Urasimu kutoa vibali kwenda masomoni majeshini.

Boko halal

Senior Member
May 14, 2014
175
124
Ninaomba mamlaka juu (mawaziri) ziangalie swala hili kumekuwepo na urasimu wa kila aina kuzuia askari wanaotaka kwenda masomoni kwenye majeshi yetu (polisi, magereza na JW) askari wanaotaka kwenda masomoni hunyimwa vibali wakati mwingine hutishiwa kuhamishwa kwenda maporini. Unaweza kufanya kazi hata miaka 10 lakini ukaomba kibali cha kwenda kujiendeleza kielimu ukanyimwa lakini wakati huo huo kuna watoto wa wakubwa wanaajiriwa hawamalizi hata miaka 3 kazini (kama utaratibu unavyo taka) wanapewa vibali vya kwenda masomoni hii inavunja moyo kwa askari wetu wanaofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha nchi yetu ni salama, swala la kujiendeleza kielimu ni haki ya kila mtumishi wa umma aliyetayari.
Matokeo ya kunyimwa vibali yamepelekea askari wengi sana kuacha kazi na kwenda kujiendeleza kielimu hali ambayo inawapunguzia nguvu kazi majeshi yetu.
Utaratibu wa utoaji vibali uangaliwe upya ili kuondoa manung'uniko kwa wapiganaji.
 
Suala LA ruhusa lina utaratibu wake....ikumbukwe wanaoomba ni wengi sana.....jeshi haliwezi kuruhusu watu wote waende kazi atafanya nani???


Ila si kuna Open university of Tanzania waombe huko..suala LA watu kwenda masomoni kwa upwndeleo.....majeshini lipo sana tu..
 
Back
Top Bottom