Zanzibar 2020 Urais Zanzibar: Kwanini nawapa chapuo Makame na Mwinyi

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,744
21,194
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Makame Mbarawa amechukua fomu za kuwania kuteuliwa kuwania nafasi ya urais kupitia chama cha mapinduzi uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu mwezi wa kumi (Oktoba).

20200619_182914.png

PICHA: Prof. Makame Mbarawa kushoto na Dr. Hussein Mwinyi kulia.

Profesa Mbarawa anakuwa ni mwanachama wa 11 kati ya wanachama waliojitokeza upande wa Zanzibar waliojitokeza kusubili vikao vya juu vya chama kuteua jina moja litakalopeperusha bendera ya chama kwa upande wa Zanzibar.

Kabla ya Mbarawa waziri mwingine kutoka serikali ya muungano ni Hussein Mwinyi ambaye alichukua fomu siku mbili zilizopita ikiwa ni siku moja ambayo mwenyekiti wa ccm ambaye ni mgombea kwa upande wa bara Dr. John Magufuri alikwenda kuchukua fomubpale jijini dodoma.

↘Kufuatia msururu mrefu wa wanaowania nafasi hiyo, nashare na wewe kuhusu wagombea hawa wawili Makame na Hussein ambao kwa muktadha unaoonekana waziwazi hawa wawili ndiyo watakaoingia kwenye mchuano mkali sana kumpata mmoja atakayechuana vikali na mgombea kutoka upinzani.

Hussein anapewa chepuo kutokana na nafasi aliyo nayo toka baba yake alipoondoka madarani, amekuwa ni waziri asiye na papara na kujinasibu sana kama wengine wanavyoonekana, hali hiyo imekuwa kama fulsa flani ya ndani kwa ndani kuweza kumuandaa ili aje kutwaa nafasi hiyo.

Ukija kwa prof. Makame huyu kila mtu anafahamu kutokana na kuwa karibu na Rais JPM na kutokana na utendaji wake, ukaribu na presida hiyo ndiyo inanipa hoja ya kupewa nafasi, hiyo inatokana na presida kutaka kuweka mtu anayemfaham vizuri huku ikiwepo nafasi ya kumtumia kutokana na kumfaham akiwa mtu wake wa karibu ambaye anaweza kumpa maelezo na nini afanye akiwa pale.

Kutokana na hayo uchaguzi ujao ni kati ya hao wawili hawavumi sana lakini ndiyo wenye nguvu tofauti na wengine ninaowaona kama wasindikizaji.
 
Hussein Mwinyi akipitishwa kugombea Zanzibar mjue Mzee Baba atabadili katiba aendelee bila ukomo.
 
Mwinyi hapo anatoboa. Zanzibar wana upemba na uunguja.Rais anaemaliza muda wake ni mpemba.
 
Makame hata ubunge wa kuchanguliwa kachindwa kuupata!!

Hakuna viongozi hapo.
 
Mkuu nimeelewa andiko lako ila yote kwa yote mwinyi ni President material ukiachana na hata huku bara anafaa sana mda ukifika, huo ni mtazamo wangu kwa muonekano wake ila sijui ya moyoni mwake maana madaraka watu wakisha pata hubadika sana, na kusahau wametokea wapi hata kuwasahau walio nyuma yao hasa wananchi.
 
Prof Makame atawafaa zaidi,Mwinyi yupoyupo tu bora hata ya Shein. Na isingekuwa huo ubin hakuna mtu angempigia hata chapuo kama sasa!
 
Safari hii uchaguzi wa Zanzibar umekuwa hot kuliko ule wa Tanganyoka?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom