Ureno watafanikiwa kutetea Euro Cup, Sioni wa kuwazuia

Sijui kama ni macho yangu au ndo ukweli wenyewe, CR7 ameshafika mwisho sasa, kwa ile pace aliyokuwa nayo ujanani, siwezi kushangaa katika umri wake huu ila naona kama atafifia kwa kasi sana, ni bora apumzike kwa heshima tu, ameshafanya karibu yote kwenye soccer, lililobaki ni wazi haliwezekani, hivyo akubali yeshe tu😊 asisubiri kusajiliwa na Sheffield Utd au kwenda Uchina au US.
Ronaldo amethibitisha kuwa umri ni namba tu!! Wanaoitwa vijana hawana ubavu wakupambana naye! Mbape ni kijana sana lakini katika mechi tatu kwenye kundi lake amefunga magoli mangapi? ni 0!! Ronaldo kwenye kundi hilo hilo amefunga 5!! Serie A ameibuka mfungaji bora! Na mwakani atakiwasha kwenye kombe la dunia na hana mpango wa kwenda Marekani! Mwenye mpango wa kwenda Marekani ni Messi!! Tayari Messi yuko kwenye mipango ya kusajiliwa Marekani kwenye timu inayomilikiwa na David Bekam.
 
Siku wanacheza na Ufaransa waliponea bahati tuu.

Sema hivi wewe ni mpenzi wa Ureno hususani CR 7 ndio maana unajifariji.

Ureno wanaweza ishia kwa Ubelgiji
 
Timu ya Ureno chini ya nahodha Ronaldo itafanikiwa kutetea ubingwa wa mataifa ya ulaya. Japo waliteleza kwa kujifunga mabao mawili dhidi ya Germany na yakawachanganya hadi kupoteza mechi hiyo, lakini kikosi chao kimekamilika sana. Dalili kuwa watabeba kikombe itaonekana watakapocheza na kinara anayeshika namba moja katika ranking ya FIFA kwa sasa yaani Belgium. Belgium igakiona cha mtema kuni! Baada ya hapo ni mtelemko!! Ronaldo kuibuka na kiatu cha dhahabu.
Labda wachezaji wa Spain wauliwe
 
Back
Top Bottom