Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada

Vipi heleni? Au kusuka nywele? Hivi leo tutaweza kusema kweli hivyo ni vitu vya wakina mama tuu?

Au tuangalie ndonya ya wamakonde. Hii mbona baada ya muda wake kupita imepotea. Lakini naamini mjanja ukii-market ulaya ambako vijana wanajitoboa kila sehemu,, unaweza kupata market! Na wakianza wao basi na sisi tutawaiga.

Amandla....

Kabisaa hapo nakubaliana na wewe fundi!
 
Na kwa kuongezea tu,
Hizi tafsiri mbaya za hereni na vikuku hao wa magharibi ndio waliotupatia... maana kwa jadi zetu vikuku na vishaufu ni utamaduni wa makabila mbalimbali ya kiafrika! Inachekesha jinsi tulivyo wepesi kuiga hata kama ni kujidhalilisha!


enhee WoS,, hizi tafsiri ni za kuiga wakati uvaaji huo ulikuwepo tangu enzi na hakukuwa na tafsiri mbaya kuhusu hivyo.....kwa hiyo lawama zimwendee mtafsiri na sio mvaaji!
 
DSC07523.JPG

Katika pita pita mitaani si haba kuona wadada kwa kina mama wamevaa vikukuu miguuni eti hivi iwa vinamaana gani?
Nasikia kila mguu unamaanake kama mguu wa kishoto unamaanake hata wa kulia pia unamaanake.
Je ukichanganya yote inakuwaje ?
Nawakilisha wadau.
 
Kuweza kumuelewesha ina maana ulimuelewa.

Swala si kuelewa tu, swala ni kutumia maneno sahihi pia. Kama mimi nilielewa inawezekana wengine wasingeelewa, maana ya kuwa na lugha ni nini kama si kutumia maneno yaliyokubalika?

Kwa msingi wako ukisalimiwa jambe au jamba instead of hujambo itakuwa poa tu? Sasa anayechemsha atajuaje kama wewe utaelewa au hutaelewa? Kama huwezi kusema na/au kuandika Kiswahili kubali kujifunza au tumia lugha nyingine, lakini kamwe usitetee mmomonyoko wa lugha.

Tusiwe vichwa ngumu tunapokosolewa, tutakuwa hatujifunzi.
 
Swala si kuelewa tu, swala ni kutumia maneno sahihi pia.

Kutumia maneno sahihi ili iweje zaidi ya kuelewana?

Ndege wa angani na wanyama wengine hawana "maneno sahihi," kama wana maneno, na bado wanakaribia kuelewana. Fahari la ngo'mbe linafahamishwa na jike kwamba sasa ni wakati wa kuumba ndama. Na katika zizi zima, fahari huwa halifati-fati jike lolote ambalo halina mpango wa kupata ndama kwa wakati huo. Mhusika linamjua bila "maneno sahihi." Linajuaje?

Kama mimi nilielewa inawezekana wengine wasingeelewa...

"Kama mimi nilielewa inawezekana wengine wasingeleewa..."

Hebu rudia tena? Umeseje hapo? Angalau aliyesema "kikukuu" alieleweka!

maana ya kuwa na lugha ni nini kama si kutumia maneno yaliyokubalika?
Maneno yaliyokubalika na nani? Maneno mapya yanaingiaje kwenye msamiati?

Kwa msingi wako ukisalimiwa jambe au jamba instead of hujambo itakuwa poa tu?
Lugha haina ukamilifu. Atakaesema "hujambo" na atakaesema "jamba" wote wawili hakuna mwenye uhakika wa kueleweka. "Jamba" lina maana nyingi, ya kwanza si neno la kupendeza, na la pili ni neno la kitaalam, yani nafasi yenye hewa iliyoko tumboni. Hujambo ni salaam, na pia ni jina la mtu. Nikikupa mkono nikasema "Hujambo," naweza kuwa najitambulisha, wewe ukaanza kunipa historia ya afya yako kumbe hata sijauliza, maana ninakotoka mimi "Hujambo" ni jina la mtu!

Sasa anayechemsha atajuaje kama wewe utaelewa au hutaelewa?
Vyovyote iwavyo kamwe hawezi jua. Lugha si timilifu. Nikipayuka "BLURAY..." utageuka kukurupuka kuitikia au utaangalia kwanza kama nashangilia kuokota sahani ya kisasa ya kurekodia muziki? Utajuaje kilicho mawazoni mwangu? Lugha inaweza kuwakilisha fikra?

Kama huwezi kusema na/au kuandika Kiswahili kubali kujifunza au tumia lugha nyingine, lakini kamwe usitetee mmomonyoko wa lugha.
Kila mmomonyoko hupelekea mkusanyiko. "Kikuku" likimomonyoshwa linaweza kuzaa "kikukuu" na "kikuu" katika msamiati mpya. Ukiliangalia kwa mapana, unaweza kuanza kuelewa kidogo ninachoongelea.

Tusiwe vichwa ngumu tunapokosolewa, tutakuwa hatujifunzi.
Kweli, tusiwe vichwa ngumu. Na tusiwe vichwa panzi kukubali kubali vitu bila kuvichuja. Nikisema nimeelewa bila kukubaliana nacho ina maana nimeamini. Sitaki kuamini, nataka kujua: kama haeleweki umejuaje ni kikuku na sio kikukuu au kikuukuu?
 
ni urembo tu...... wenye yao ndio hutafsiri vibaya

Naona raia wameanzisha ligi baada ya kumwelewesha ndugu yetu. Fidel80, nadhani dada hapo juu kakujibu vizuri sana. nikweli niurembo tuu. Hata mimi nilisha ambiwa kuwa kikuku kinamaana yake mguuni tofauti na urembo. kwa kifupi watu wanaassociate mvaaji kikuku na ''Naughty gal''. Binafsi nimefuatilia kwa undani zaidi kuanzia hapo Bongo mpaka huku kwa wajomba. Kimsingi kuna ''naughty gal'' wanavaa vikuku may be ni identity kwao, lakini uvaaji vikuku hauja anzia Bongo wadada kwa wamama almost all over the world wanavaa kama urembo tuu pasipo kuwa na maana kama inavyodhaniwa na baadhi ya watu Bongo. Hivyo ndugu yangu elewa kikuku ni sehemu ya urembo wa kinadada.

Nawakilisha
 
Hahahaha yeah ukivaa mguu wa kushoto kibongo bongo ndo unatoa jicho teh teh teh huna haja ya kuuliza.


hakuna lolote, mie ndio mguu ninao valia, na ni urembo kama ninavyoweza vaa hereni vile...
 
Back
Top Bottom