Uchaguzi 2020 Urambo, Tabora: Dkt. Magufuli 'akandia' sera ya majimbo; asema inakaribisha mafarakano na umasikini kwa Watanzania

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,778
Kampeni za urais zinaendelea na leo mgombea Urais kupitia chama cha mapinduzi, Dkt yuko Urambo. Kwa sasa aneongea ni Magreth Sitta na anawaombea kura madiwani, Rais na yeye mwenyewe kwenye nafasi ya ubunge kwa kupiga magoti mara tatu kwa kila nafasi.

3:28 Asubuhi: Dkt. Magufuli amewasili uwanjani na viongozi wa dini wanachukua nafasi yao ambao wamewakilishwa na Sheikh Zaid Nassor, Sheikh wa wilaya ya Urambo ambae anawaombea wagombea wote wapate wepesi katika safari yao, baba Paroko Edward Mtunge kutoka kanisa Katoliki Urambo analiyemuombea Rais Magufuli aendelee kuliongoza Taifa kwa salama na kuwaombea wapate kura mbunge na madiwani wa CCM na mwisho alimaliza Mchungaji Alfred kutoka Morovian na yeye aliliombea amani Taifa katika kipindi cha kampeni na kukiombea chama cha mapinduzi.

===================
Mmesikia kwenye Kampeni za hivi karibuni mnaambiwa yatatengenezwa Majimbo,Tanzania itagawanywa ni Chama fulani kina sera yake hiyo ya kuigawanya Tanzania katika Majimbo ya Utawala, ukishatengeneza Majimbo katika Nchi huo ndio mwanzo wa mfarakano”-JPM akiwa Urambo

Ukishagawanya Nchi katika Majimbo ni mwanzo wa ufarakano kwasababu kila Jimbo litakuwa linajitegemea lenyewe likiwa masikini linakuwa masikini wa kutupwa, Nyerere alipokuwa akiomba Uhuru wa Taifa hili angeligawa kwenye Majimbo tusingefikia hapa”-JPM akiwa Urambo



Tanzania tuna Makabila zaidi ya 121, Nyerere alituweka Watanzania kama Taifa moja, tangu 1961 hatujaingia mfarakano kati ya Kabila na Kabila, Dini na Dini, Maeneo, sitaki nitoe mifano ya baadhi ya Nchi ambazo ziliingia kwenye mtego wa Majimbo na wamefarakana”-JPM

Msisikilize maneno ya watu, mti wenye matunda ndiyo unapondwa mawe na watoto, hata mimi hapa mnasikia yanayozungumzwa juu yangu, tumehangaika tumeomba wote na Corona ikapotea na wao wakatukimbia lakini wakija hapa wanatutukana



 
STAMINA AKIPANDA JUKWAANI KUIMBA WIMBO WA CCM
CHAGUA CCM, CHAGUA DKT MAGUFULI
 
Ndugai sawa upinzani unapinga kila kitu hivi CCM inakubaliana na mambo yote ya upinzani? Ni sawa na Yanga kucheza na Simba na Yanga kuitakia simba ishinde tu.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Ila kweli Wana pingapinga kila kitu. HAKUNA hata Jambo moja wanakubali.
Wanawanyima haki yao wananchi katika maamuzi wamekuwa sio watetezi sahihi wa wananchi.

Naamini mwaka huu wananchi wanaenda kuwaweka pembeni kupata maendeleo.

2020 Wananchi wanaenda kuchagua maendeleo yanayosimamiwa na Chama cha Mapinduzi CCM
 
Aaaah ndio maana !! Amegoma kabisaa kusafiri nje ya Tanzania kwa sababu hataki kujifunza Jambo jipya kwake huyu dokta sijui lakini Ila tumfanye kumtoa alipo mbona makusanyo ya hela ya halmashauri toka amechukua halmashauri zinazidi ktota naona Sera ya majimbo ndio nzuri kuliko hata anavyojua atanyimwa ulaji mkubwa. Akikende tu sisi tutatengeneza miji yetu Safi kabisa.
 
Sera ya majimbo inaonekana haifai! Taifa linalompa misaada mingi lina majimbo Huyo huyo anasema "usiponichaguria kijani hapa sireti maji nawambia ukweri" mwisho anasema tena "maendereo hayana chama"
 
Ndugai sawa upinzani unapinga kila kitu hivi CCM inakubaliana na mambo yote ya upinzani? Ni sawa na Yanga kucheza na Simba na Yanga kuitakia simba ishinde tu.


Ndukiiiii
Kama upinzani utakubaliana na yote ya CCM, dhana ya upinzani inakufa. NEC inaubana upinzani kwenye mikutano ili CCM na hasa Magufuli asiumbuliwe kwa madudu yaliyofanyka miaka hii 5.
 
Sijui anafikiriaje hiyo mifarakano na tofauti za maendeleo!! Mpaka muda huu ambao hakuna majimbo hayo, bado kuna tofauti kubwa sana kati ya wilaya ya arusha na longido!!

Bado tuna tatizo na kuwa comfortable na tulichonacho na kuogopa tusichokuwa nacho tukiamini hatuna uwezo wa kukipata!!! Majimbo kujipangia maendeleo yao ni jambo sahihi kisiasa kwa sababu tuna mfumo wa serikali za mitaa!! Zipewe majukumu na uwezo zaidi!!! Lissu kwa jambo hili naona yuko sahihi kuliko wapinzani wake!
 
Back
Top Bottom