Elections 2010 URAMBO: Jeshi la wanyama pori laua wapinzani 25

Emma Lukosi

JF-Expert Member
Jul 22, 2009
929
147
Kuna habari Zimenifikia hivi punde kutoka urambo tabora kuwa jeshi la wanyama pori
Urambo, Tabora limechoma nyumba za kijiji kimoja na kuua watu 25 kwa kuwasingizia
kua ni Majambazi.
Watu hao ambao inasemekana ni wafuasi wa CUF na wapinzani wakubwa wa CCM
Walizushiwa kuwa wamevamia Eneo la wanyama pori na baadae nyumba zao kuchomwa
moto. Baada ya watu kuhoji kuwa watu wale walikuwapo hapo kwa mda mrefu na si wavamizi, Askari wale waliamua kuwaua.
Mwenye kina tunaomba atujuze zaidi.
 
Wakulu walioko jirani na hii habari mtujuze ili wanaharakati tuingie kazini.
 
Bw. Lipumba nasikia ameamua kufunga safari, kujionea tukio. Mr jinius sijui yuko wapi angeweza kutujuza zaidi
 
Ipo siriaz ki hivyo. thats blasting.
Jeshi wameshaanza sasa.....
 
Mkuu Imma. hebu tupe more hints here.
inawezekanaje askari kuua watu 25 kwa kuwahukumu kuwa ni majangili/ majambazi? wapi kwenye sheria duniani seuse tanzania inatoa ruhusa hiyo?
Nataka undani wa hili maana ni ajabu na kweli tena ktk kipindi hiki ambacho jeshi limeshaanza kukenua meno na kukunja ndita dhidi ya watu.
 
Nadhani hii inahitajika kuwa handled kikamilifu na kiangalifu isije ikaleta vurgu na kuvuruga amani... hata kama kuna upinzani, nadhani sisi wote ni wamoja na hakuna haja ya kuuana au kuchochea mauaji
 
sasa tunaelekea kubaya.

hata kama hatutaweka hisia za kisiasa, askari hawana mamlaka ya kuchoma moto nyumba za wananchi sembuse kuwauwa!

Linapaswa kupigiwa kelele na watu wa kada zote hili
 
Bw. Lipumba nasikia ameamua kufunga safari, kujionea tukio. Mr jinius sijui yuko wapi angeweza kutujuza zaidi

Taarifa za uhakika ni kwamba Prof.Juma kapuya anapumulia mashine.Afya yake kisiasa ni mbaya sana CUF wamemshika pabaya haponi inavyosemekana
 
duuh.....tupeni detail zakutosha mana watanzania wenzetu wameuwawa isivyo stahili.
 
Habari nadani ya habari. Bado tunasema kuwa DAMU HAZIMWAGIKI TU! Hapo nako tutasingizia CHADEMA?
 
siamini kama hii ni kweli. siamini kama sisiemu ingefanya kosa kubwa kama hili wakati wa uchaguzi kama huu..hiyo ni negligence ya hali ya juu kwenye selikali yao, na kama ni kweli, itawasumbua sana kwasababu watalipa garama kuanzia kitaifa hadi kimataifa. mashirika ya kimataifa yatahitaji kujua kulikoni, wapiga kura tunahitaji kujua pia kulikoni...wanyama ni bora kuliko binadamu? tuwajengee nyumba basi hao wanyama ili waishi na watz tuhamie nchi zingine.
 
Hii habari inaonekana kuna ukweli ndani yake, leo asubuh TBC taifa walimuhoji Prof. Lipumba akaelezea liyoyaelezea, na baadae Gabriel Zakaria (mtangazaji) akmuhoji mkuu wa mkoa wa Tabora Abeid Mnyimusa kuhusiana na ukweli wa habari hizo. Mkuu wa mkoa akazungumzia point km 3 hivi. 1: Anadaia ni wavamizi ktk hifadhi, 2: waliouwawa ni wahalifu waliojificha huko si wapinzani kwani wanafanya uhalifu kwingineko na wanaenda kujificha huko porini. 3: Hakuna nyumba iliyochomwa moto, ila vibanda vya hao wavamizi ndio vilivyochomwa moto.
Mwandishi alipomuuliza km waliouwawa ni wapinzani kuna ukweli upi hapo? akang'ang'ania kusema ni wahalifu waliojificha ndani ya hifadhi.

Wito alioutoa prof. lipumba wa kutaka uchunguzi huru ufanyike una nafasi kubwa zaidi km ni kweli tunastahili kuitwa nchi ya demokrasia na yenye utawala bora wa sheria.
Mhalifu hauwawi anakamatwa na kupelekwa mahakamani, na mahakama ndio itathibitisha uhalifu wake na hukumu yake anayostahili kulingana na makosa aliyofanya.

Asasi huru za kisheria nchini na za kimataifa ziende eneo la tukio zifanye uchunguzi wao na kutupatia matokeo halisi yasiyochakachuliwa!!!
 
Not withstanding!!!................ Kwa nini vibanda vya waarifu vichomwe moto?? Suala ni kuwashika waarifu; kwa nini vibanda vichomwe moto?? Polisi au Jeshi wameamuru hvyo vibanda vichomwe moto??....waarifu'walikuwa na silaha za moto''''''Banana country!!!!! We are not different from SUDAN and Somalia; are we??
 
Back
Top Bottom