Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!.

maadamu mwenyewe umejitambulisha kuwa ni masikini basi nakuhakikishia Zitto hafai kuwa Rais wako, yeye alishajitoa kwenye umasikini siku nyingi. Ni fisadi mzuri tu japo mara kadhaa amefanikiwa kuwahadaa watz wasioshughulisha bongo zao kuwa eti ni mpinga ufisadi. Ana mali kuliko umri wake!
vipi slaa na mbowe ambao wewe unawaabudu ni masikini? vipi slaa kushinikiza chama kimlipe shahara na marupurupu mengine kama kusacrifies ubunge kwenda kugombea urais. wewe unafikiri hatujui? think twice.
 
Tuache demokrasia ichukuwe mkondo wake! Kama CHADEMA itampitisha sawa!
 
Pasco umegonga pwenti, endapo ZZK anakusoma bila shaka atalazimika kutazama upya strategies zake ili aziboreshe zaidi.
Sijawahi kuona tatizo la Mtanzania yeyote kuwa na nia ya kugombea uraisi wa nchi yetu almuradi ataweza kuongoza na kushirikisha wananchi kukabiliana na changamoto mingi zinazokwaza Watanzania. Ukiachilia mbali CCM ambayo imekaa madarakani miaka 50 ambayo haijatosha kuwanasua watanzania kwenye lindi la umasikini zaidi ya kuwajengea utengano na matabaka kwa misingi ya kisiasa na kidini hususani miaka 6 iliyopita, wagombea uraisi kupitia upinzani hawajafanya jitihada za kutosha kuwaelimisha wapiga kura kuhusu haki zao za uraia. CHADEMA ndio pekee wanaojitahidi kusambaza elimu hii kwa sasa. Kule ZNZ chama cha wananchi kilifanya kazi hii vema na kinastahili pongezi kwa hilo. Hivyo basi, ZZK kama kweli ana dhati ya kuwa raisi wa Tanzania hana budi kusikiiza sauti ya Pasco ili arekebishe "strategies" zake. Vinginevyo ngoma LAZIMA IPASUKE pwaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Kwenye siasa usingoje sana kusifiwa kwa sababu kawaida ya siasa mambo hayatokei bila kupangwa. ZZK anapiga ngoma yake live, wengine wamerekodi ngoma kwenye CD na kuzipiga kwa redio - hakuna anayesifiwa tu bila mkakati...
 
ZZK anacheza michezo ya hatari yenye madhara makubwa kwake kisisasa

kwanza akitaka support ya wananchi na chama chake inabidi aongoze mapambano katika kupatikana katiba mpya ambayo itamwezesha kugombea uraisi akiwa na miaka 39 mwaka 20015

pili tatizo kubwa tulilonalo ni la mifumo wa utawala yaani (katiba). kwa mtu mzalendo kama yeye alivyowahi kujiita ni busara zaidi kupigania katiba nzuri zaidi ya kupigania madaraka ya uraisi, kwani ukisha kuwa na katiba mzuri, mtu yeyote toka chama chochote anaweza kuwa Rais. na malengo au mikakati binafsi ya ZITO au mtu yeyote,ya kuwalete wananchi maendeleo itashinikizwa kupitia nafasi za uwakilishi au ushari kwa wahusika

CDM wanapigania katiba bora si madaraka nadhani CDM wawe radhi waukose urais 2015 lakini wapiganie katiba nzuri ili tuwatofautishe na CCM. kama CDM watazingatia hili watafanikiwa huko mbeleni, watu wenye malengo mazuri na nchi yetu wanapigania mfumo mzuri wa utawala siyo madaraka

nawashauri CDM wapiganie upatikanaji wa katiba bora na nzuri hata kama 2015 hawatatoa raisi wa nchi haitakuwa mwisho wa harakati za kisiasa ila watakuja kuchukua madraka kiraisi huko mbeleni. na watayaenjoy hayo madaraka kuliko hii tamaa inayojionyesha miongoni mwa wanachama wake mfano ZZK
 
Mimi ninafikiri ZZK ana mkataba na wasanii wa filamu za bongo kuandaa mazingira ya kutengeneza filamu ijayo: "ZZK for President - 2015".
 
Kwa hiyo tuseme wewe ambae ni supporter wake mkubwa
'humuelewi na unaona hataweza na anajiumiza mwenyewe'?
this is more than funny....
Utamu wa ngoma, ni kupigiwa na kuingia kucheza, sio mgoma upige wewe na kucheza ucheze wewe!. Hivi umeishamsikia EL au Membe akijipigia debe la urais 2015?, wao wanafanya mambo, huku wapiga ngoma, wakipiga kuwasubiri waingiaji wacheze!
 
kwa mfano wapi amepwaya?. zitto ni rais wangu na masikini wenzangu

ZItto si maskini wa hela .Ni wa fikra, sasa kam ana wewe ni mwenzake you are gone.Ubaguzi wa kijinga wa watu wa kigoma utawapeleka pabaya sana.Mnaanza watisha watengeneza hela from nothing mapema hivi mjue itakula kwenu.Waganda waliwakimbiza wahindi leo, wahindi walipokwna wlaifanikiwa ila waganda hawajakwenda popote.
 
Utamu wa ngoma, ni kupigiwa na kuingia kucheza, sio mgoma upige wewe na kucheza ucheze wewe!. Hivi umeishamsikia EL au Membe akijipigia debe la urais 2015?, wao wanafanya mambo, huku wapiga ngoma, wakipiga kuwasubiri waingiaji wacheze!

This is what Zitto should learn. Hakuna hata mwana ccm mmoja aliyetangaza nia yake kutaka hiyo top job. Hii strategy yake ni tata sana. Ila anasumbuliwa tu na ujana
 
ZZT anajichimbia mwenyewe kaburi lake kisiasa.

back ground ya Zitto ni kama ya Nyalandu.Inawarudia na kuwavuta chini....udhaifu wao kikabila na kidini ndio unawafanya washindwe fanikiwa kuona na kukubali kuwa watu wa makundi tofauti na yao(ama kidini, ama kibala, ama kikanda) walifanya hivyo bila kuwa na mpango maalumu ila kama indvividual struggle na kuwafikisha hapo wanapoonekana kama kundi.

Kutokuona haya kunamfanya huyu jamaa anunue distorted views na excuse za loosers wa upande wao.Mfano.Kuna mikoa mingi ana watu wake hawakupenda rudi iendeleza kwa hofu za uchawi, na kuvunja miiko ya imani zao.Leo hii wapo watu hawapo tayari kumeza huu ukweli na kuwaambia watu wao kuwa wao ndio tatizo na si ubaguzi wanolalamikia na kuufanya dhidi ya wengine.
 
Nadhani nia ya ZZK ni kuwa mgombea binafsi ( hii inakuja kwenye katiba mpya). Hapa anataka ku split kura za CDM ili ccm iwe na kazi nyepesi kuvuka.
Anajua CDM hajatosha kupewa mkoba huo wa kugombania uraisi.........
Whats pushing him.???????????
 
Nadhani nia ya ZZK ni kuwa mgombea binafsi ( hii inakuja kwenye katiba mpya). Hapa anataka ku split kura za CDM ili ccm iwe na kazi nyepesi kuvuka.
Anajua CDM hajatosha kupewa mkoba huo wa kugombania uraisi.........
Whats pushing him.???????????

Masikini na mdini akipewa nafasi ya upendeleo kwa udini na ukabila hugeuza yote kuwa kinyume.Hajui anathibitisha kwa wenye akili kuwa tatizo ni wao wenyewe na si ubaguzi.
 
Pasco nilikuwa nafikiri idea imetoka kwako manake wewe ni mmojawapo wa washauri wa karibu wa zzk'hivi mmegundua madhaifu ya watanzania yanayosemwa sana??hili ni mojawapo'kwa level aliyofikia zzk politicaly hakutakiwa atoke vile'' pasco amejaribu kuonyesha njia ambazo angetumia but is too late kwa sababu maji yameshamwagika'sisi wanachama wa kawaida tunaona kama zzk anatumiwa kutuharibia chama chetu'zk jiandae kaka unavutiwa pumzi december mbali sana
 
Tukana matusi kama ulivyozoea kumtukana Mbowe na Dr Slaa kule Facebook ukishirikiana na Habib Mchange na Juliana Shonza.

mkuu hawa ni watoto wadogo sana wanajifunza siasa, pia tusiwalahumu sana kwani ni watu ambao hawana cha kupoteza ndani ya chama na ni WASHIBIKI tu kama washabiki wa yanga au simba na kikubwa wanashindwa kutofautisha USHABIKI na KAMBI.

HIVI MTU HATA HUJULIKANI ALAFU NA WEWE UNAJIITA UNA KAMBI? aibu gani hii juu ya hawa watoto sample ya chagulani.
 
Back
Top Bottom