Urasimu mwingine, Afisa wa TRA anakukadiria kodi akiwa ofisini bila kutembelea biashara yako

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,973
1,398
Huu ni upumbavu mwingine mwingine wa maafisa wa TRA anakukadiria kodi akiwa ofisini bila kutembelea biashara yako, makadirio yanakuwa makubwa, ukilalamika anakwambia andika barua ya kuomba kupunguziwa kodi. Baada ya hapo anakwambia kodi haipungizwi kwa kuandika barua tu, mpaka tufike tuone biashara yako. Hapo swali linakuja mbona wakati unakadiria hiyo kodi hakuja kwenye biashara kwanza

Ujinga mwingine anakwambia ufuate ratiba yake pale anapokuwa na nafasi na umtafutie usafiri wa kumpeleka na kumrudisha
 
Achana na Tra. Tumia kitambulisho cha wanyonge. Wewe vipi?. Mnataka rais wa wanyonge aongee lugha gani uweze kumuelewa?.
 
Sasa mkuu unashindwaje kuzungumza na hao mafic mpaka unakuja kulala-mika humu wakati watu wako busy kuchambua utopole wa Humphrey Polepole
 
Imetoka hiyo jiongeze Acha uzembe mzee

Usimdanganye mwenzio bhana, hivyo vitambulisho ni kwa ajili ya machinga. Kama anafanya biashara na amepanga fremu hicho kitambulisho hakitamsaidia. Sana sana ndio watakuwa wanamtembelea na kuchukua hela ya maji kila siku ambapo kwa mwaka ukijumlisha ni bora kulipa tu hiyo kodi. Labda kama fremu iko ndani ndani huko..ila kama yuko sehemu peupe wakimtembelea kukagua leseni wakimkuta na hicho kitambulisho hakitamsaidia.
 
Ujinga mwingine anakwambia ufuate ratiba yake pale anapokuwa na nafasi na umtafutie usafiri wa kumpeleka na kumrudisha
hapo kama utaendelea kulia lia mjinga ni wewe,unatakiwa kumripoti kwa bosi wake badala ya kulia lia
 
Assumption ni kuwa kila mwaka biashara hukua tu hata ukibakiwa na frame tupu wao wataongeza kodi tu mwaka inaofuata.
 
Back
Top Bottom