Urembo, Michezo na Usafi - Vipaumbele vya Watanzania

Mwakjj:
Kwa kutumia mashindano ya Urembo au Timu ya Taifa, brand yao inatangazwa nchi nzima na kuendelea. Kwa usafi, brand inabaki local.
Do we need some directive on ulimbwende and michezo?

Hii ndiyo biashara na walikuja kufanya biashara. Lakini je kuna haja ya kuwapa wafanya biashara directive yoyote kulingana na mahitaji ya nchi yetu? kumbuka wakati mwingine kupata kibanda cha kufanyia biashara na ikauzika huwa ni kazi ngumu, pamoja na kwamba unalipa mishahara.

Je ukipewa nchi nzima,unatakiwa kupewa ni nini matarajio ya nchi baada ya kulipa kodi? Nchi nyingine walio na uzoefu zinafanyaje?

Je katika Urembo huo huo ni warembo wangapi wameweza kufaidika na makampuni hayo hata kwa kuwasomesha baada ya kumaliza muda wao?

Je katika michezo ni wanamichezo wangapi wameweza kukumbukwa na makampuni hayo baada ya kumaliza kipindi cha kusukuma kabumbu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom