Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada

Discussion in 'Urembo, Mitindo na Utanashati' started by WomanOfSubstance, Dec 24, 2008.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nini madhumini na matumizi ya vitu vifuatavyo wavaapo wakina dada na akina mama katika jamii yetu?

  1: Kipini cha puani a.k.a (Kishaufu) iwe kushoto au kulia
  2: Kikuku iwe mguu wa kushoto au kulia au yote kwa pammoja
  3: Na mwisho ni Shanga za kiunoni.

  Je, waonaje? Vyapoteza maana halisi kwa wanaovaaa hole hole hole au?

  Maoni yako tafadhali changia..


  ======================================
  MAJIBU YALIYOPATIKANA
  ======================================

  Nimeona nilete mada hii ili kuwekana sawa katika ishu ambayo inaongelewa pasipo kuwa na ufahamu wa kina. Katika mapambo yanayotumika sana ulimwenguni na tena na watu wa marika tofauti ni pamoja na vikuku na vishaufu.

  => Kuhusu vikuku miguuni

  [​IMG]

  Kwa makabila ya kiafrika vikuku huvaliwa kuanzia na watoto wachanga, wasichana, wanawake wa makamo na hata vikongwe.

  Vikuku hivyo vyaweza kuwa vya shanga, ngozi, au hata madini kama dhahabu, fedha na hata shaba. Vyaweza kuvaliwa mguu mmoja au hata miguu yote.

  [​IMG]
  => Kuhusu uvaaji wa Vishaufu/kipini puani
  [​IMG]
  Tukirudi kwa vishaufu, urembo huu ambao huvaliwa puani aghalabu hupatikana kwa makabila ya pwani lakini kwa miaka ya karibuni umeenea hata kwa makabila mengine hasa kwa wasichana.

  => Kuhusu uvaaji wa shanga kiunoni  Hitimisho:
  Kwanini basi naleta hii ishu tuijadili ni kwamba, hapa JF nimesoma baadhi ya wachangiaji wakihusisha hasa vikuku na mienendo isiyofaa na kuleta dhana kuwa wenye kutumia mapambo hayo basi wana ajenda nyingine.

  Binafsi napenda kusema kuwa urembo wowote waweza kutafsiriwa vyovyote - kwa ubaya au uzuri ila mwisho wa siku mtumiaji/mvaaji tu ndiyo mwenye kujua maana.

  Wenzangu sijui mnasemaje?

   

  Attached Files:

  • pini.jpg
   pini.jpg
   File size:
   26.9 KB
   Views:
   29,553
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Nakumbuka mada kama hii imewahi kujadiliwa hapa kitambo kidogo.... Well, mimi bado nasema kuwa kikuku kina maanisha kitu fulani... na anayejipamba kwa kikuku huwa analengo la kufikisha ujumbe kuwa mambo fulani hapo kwake ni ruksa...!
   
  Last edited by a moderator: Dec 24, 2008
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nijuavyo mimi kikuku ni pambo kama kuvaa hereni, bangili au mkufu.Je hicho kitu kingine unachosema wewe ni kipi maana tunaelimishana hapa.

  Nimewahi kusikia pia kupaka wanja,kupaka hina, au kuvaa kofia zile za wenzetu watu wa pwani kuna maana yake.Je hizo maana ni of universal application?
   
 4. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Hapa naomba mtu yeyote aniambie kila pambo analovaa mtu wa jinsia hasa ya kike na maana yake;ikibidi hata jinsi ya kiume pia.
  Binafsi sina la kusema zaidi ya hapo,labda nikisha pata maelezo ya awali inaweza kunisaidia mimi na wengine pia.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,465
  Trophy Points: 280
  Dada zetu na mama zetu, mapambo ni kwa kiasi yakizidi ni tatizo. Kwa upande wa vikuku mimi sikujua ni batili mpaka pale Mwana FA katika wimbo wa 'Mabinti' aliposema 'Unaona shanga za miguuni naita vikuku, japo kwa wenye ufahamu ni batili'.

  Ukweli unabaki kuwa wadada wamama jipambeni kwa kiasi. Naamini hata wewe ukiona mapambo yanazidi yanageuka kero. Mimi naomba nikupeleke deep zaidi kwenye saikolojia ya mapambo. Kwa vile lengo la mapambo toka enzi na enzi ni kumfanya mwanamke apendeze na mwanamke akishapendeza amini usiamini anakolea zaidi katika mambo fulani.

  Wanawake walioongoza kwa kuvaa dhahabu walikuwa wanawake wa Kimisri enzi za Malkia Cleopatra. Mapambo haya yalifikia kilele chumbani wakati wanawake hawa walipojifunua miili yao na kubaki kama walivyozaliwa na walianza kucheza kila aina za mikatiko huku wakisaula kimoja kimoja hatimaye walibakisha shanga za kiunoni, vipini na vikuu na shughuli ilifuatia.

  Mpaka leo wanaoongoza kuvaa mapambo hswa dhahabu ni wanawake wa kiarabu lakini mapambo yote ndani ya baibui mpaka muda muafaka wa kujifunua tena kwa mlengwa pekee.

  Kutokana na dhahabu kuwa ghali, wadada zetu ili kuonyesha jeuri ya pesa sasa ni kupanga macheni, mapete na mahereni lukuki tena wengine mpaka shanga za dhahabu!. Na asienavyo si haba shurti aazime.

  Hapa ndipo kwenye matatizo. Mapambo yakizidi ni dalili ya inferiority complex kwa baadhi ya wanawake kujipamba kupindukia ili kujiridhisha nafsi zao kwa sasa wamependeza. Wajipambao kwa dhahabu ama wametoka familia duni na sasa wamepata wanataka kuutangazia ulimwengu wote hiyo sasa ndio thamani yao. Wanawake matajiri wa kiukweli wanavaa mapambo simple tuu halafu nenda kwenye mkesha wa mdundiko
  Uone mijimama inavyoshindana kwa dhahabu.

  Namalizia na pambo la ndani la shanga za kiuno. Baadhi ya wanawake wanaamini shanga hizo huwapagawisha wenzi wao. Basi utawakuta wengine wanafikiri ukizidisha idadi unakuwa bingwa zaidi. Niliwahi kuzihesabu za bingwa mmoja a Tanga, alinivalia 40!. Kwa vile mie sio hoi kwa somo hilo, huyo dada japo ulikuwa bingwa hilo zigo la maashanga kwangu lilikuwa kero kiasi cha kuharibu ladha yote ya somo zima!.

  Na sasa hivi visichana vinavyochipukia, vinavaa lundo la shanga mikononi kama bangili ili kukupa nafasi ya kujiuliza kama mkononi ndio hivyo, huko kwenyewe itakuwaje?!.
  Mapambo ni kwa kiasi tuu yakizidi inakuwa taabu.
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwa wanawake wa mwambao wa pwani kikuku ni zaidi ya pambo ni alama kuwa anakwenda zaidi ya mwanamke wa kawaida katika shughuli nyeti... Kwa wadosi sijui kama wana maana nyingine zaidi ya kujipamba kwani wao huwa na vikuku katika miguu yote miwili.

  Kupaka wanja na hina kwa wanaume wa Pwani ni suna, kwa kina dada hina ina sifa zake kutokana na shughuli inayokusudiwa ikiwa ni pamoja na arusi na mambo mengine katika mapenzi.
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ni vizuri umerudisha nyuzi hii. Kwa ufahamu wangu mdogo niliopata kwenye maelezo niliyopewa na mtu anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja, hivyo vipambo vina maana tofauti kwa watu tofauti. Sijui kwa watu wa pwani vina maana gani.

  Lakini kwa wanawake wanaovaa vikuku mguuni ishara yake ni kuwa hawana tatizo kwenda na kinyume na maumbile au wanafurahia zaidi kwenda hivyo(sijui kama hii ndio maana ya kina dada wetu hapa Tanzania), na kwa wanaume wanaovaa aina fulani ya hereni au kwenye sikio la kulia nao wanatoa ishara fulani kwa wanaume wanaovutiwa na watu wa jinsia yao, nakumbuka niliambiwa kuna ishara nyingi, nyingine ni natural zinatokana na physical appearence hasa kwa wanaume ambao ni feminine, na kwa wanawake ambao ni masculine, hii inatambulisha kwa urahisi kuwa wao ni homos, au uki-initiate kitu fulani basi kuna uwezekano mkubwa wa kupata response fulani.

  Kwa wanaovaa vipambo hivyo, kama wanaiga watu wa magharibi basi naamini kuwa wanatoa ujumbe kama wanaoutoa watu wa magharibi kwa kuvaa vipambo vya namna hiyo, kama sivyo basi watakuwa ni kama vijana wetu ambao wanajisifu kwa kujiita nigger bila kujua maana ya neno lenyewe.

  I am sure kuna members humu wanaofanya hivi na wanaojua kwa undani zaidi.
   
 8. O

  Onychomycosis Member

  #8
  Dec 24, 2008
  Joined: Dec 24, 2008
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikukuu najua kuwa kikivaliwa miguu yote na maana mvaaji anacheza Middle,foward na pia ana deffend kwa watu Kibunango nisaidie.
   
 9. O

  Onychomycosis Member

  #9
  Dec 24, 2008
  Joined: Dec 24, 2008
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unakosea woman ukivaa miguu yote wajuvi tunajua unacheza pande zoote kwamba unakaba unashambulia na vinginevyo...ukivaa kushoto pia kuna maana yake na ukivaa kulia kuna maana pia pia

  Rita Mlaki alivaa kushoto kulia?
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Naam, upo juu ya mstali...!
   
 11. M

  Mutu JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hivi vitu vilikuwa mambo ya kawaida tu hapo kitambo.Sasa inakuwaje kama kipindi cha leo wanao tumia vikuku kuwa ni wengi wao wanaujumbe fulani na wanatoa huduma fulani kunako faragha?Basi ndio imekuwa hivyo kuwa vikuku leo vina mana pana tu!

  Ndio maana watu wengine wakiona vikuku kama vya kina Rita mishipa inashtuka maana ndio imekuwa hivyo. Kwa hivyo kama wewe unavaa hujui vinamaanisha nini ni kama kutumia new code bila kujua maana yake,mnawatesa mabazazi tu.
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Dec 25, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mama weeee!!
  Jamani..mbona karibu nizimie kwa tafsiri mnazotoa!
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  Dec 25, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Binafsi sidhani kuna haja ya kujitia kiwewe ati mtu atakutafsiri vibaya kama hushiriki vitendo hivyo.The bottom line ni kuwa na kiasi.
  Kama mtu ataamua kujitafsiria vingine hiyo itakuwa juu yake.

  Najua kwa mfano, kuna wenye kutoa tafsiri hata ya wanja! Ati kuna ujumbe kama " sina mwenyewe" n.k. je tumefikia mahali pa kuwa waoga wa kufanya ile roho inataka kisa ati wajuzi wa kutafsiri watatafsiri?
  Na je kwa wale wenye kununuliwa mapambo hayo na waume au wachumba zao ikoje hiyo?
   
 14. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #14
  Dec 25, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Interesting !!!!!!!!!!!!!!!!!

  Kwa mantiki ya hoja yako. Wanawake wa kimasai ni mahiri kwa kucheza pande zote. [​IMG]
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Kama ambavyo binadamu tunavaa pete zinazoonyesha kwamba msichana yuko engaged au Mwanaume au Mwanamke ameowa au kuolewa.

  Nimeona katika baadhi ya nchi hivi vikuku wameviwekea maana maalum inayokubalika.

  Nakumbuka nilikuwa na email inayoonyesha maana ya hivi vikuku vinavyovaliwa miguuni (kuna maana tofauti kati ya kuvaa mguu wa kushoto na mguu wa kulia na kuvaa miguu yote) vina maana gani lakini bahati mbaya inaelekea niliifuta.

  Kwa Tanzania miaka ya nyuma wengi walikuwa wanavaa kama urembo tu lakini kwa miaka ya karibuni baadhi ya wavaaji hukusudia pia kupeleka message fulani kwa wale waangaliaji wa hivyo vikuku na vibata
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Hawa bado wanafuata mila zao za kuvaa hizo shanga miguuni. Hakuna ujumbe wowote wanaopeleka zaidi ya kufuata mila zao walizorithi kwa mababu na mabibi zao.
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Katika mavazi au mapambo yeyote kuna wale wanaovaa kwa kujifurahisha wao au wenzao na wale wanaovaa ili kutuma ujumbe kwa wale wanaoelewana lugha. Ubaya ni kuwahukumu wote kwa matendo ya wachache. Mwanamke ana uhuru wa kuvaa anavyotaka na kujipamba atakavyo ili mradi conscience yake haimshtaki. Sisi wengine inabidi tuangalie na kushukuru Mungu kuwa ameumba watu wa jinsia tofauti. Kama tunaona wafanyavyo hakutufurahishi, basi tugeuze macho na kupitia kwengine. Mimi sijali hizo maana zinazosemekana bali nafurahi kuona mguu ulioumbika umerembwa ipasavyo. Hayo mengine nawaachia nyie.

  Amandla.....
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nadhani kuna wanaovaa urembo huu bila kujua maana hizi... lakini na Rita naye hafahamu maana yake au alikuwa anatuma ujumbe fulani???
   
 19. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu nina hakika wamasai kuvaa wanavyovaa kunatoa ujumbe fulani, na kuvaa kwao sio kuiga ni kitu ambacho wamekuwa nacho toka enzi kabila lao lilipoanza na mapambo hayo yalipopatikana. Sio waigaji wanadumisha utamaduni wao na identity yao, ingawa mimi sio mmasai na sijui maana ya wanavyovaa, na ingawa kuna baadhi ya mambo ambayo wamasai wanafanya yanayoniudhi, lakini ukweli ni kuwa I AM VERY VERY PROUD of these fellow country people of mine.

  Kama Mlaki naye anavaa kutokana na utamaduni wa kabila lake i can be proud of her as well. Lakini kama anavaa kwa kuiga watu wa magharibi ambao maana yao ni kucheza kotekote, sitapinga kwa sababu ana uhuru wa kuvaa anachopenda na kutoa ujumbe anaopenda, this is all what democracy is about.
   
 20. M

  Mutu JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Yah hainatatizo kama hutojari nani atakuhisi vipi ilimradi wewe unajua unachofanya and you find it urembo.Binafsi mimi naona vinapendeza,sijuhi kwa nini hizi tafsiri zimekuja!
  Kuhusu wanja ahaaaaaaaaa sio wanja wote una matatizo kuna ile wanaopaka wale mashankupe unakuwa mithili ya chui kisha unakuwa mrefu sana kupanda juu,sasa ule wenyewe wanaopaka wanakwambia unaitwa "sina bwana" sasa sisi tusemeje!?
   
Loading...