Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!.

Mkandara umenena! Kwa hali hiyo c haba kuamini kabisa ZZK lengo lake hasa ni kuharibu tu chama na kuandaa mparaganyiko flani
 
Mtei na wazee wengine ni very smart hawakuingiza mtu ni mtu tuu just because kaweza leta ubishi wa uswazi na kuwashinda wengine.Zitto anthibitihsa hilo kwa vitendo kuwa bado hajastaarabika vya kutosha kuwa kiongozi wa kitaifa pamoja na exposure aliyopata.

Mtei anataka mkaskazini mwenzake.teh teh teh
 
Ebu msomeni kijana mwenzake January Makamba jinsi alinavyokomaa kisiasa.. Hata kama anautaka Urais lakini he knows how to play the game..source Bofya

Kama nilivyowaambia Jumamosi nilikuwa na Mhe January Makamba ambapo pamoja na kuelezea maisha yake ya kawaida ya kisiasa pia alijibu maswali yenu. Moja ya vitu alivyosema ni kuwa hana mpango wa kugombea Urais.
Alisema
anaamini nafasi ya urais inahitaji mtu ambaye amejiandaa Kisaikolojia, Kisiasa na Kifikra na kumalizia kwa kusema kuwa Urais sio uamuzi wa mtu mmoja kwa sababu nchi haiendeshwi na mtu mmoja na inahitaji watu ambao wanashauriana, kuandaa dira ya pamoja na kupeleka ujumbe wa kuwaunganisha Watanzania.

Alipoulizwa Rais anayekuja anatakiwa aweje alisema anatakiwa awe ni mtu atakae waunganisha Watanzania huku akisema mianya ya ukabila, udini na rushwa ambayo baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliitaja imeanza kuonekana.

Pia Makamba alisema rais ajaye anatakiwa asiwe mtu mwenye hulka ya visasi na atakiwa awe na uwezo wa kuwaambia wananchi kuwa yeye sio masihi wakuyafanya maisha yao yabadilike papo kwa hapo kwa kuwa nchi ni ya watu wote, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kutumia nafasi yake kuleta mabadiliko.
 
Mtei anataka mkaskazini mwenzake.teh teh teh

hujajua unachoambiwa.Kwa ujumla ukibeba watu waliosoma ila hawakuelimika,unapochukua watu wasio na roho za kazi bila kudai marejesho mapema si rahisi kufika mbali.Mtei ni mmoja tuu katik waanzilishi,na akikataliwa Zitto akina Bob Makani walikuwa hai.Hata katika biashara vijana wengi wameshindwa anzisha biashara na kufanikiwa kwa vile vijana wengi hawataki sacrifice na mara wapatapo deal ya kwanza kubwa basi fujo huanza.Huanza gombea mgao bila hata kuangalia kiasi gani kinahitajika kuweka biashara ktk mazingira bora ya kiushindani na uwezo wa kustahimili mabadiliko ya soko.

Zitto ni mmojawapo ya aina ya vijana tunaowakosa katk ujasiriamali wa vikundi.kaona kuna harufu ya kuchukua nchi basi anataka yeye ndie awe ama chama kikose.Ni kutostaarabika.Ndio hapo waanzilishi na wajumbe wengine walipoamua kutochukua hiyo risk wakawaweka akina mbowe na dr .Slaa. Sasa haya yanaonekana.
 
Hivi Tanzania kuna ethics!? tangu lini!? hizo ethics ziko katika nyanja zipi? Kama tungekuwa na ethics madudu mbali mbali yanayotokea tungekuwa tunayasikia nchi nyingine tu na si kwetu. Mifano hai ni wale TBC1 na utangazaji wao, magazeti ya uhuru, mzalendo, daily noise jinsi yalivyo biased katika kufukia madhambi ya Serikali ya magamba na kutaka kuinonyesha kama ni Serikali iliyotukuka.

Ila nakubaliana nawe jinsi ulichanganua kuhusu ngoma ikivuma sana....!
Mkuu BAK, kuhusu uwepo wa ethics, hizo zipo tena kwenye maandishi!, lakini issue ya jee hizo ethics zinafuatwa?, hapa ndipo tatizo lilipo!. TBC na Magazeti ya Daily News, vinajulikana kama "vyombo vya habari vya serikali" "government media!", kiukweli, hivi sio vyombo vya habari vya serikali, hizi ni "public media", yaani vyombo vya habari vya umma!.

Hivyo TBC ni "public broadcasting station" na sio "government broadcasting station" hivyo inapaswa kufuata ethics za "public broadcasting stations" ndio maana uchaguzi wa 2010, hamkuona kipindi chochote cha chama chochote!. Hata vile vipindi vya "Salva", kwa mwamvuli wa "Kurugenzi ya Mawasiano Ikulu" ambavyo Ahmed Kipozi (ameshapewa asante yake) alivitangaza, Tido, alivigomea!, baada ya ya uchaguzi, Tido naye alipatiwa ujira wake stahiki kwa kusimamia "ethics"!.

TBC ina behave kama "government broadcasting station" kwa sababu hakuna "watu" wa kuinyooshea kidole na kuilazimisha TBC, itimize wajibu wake!. Japo mimi sio mwana Chadema, na Chadema sii lolote sii chochote kwenye kupigania maslahi ya taifa kwa vitendo, hivyo kwenye hili, akina sisi ambao hatuna vyama, tutajikuta kama tunaisaidia Chadema, kwa njia moja au nyingine!.

Gazeti la Uhuru, lenyewe ni gazeti la CCM kama ilivyo radio uhuru, hivyo ni haki yao na halali yao kuegemea upande wao wenye maslahi nao!. Chadema haikatazwi kuwa na redio yake!, gharama ya kuanzisha kituo cha redia cha kisasa kabisa, ni robo tuu ya gharama ya kununua yale magari ya M4C. Kupanga ni kuchagua, priority ya Chadema sio kumiliki vyomvo vyake vya habari, bali kununua PA ya nguvu na kuwafikia wananchi mamia kwa ma elfu kwa urahisi huki ikiwahamasishe waandamane, wakati kumbe wangekuwa na redio yao, na tv yao, wangewafikia mamilioni na sio kuhamasisha maandamano, bali kutangaza sera mbadala dhidi ya hizi za CCM zilizofeli!.
 
Wengi sisi tumekuzwa na difficult realities. Huyu dogo naye atajifunza tu mwenyewe as he grows up. Sasa hivi haoni wala haskii.
Mkuu Facilitator, hili la kutoona, wala kusikia, ni moja ya matatizo ya ndani kabisa ya ZZK, hii inaitwa "ego"!, kwa vile ZZK ni mtoto "born and breed" Chadema, anapoota pembe na kujiona sasa yeye ni mkubwa, ame i over grow Chadema, hivyo haoni, wala hasikii!, kama bado anahitajika nyumbani, then hufunza adabu kwa hizo pembe kukatwa, hivyo kuonyeshwa na kusikilizishwa kwa nguvu kwa mtindo wa "spare the rod and spoil the kid"!, au kama ni kweli amekuwa mkubwa, huachwa ku fall out na kuji detach na base hivyo kuanza kujitegemea!.
 
Hivi wana forum, mnafikiri ZZK ni mjinga? Mnafikiri hajui anachofanya?

Swali linalotakiwa kuulizwa na kupatiwa jibu ni WHY is he doing that?

Kwanini?
 
Hakuna faida yoyote ya kuwa na ethics kwenye maandishi ambapo hakuna yeyote yule anayezifuata na hivyo utekelezaji wako ni sifuri. Kwa maoni yangu sheria inayohusiana na vyombo vya habari nchini inahitaji marekebisho makubwa sana ili vyombo hivyo visitumiwe katika kuficha maovu mbali mbali yanayofanywa na Serikali husika eti ni kwa sababu tu ni gazeti/TV la/ya Serikali.

Ikumbukwe Serikali iliyopo madarakani ni Serikali ya Watanzania wote bila kujali itikadi zetu hivyo gazeti/TV station la Serikali ambalo/ambayo linalotumia/inayotumia kodi za walipa kodi ili kujiendesha, kuendelea kutumika kwa kueneza propaganda ambazo mara nyingi zinakuwa si kweli ni kukiuka maadili ya uandishi/utangazaji wa habari.

Sasa hivi tuna vyombo vya habari vingi tu nchini wakati umefika Serikali kuyaachia magazeti na TV za Serikali ili vyombo hivi viwe huru katika kufanya kazi zao kama waandishi au watangazaji bila woga wa kuingiliwa na Serikali.

Mkuu BAK, kuhusu uwepo wa ethics, hizo zipo tena kwenye maandishi!, lakini issue ya jee hizo ethics zinafuatwa?, hapa ndipo tatizo lilipo!. TBC na Magazeti ya Daily News, vinajulikana kama "vyombo vya habari vya serikali" "government media!", kiukweli, hivi sio vyombo vya habari vya serikali, hizi ni "public media", yaani vyombo vya habari vya umma!.

Hivyo TBC ni "public broadcasting station" na sio "government broadcasting station" hivyo inapaswa kufuata ethics za "public broadcasting stations" ndio maana uchaguzi wa 2010, hamkuona kipindi chochote cha chama chochote!. Hata vile vipindi vya "Salva", kwa mwamvuli wa "Kurugenzi ya Mawasiano Ikulu" ambavyo Ahmed Kipozi (ameshapewa asante yake) alivitangaza, Tido, alivigomea!, baada ya ya uchaguzi, Tido naye alipatiwa ujira wake stahiki kwa kusimamia "ethics"!.

TBC ina behave kama "government broadcasting station" kwa sababu hakuna "watu" wa kuinyooshea kidole na kuilazimisha TBC, itimize wajibu wake!. Japo mimi sio mwana Chadema, na Chadema sii lolote sii chochote kwenye kupigania maslahi ya taifa kwa vitendo, hivyo kwenye hili, akina sisi ambao hatuna vyama, tutajikuta kama tunaisaidia Chadema, kwa njia moja au nyingine!.

Gazeti la Uhuru, lenyewe ni gazeti la CCM kama ilivyo radio uhuru, hivyo ni haki yao na halali yao kuegemea upande wao wenye maslahi nao!.
 
Zitto pamoja daima, pamoko hadi kieleweke unajenga hoja, unasoma, una uwezo wa kuwa rais
 
Hakuna faida yoyote ya kuwa na ethics kwenye maandishi ambapo hakuna yeyote yule anayezifuata na hivyo utekelezaji wako ni sifuri. Kwa maoni yangu sheria inayohusiana na vyombo vya habari nchini inahitaji marekebisho makubwa sana ili vyombo hivyo visitumiwe katika kuficha maovu mbali mbali yanayofanywa na Serikali husika eti ni kwa sababu tu ni gazeti/TV la/ya Serikali.

Ikumbukwe Serikali iliyopo madarakani ni Serikali ya Watanzania wote bila kujali itikadi zetu hivyo gazeti/TV station la Serikali ambalo/ambayo linalotumia/inayotumia kodi za walipa kodi ili kujiendesha, kuendelea kutumika kwa kueneza propaganda ambazo mara nyingi zinakuwa si kweli ni kukiuka maadili ya uandishi/utangazaji wa habari.

Sasa hivi tuna vyombo vya habari vingi tu nchini wakati umefika Serikali kuyaachia magazeti na TV za Serikali ili vyombo hivi viwe huru katika kufanya kazi zao kama waandishi au watangazaji bila woga wa kuingiliwa na Serikali.

Kama nje ya mada vile......?
 
Nianze kwa nukuu kutoka sehemu ya maandishi ya Pasco na Mkandara
"The proper way ilikuwa sio yeye kutangaza nia bali kuwaonyesha Chadema kwa vitendo kuwa anaweza na ni kwa kupitia vitendo hivyo vya kuonyesha uwezo, ndipo Chadema waonyeshe kuwa wanamhitaji ZZK kupeperusha bendera yake 2015, not the other way round!.(Pasco)"

"Kama anataka kugombea Urais anatakiwa kujipanga nyumbani kwake kwanza….CDM (Mkandara)"

Wana-JF niliyowataja hapo juu mawaidha yao nayakubali, na wana kitu kimoja kinachofanana……ZZT ajiimalishe ndani ya CDM kwanza. Nakubaliana nao sana hasa kwa kipindi hiki ambapo CDM inaelekea kujijenga kwenye mizizi ya CCM (mikoani), chini ya M4C unaitajika mchikamano wa dhati wana-CDM wote. Viongozi wa CDM wanapopanda majukwaani kuutubia, wananchi wanajua pasipo na shaka makamanda wapo kujenga chama, lakini inapotokea mmoja wao tayari ana ajenda yake ya uraisi mfukoni; moja-wananchi wengine watahisi ZZT yupo kwenye kampeni ya kujijenga binafsi kwa wananchi ili kuwa rais, so M4C itaanza kupoteza maana.

Hii itakua advantage wa CCM na ninaamini watatumia udhahifu huu kuimaliza M4C kwa kuipa sura ya kampeni ya urais. Pili ZZT harakati zake kwa sasa zitamfanya hakose kuaminika kwa makamanda wenzake chini ya harakati za M4C, wakiwa naye watakuwa hawajui mwenzetu tupo nae kwa kuimarisha chama or yupo kwa kampeni binafsi za urais?. Kwenye vita makamanda wasipoaminiana hakuna ushindi. Nimeizungumzia sana M4C kwa sababu nahisi ndio itakua mwathirika wa kwanza wa harakatazi za urais wa ZZT kwa sasa sababu nilizozitaja hapo juu. Nieleweke simpingi ZZT kugombea urais, ila kauli yake hajaitoa wakati muafaka….kama manabii walivyopata kunena"kwa kila jambo kuna majira yake, (Muhubiri 3:1)". Basi nami nasema majira ya sasa ni ya kuimarisha na kuisambaza CDM mikoani, majira ya urais bado.Harakati zake za sasa zinaisaidia CCM na sio CDM.
 
Ebu msomeni kijana mwenzake January Makamba jinsi alinavyokomaa kisiasa.. Hata kama anautaka Urais lakini he knows how to play the game..source Bofya

Kama nilivyowaambia Jumamosi nilikuwa na Mhe January Makamba ambapo pamoja na kuelezea maisha yake ya kawaida ya kisiasa pia alijibu maswali yenu. Moja ya vitu alivyosema ni kuwa hana mpango wa kugombea Urais.
Alisema
anaamini nafasi ya urais inahitaji mtu ambaye amejiandaa Kisaikolojia, Kisiasa na Kifikra na kumalizia kwa kusema kuwa Urais sio uamuzi wa mtu mmoja kwa sababu nchi haiendeshwi na mtu mmoja na inahitaji watu ambao wanashauriana, kuandaa dira ya pamoja na kupeleka ujumbe wa kuwaunganisha Watanzania.

Alipoulizwa Rais anayekuja anatakiwa aweje alisema anatakiwa awe ni mtu atakae waunganisha Watanzania huku akisema mianya ya ukabila, udini na rushwa ambayo baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliitaja imeanza kuonekana.

Pia Makamba alisema rais ajaye anatakiwa asiwe mtu mwenye hulka ya visasi na atakiwa awe na uwezo wa kuwaambia wananchi kuwa yeye sio masihi wakuyafanya maisha yao yabadilike papo kwa hapo kwa kuwa nchi ni ya watu wote, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kutumia nafasi yake kuleta mabadiliko.
Mkuu Mkandara, asante sana kwa hii link.
 
...
ZZK: Namkubali sana tuu ila natatizwa na determination yake ya kuwa a
ZZK alipofanya atempt ya kumvaa Mbowe kwenye Uenyekiti wa Chadema, alikurupuka bila kutoa sababu, na alipojitoa hakutoa sababu za kujitoa!
Kwa vile mpiga ngoma hii mkubwa ni ZZK mwenyewe na ikitokea ngoma hii kupasuka kiukweli, then itakuwa ni haki tukisema aliyeipasua ngoma ya ZZK kwenye urais wa 2015 ni ZZK mwenyewe hivyo wapenzi wa ZZK ngoma ikishapusuka, nawaombeni sana msitafute mchawi!.
Pasco.
Hapo. Pasco nakukubali maana leo 2012 hadi 2015 ni mbali kuanza kuwashawishi WaTZ km ya Lowasa.either itatokea km alivyosema Mkandara au yaje ya Walid Kabour kwa wana Kigoma wenzie
Suala si ushabiki ni je? Wazee na Wanachama wamekupitisha uwawakilishe Pasco kumbuka ZZK uenyekiti hakulala mbele ila vigezo bba ridhaa ya Chama chake haikuwepo
Hivyo Urais kwa yeyote ni ridhaa ya wenye Chama
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu wanakubali kujipeleka kama treni ndani ya taluma zake......au robot in the assembly plant.
 
maadamu mwenyewe umejitambulisha kuwa ni masikini basi nakuhakikishia Zitto hafai kuwa Rais wako, yeye alishajitoa kwenye umasikini siku nyingi. Ni fisadi mzuri tu japo mara kadhaa amefanikiwa kuwahadaa watz wasioshughulisha bongo zao kuwa eti ni mpinga ufisadi. Ana mali kuliko umri wake!
ZZK kuwa na mali kuliko umri wake sio tija, ameshitakiwa wapi kwamba amekwiba? Kuna eneo unaloweza kuthibitisha kuwa mali alizonazo ameziiba au kudhulumu sehemu, au ni wapi kaingia mkenge wa kusaini mikataba hewa? msimuonee kijana utajiri sio kipingamizi cha mtu kuwania kugombea urais. hao unaodhani ni wasafi sio chochote.
 
Tofautisheni kati ya KAMBI na USHABIKI.

Sasa mtu hajulikani hata na wilaya 2 alafu naye anajiita yupo kambi ya Zitto ama slaa.

Huu ni ujinga kweli.
 
Labda tu nichomekee kidogo ingawaje iko nje ya mada hapo Bw. Jakaya Kikwete unamweka wapi ktk hizo sifa za kiongozi?

Ngoja nimsaidie Mgaya, au na mimi nichomekee kidogo. Kikwete is a historic mistake. Hafai na hakufaa kabisa kuwa rais wa Tanzania. Tusirudie tena kosa hilo.
 
kwa mfano wapi amepwaya?. zitto ni rais wangu na masikini wenzangu

RED: Hapo sawa na hongera zako

BLUE: Hapana mie masikini lakini ZZK hawezi na hatakuwa Rais wangu 2015, sijakutuma unisemee wala sie masikini hatujakutuma uwe msemaji wetu
 
Back
Top Bottom