Urasimu kwa Serikali kulipa wadeni wake na usumbufu wapatao watoa huduma

ChanjoSugu

Member
Oct 22, 2021
14
33
Kilio cha Wakandarasi na Wazabuni wa Serikali,Nini kifanyike watu wanateseka!

Kwa miaka michache ya karibuni serikali imeandaa utaratibu mpya wa malipo kwa Wakandarasi na Wazabuni wanaoidai serikali kutokana na huduma mbalimbali walizotoa.

Mfumo huu uitwao Gpay hutaka mdai kukamilisha taratibu zote na wizara anayoidai na kisha wizara husika kupeleka madai hayo wizara ya fedha kws hatua za mwisho za uhakiki kabla ya malipo.

Ni utaratibu mzuri iwapo ungelikuwa na ufanisi hasa kwenye Wizara ya fedha ambako inaelekea ama ni kwa kuelemewa na wingi wa madai ama urasimu kumekuwa na ucheleweshaji wa malipo ya wahusika kwa muda mrefu hali inayopelekea usumbufu na matatizo mengi kwao ikiwamo kulipa madeni ya watumishi wao na kubwa madeni ya mabenki yaliowakopesha mitaji.

Migogoro ya Mabenki na wadai wa serikali imekuwa mikubwa mabenki yakifikia hatua ya kuuza dhamana za wateja na wengine kukimbilia mahakama kuweka zuio na kuongeza mitafaruku na kuvunja mahusiano ya mabenki na wateja yaliyojengwa kwa uaminifu mkubwa na kwa muda mrefu.

Ukifuatilia sababu ya msingi ya madai haya kupita Hazina ambako yanapitia mikono zaidi ya watu kumi kuyaidhinisha utaona ni urasimu usio na sababu za msingi kwani Hazina sio wanaofahamu kipi kilichofanywa baina ya mzabuni/mkandarasi na wizara husika au Taasisi.

Kimsingi Hazina inapaswa kuangalia tu taratibu za kiserikali kama zilifuatwa kiusahihi wakati wa malipo.

Ni kama msimamizi wa mabenki yaani BoT alivyo kwenye usimazi wa uendeshaji wa benki za biashara na siyo kuwa mteja akitaka mkopo katika benki yake basi uidhinishwe na Benki kuu maana itapoteza mamlaka ya benki za biashara na kupoteza lengo la usimamizi la BoT huku ikielemewa na orodha za waombaji mikopo kutoka benki mbalimbali.

Kuendelea na utaratibu huu si tu kunawaumiza wadai wa Serikali bali pia kunadidimiza maendeleo ya miradi, maendeleo ya uchumi wa nchi na wa makampuni ya sekta binafsi na mtu mmoja mmoja kwa maana ya wafanyakazi waliotumika na makampuni kukamilisha kazi mbalimbali.

Tunatoa wito kwa serikali kupitia utaratibu huu na kufanya marekebisho ili malipo yakamilike kwa muda katika Wizara na Taasisi husika huku wizara ya fedha nayo wakiendelea na utaratibu wa kupitia malipo yaliyofanywa na wizara zingine na Taasisi zake.

Kwa kuzingatia hili na kuchukua hatua stahiki tunaamini kuwa tutaongeza kasi ya maendeleo ya Taifa na watu wake
 
MALALAMIKO MFUMO WA MALIPO YA HUDUMA ZILIZOTOLEWA SERIKALINI

Kama mtumishi wa umma anaweza kudai laki mbili kwa miaka kumi halipwi hao wengine itakuwaje?
 
Mdau kama una madai mbona simple tu nenda pale magogoni muone Lukuvi kapewa kazi hiyo ya kusimamia wizara uone kama itapita wiki,cha msingi nyaraka zako za madai zitimie..ikiwa kuna mtu hakuwajibika basi bench linamuhusu watu wengi hawana kazi wanatafuta hizo nafasi
 
Serikali wagumu sana kulipa.

Hata pesa za mirathi tu warithi huwa wanazungushwa sana kulipwa.

Yaani pesa zako unaweza weka benk crdb ama nmb. Siku ukifa benk zitatuma hizo pesa kwenye account za mahakama hazina. Ili mahakama ilipe warithi. Hapo ndipo balaa linapoanza
 
Back
Top Bottom