Tayana-wog
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 23,144
- 26,646
Pasco umegonga pwenti, endapo ZZK anakusoma bila shaka atalazimika kutazama upya strategies zake ili aziboreshe zaidi.
Sijawahi kuona tatizo la Mtanzania yeyote kuwa na nia ya kugombea uraisi wa nchi yetu almuradi ataweza kuongoza na kushirikisha wananchi kukabiliana na changamoto mingi zinazokwaza Watanzania. Ukiachilia mbali CCM ambayo imekaa madarakani miaka 50 ambayo haijatosha kuwanasua watanzania kwenye lindi la umasikini zaidi ya kuwajengea utengano na matabaka kwa misingi ya kisiasa na kidini hususani miaka 6 iliyopita, wagombea uraisi kupitia upinzani hawajafanya jitihada za kutosha kuwaelimisha wapiga kura kuhusu haki zao za uraia. CHADEMA ndio pekee wanaojitahidi kusambaza elimu hii kwa sasa. Kule ZNZ chama cha wananchi kilifanya kazi hii vema na kinastahili pongezi kwa hilo. Hivyo basi, ZZK kama kweli ana dhati ya kuwa raisi wa Tanzania hana budi kusikiiza sauti ya Pasco ili arekebishe "strategies" zake. Vinginevyo ngoma LAZIMA IPASUKE pwaaaaaaaaaaaaaaaaa!
na imepasuka pwaaaaaaaa