo kwa kasi, pia epuka kupilizia marashi ukeni, ama kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu. Hizo huua bacteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bacteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi
Ujisafishapo baada ya kujisaidia anzia mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha bacteria walio eneo la haja kubwa kuingia njia ya mkojo
Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauliana na daktari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni kuwasaidia kujikinga na maambukizi
Kwa wanaume
Kuhakikisha maeneo ya ncha ya uume ni masafi mara zote, hasa ikiwa hujatahiriwa kuepusha kujihifadhi na kuzaliana kwa vijidudu visababishao maradhi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom