Urembo ulionishinda mimi.....

Kuvaa wigi na wivin nilivaa wakati wa kipaimara . ...
Kufuga kucha na kubandika yani hata za miguu huwa nakuta vipisi tu na maumivu zimekatikia wapi hata sijui natembea miguu baja ha haha ...

Kuongeza kalio yani nimeletewa dawa mpaka na shuhuda mi hata hawanishawishi wameishia kuniita pasi na mbahili.. niongeze kalio halafu iweje Acha niendelee kutikisa mgongo
dada nina shida na wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
urembo ulionishinda ni kuvaa uchi au nusu uchi kwenye public, kutinda nyusi na kuchora mijiwanja, kubanika makucha maana sijui walibandika wanajitawazaje, kupaka lipstic iliyokolea mpaka unashindwa kumhag mtu, kuvaa kiatu kirefu zaidi ya nchi tano unakua kama ngongoti, kuvaa nguo za kubana mpaka maumbile ya mwili kuonekana kwenye public, kuongeza kope za bandia na kuvaa miwigi kwa kweli vimenishinda.
 
Kuna vingine sijawahi kujaribu, vingine nimejaribu vikanizidi uwezo....

1: kupaka wanja kwenye nyusi
Huu urembo ulinishinda tangu enzi za mwalimu, kila nikijaribu naona nakua Kama nyau hasa hasa wanja mweusi, basi nikijaribu kupaka nafuta naendelea na mambo mengine, mara chache nimejaribu wanja wa brown napaka kwa mbaaali naona unakuja kuja mdogo mdogo ntaweza.

2: kuvaa wig/kushonea weaving
Hapa nimeinua mikono, wig nilivaa mwaka flani wakati naanza kusokota dread siwezi kwenda kazini vile, nikanunua wig kwanza dukani tu naambiwa linauzwa elf 25 nikashtuka nlijua buku ten, nikanunua nikavaa mmh najiona nakua kama kanjibai, linawasha, lina joto nlipata shida, nywele zilivorefuka sijarudia tena huu urembo siuwezi kabisa.

3: kubandika kucha
Nilijaribu siku moja kutoa ushamba, naona shost angu kila siku anabandika anapendeza, akanipeleka namie nikabandika mmh siku hiyo hata kutandika kitanda nilishindwa, kuchomeka shuka kwenye godoro ikawa tabu, siku chache nikazoea, siku ya kuzibandua sasa yani zinang'olewa utadhani nimetekwa nlikua na kazi ya kupiga kelele kama kimbwa, sirudii tena sitarudia kabisa.

4: kubandika kope
Hii kujaribu tu siwezi make, nikiwaona kina mwajuma ndalandefu wanavokua huwa nacheka, kope zinasimama utadhani mtu kavaa kofia, yana wenyewe haya

5: kupaka cream/kujichubua
Hii kazi ya kujipa mateso hii, uso mweupe miguu myeusi, kuna siku nliwekewa maji ya cream bila kujua ushamba huu, nimeulizwa tu niweke maji nkajibu eeh weka nlijua labda glycerin, duh siku mbili tu nkaanza kuwa kama tumbili....

Wewe huwezi nini?

Nb: naombeni mniambie mafuta ya nywele natural, naona nywele zinakatika

Napenda mwanamke wa hivi

Ndio maana yule mchagga huwa namwambia awe ananyoa panki kama zamani.
 
Jaman kujiremba nimeshindwa kabisa, yaani nikipaka mafuta yangu uson,
Nimejiremba sana nina lipbalm mdomoni huyo napepea,
Najitahid hizo make up siwez sasa sijui ushamba
 
Hahha yani hayo yoooote ni kama umenipoint mimi,kope,kucha za bandia,wigi,wanja,mkorogo uwiiiiii emu nibaki na weusi wang
 
Urembo wa kuvaa skirt na magauni naelekea kuuzika kaburini

Mawigi,kucha kope siwezi kuacha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom