Urais wa Muungano 2015 ni zamu ya Zanzibar - Maalim Seif

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema si haki hata kidogo Rais wa muungano atoke upande wa bara tu kila awamu.Maalim Seif amesema kamwe haikubaliki kwani ni nchi mbili huru ziliungana.Ameongeza huu ni upendeleo wa waziwazi ambao katiba mpya itabidi iufanyie kazi kwa maslahi ya nchi hizi mbili. SOURCE HABARI ITV.

Makamu wa Kwanza wa rais wa zanzibar. Hivi katiba tuliyonayo sasa inakitambua cheo hicho. Kabla ya kuoba uraisia aombe cheo chake kitambuliwe rasmi na JMT
 
kha! Sasa sefu anautaka urais wa muungano. List inaongezeka.
1. Lowassa.
2. Mkapa
3. sumaye
4. sitta
5. Membe
7. Migiro
8. Sefu
 
Kumbe huwa kuna zamu hata kwenye maamuzi yanayotegemea kura?!
tungoje tuone! Sasa wamekuja kwa gia ya kututamkia zanzibar na bara! next time watakuja na jina la mtu kabisa..! ndo mambo ya zamu yalivyo!
 
Kweli ninyi vilaza! Nashangaa munachangia thread ambayo imeandikwa na utashi wa mtu binafsi, mada ata haijakidhi vigezo na masharti ikiwekwa tu munaanza kuweka comments, kwa mimi ambaye nilikuwepo ndani kabisa ambamo Maalim aliongea na Waandishi wa Habari nimeshangaa kuona huu uchafu hapa ndani ambao unasema umetolewa na na Maalim!!! Tafteni ukweli wa maneno kwanza ndo muanze kuchangia nachelea musijekuonekana viziwi munacheza ngoma kwa furaha kumbe masikini hata mdundo hamuujui unapigwaje!
Mkuu mpemba mbishi
Umeona hii mada haikidhi vigezo,pia umeona ni "uchafu".
Wewe uliyesikia first hand ni vyema kuuhabarisha ukumbi kile kilichosemwa kwa waandishi wa habari.

Tunatega sikio, ukumbi ni wako!
 
Kweli ninyi vilaza! Nashangaa munachangia thread ambayo imeandikwa na utashi wa mtu binafsi, mada ata haijakidhi vigezo na masharti ikiwekwa tu munaanza kuweka comments, kwa mimi ambaye nilikuwepo ndani kabisa ambamo Maalim aliongea na Waandishi wa Habari nimeshangaa kuona huu uchafu hapa ndani ambao unasema umetolewa na na Maalim!!! Tafteni ukweli wa maneno kwanza ndo muanze kuchangia nachelea musijekuonekana viziwi munacheza ngoma kwa furaha kumbe masikini hata mdundo hamuujui unapigwaje!

aliyekuwa anaongea itv ni wewe? Usidhani watu wote ni wavivu wa kufikiri kama wewe.Mpemba usiye na haya
 
Mkuu mpemba mbishi
Umeona hii mada haikidhi vigezo,pia umeona ni "uchafu".
Wewe uliyesikia first hand ni vyema kuuhabarisha ukumbi kile kilichosemwa kwa waandishi wa habari.

Tunatega sikio, ukumbi ni wako!

mwambie ni ndoto mpemba kumtawala tena mtanganyika
 
HUYU NAE ANAZEEKA VIBAYA SASA HV NI MFUMO WA VYAMA VINGI SASA KAMA VYAMA VINATUWEKEA WAGOMBEA WAZANZIBAR NA WABARA NI JUKUMU LA WATZ KUMCHAGUA WATAKAEONA ANAWAFAA SASA UZNZ NA UBARA WATOKA WAPI? hILI LIMUUNGANO KWANINI TUSILIVUNJE TU? MAANA WENZETU SABABU NA MALALAMIKO HAYAISHI!!
 
nimeamini kweli maalim karudi ccm. Haya ni matamshi ya chini kwa chini ya ccm zanzibar. Tanzania hatuachagua rais kwa kuangalia anatoka wapi bali tanzania kama nchi tunachagua mtu yeyote atakayetupeleka mbele. Urais si kitumbua cha kula na kuachiana. What if zanzibar hakuna aliyequalify? Yaani tumuweke mtu tu hata kama mwendawazimu?. Wanzibar waliisigina nafasi adhimu sana mwaka 2005 kwa kuacha kumuunga mkono salim. Wao wenyewe walimuanzishia fitina kuwa ni hizbu kwa ahadi za vyeo toka kwa wanamtandao. Sasa leo hii wapo nje ya vyeo wanamtumia hamad seif sharif.

Kwa mzanzibar kupata urais wa tanzania ni mpaka atakapopatikana mtu kma dr salim na hii itawachukua miaka hamsini ijayo.


wakifanikiwa kuingiza hicho kipengele kwenye katiba tu wameula!
 
Huyu anaongea hivi ili kuongeza kasi ya kuvunja muungano, kwani anajua fika bara hilo halikubaliki ndani ya NEC
 
Nimeamini kweli Maalim Karudi CCM. Haya ni matamshi ya chini kwa chini ya CCM Zanzibar. Tanzania hatuachagua rais kwa kuangalia anatoka wapi bali Tanzania kama nchi tunachagua mtu yeyote atakayetupeleka mbele. Urais si kitumbua cha kula na kuachiana. What if Zanzibar hakuna aliyequalify? yaani tumuweke mtu tu hata kama mwendawazimu?. Wanzibar waliisigina nafasi adhimu sana mwaka 2005 kwa kuacha kumuunga mkono Salim. Wao wenyewe walimuanzishia fitina kuwa ni Hizbu kwa ahadi za vyeo toka kwa wanamtandao. Sasa leo hii wapo nje ya vyeo wanamtumia Hamad Seif Sharif.

Kwa mzanzibar kupata urais wa Tanzania ni mpaka atakapopatikana mtu kma Dr Salim na hii itawachukua miaka hamsini ijayo.

Umezungumza kweli. Watasubiri sana,kama hawataki wajitoe ktk muungano. Hatuwezi ongozwa tena na mtu wa ajabu ajabu kisa eti muungano.
 
Agombee tuu tutamchuja kwenye uchaguzi mkuu au anataka wagombee wazanzibari tuu; kumbe unaweza kuwa na nafasi ya juu tu serikalini ila ukawa huna uwezo wa kufikili
Bonge la gamba! Seif anakuja kutueleza yeye hasa ni nani na kwa nini yuko mahali alipo. Kungekuwa na rais wa tanganyika tungefikiria zamu anazotaka sif. Hako kawilaya kakitoa rais....mhhhhhh! Anayetaka urais apeleke jina chamani kwake siyo leo kula na mimi nile kesho
 
Anachosema kina mantiki kubwa sana kama tunataka muungano otherwise tuvunje muungano kabisa.. maana yake ni hivi come uchaguzi say 2015; kila chama kitatakiwa kumsimamisha mzanzibar kuwa mgombea mfano:-

CCM: Watatakiwa kumsimamisha Rais Mzanzibar
Chadema: Watatakiwa kumsimamisha Rais Mzanzibar
CUF: watatakiwa kumsimamisha Rais Mzanzibar

Hivyo wapiga kura watachagua mzanzibar aliye bora katika hao..mimi naona hii honestly is very fair deal ili muungano udume tuache ushabiki..this is very fair
 
Anachosema kina mantiki kubwa sana kama tunataka muungano otherwise tuvunje muungano kabisa.. maana yake ni hivi come uchaguzi say 2015; kila chama kitatakiwa kumsimamisha mzanzibar kuwa mgombea mfano:-

CCM: Watatakiwa kumsimamisha Rais Mzanzibar
Chadema: Watatakiwa kumsimamisha Rais Mzanzibar
CUF: watatakiwa kumsimamisha Rais Mzanzibar

Hivyo wapiga kura watachagua mzanzibar aliye bora katika hao..mimi naona hii honestly is very fair deal ili muungano udume tuache ushabiki..this is very fair[/QUOTE

Na iwe hivyo pia kwa Visiani Rais ajaye atoke zBara!
 
we wacha longolongo hizo za kutaka kuiwash brain the Great thinker hapa.
Mzee Mwinyi sio Mzanzibari ni Mtanganyika aliishi tu Zanzibar kwa miaka kadhaa.


Born on May 8, 1925, in Kivure, Tanganyika; raised in Zanzibar (which joined with Tanganyika in 1964 to form Tanzania).
is a Tanzanian politician.[SUP][1][/SUP] He was the second President of the United Republic of Tanzania from 1985 to 1995.[SUP][1][/SUP] Previous posts include Interior Minister and Vice President.[SUP][1][/SUP] He also was chairman of the ruling party, the Chama Cha Mapinduzi (CCM) from 1990 to 1996.[SUP][1][/SUP]
Mwinyi married Siti in 1960 and has six sons and six daughters.[SUP][1][/SUP] In retirement, Mwinyi has stayed out of the limelight and continues to live in Dar es Salaam.
 
Huyu Maalim Seif kwa kupenda madaraka yaani hata sielewi...Huu mpango wa zamu unatoka wapi? hivi yeye akili yake anajua mkweli maana ya uchaguzi na vyama vingi yaani anataka kulazimisha kila chama kiweke mgombea Urais kutoka Zanzibar!. Hakika mzee huyu kaishiwa kisiasa kabisa na hafai hata kwa kulumbangia. Yaani nawasikitikia CUF kila kukicha maana anaondoa kabisa umaarufu wa CUF bara kwa siasa za utengano..

Muhimu lilia nafasi ya Zanzibar ktk Muungano. Zanzibar inatakiwa kuwa na pato lake la ndani States tax ambazo hazijumuishwi na federal Government kisha kuwepo na kodi ya Federal..Na itawezekana tu kama tutakuwa na serikali tatu bara wakikusanya kodi zao za ndani states na zipo za Federal ambazo zitashughulikia zaidi miradi ya Muungano. Unguja na Pemba ni visiwa ambavyo vinaweza kabisa kutumiwa kama port ya kusambaza imports na exports dunia nzima haya ndio maswala ya kuzungumzia na sio Urais. Mwinyi aliwasaidia nini zaidi Wazanzibar kuwa rais tofauti na JK..
 
Nadhani Tanzania ni nchi ya kidemokrasia ambapo magombea anaruhusiwa kutoka sehemu yoyote ya nchi, ndiyo maana vyama vya siasa haviwezi kusajiriwa bila kuthibitika kuwa vina influence sehemu zote za nchi. Kifungu cha sheria kinachotaka kila chama kutoa wagombea wawili: mmoja akitoka Tanganyika, na mwingine akitokea Zanzibar ndicho pekee kinachoweka mgawanyo wa madaraka baina ya pande hizo mbili za Muungano. Wakati Zanzibar ilipokuwa na mgombea mzuri sana ambaye angeweza kushinda kwa kishindo sana, yaani Dr. Salim, ambaye vile vile alikuwa anatoka Pemba kwa akina Hamad, wazanzibari hao hao ndio walioshiriki kumzika kisiasa. Sasa leo baada ya hamad kurudi CCM anataka apemwe mgao wa wa kuwa Rai9s wa Jamhuri kwa kutenga wagombea competent kutoka sehemu nyingine za nchi. Nadhani hii itakuwa ni kutangaza time dependent ubaguzi wa aina fulani.
 
Mnajadili maneno ya mfa maji Seif. Hivi vizee vimekula nchi toka enzi za Jumbe akiwa rais wa Zanzibar, sasa vimezeeka vinabwabwaja tu bila hata kufikiria, akili imechoka hiyo, enzi zake kwenney kabisa, analopoka tu ili naye aonekane yupo bado kwenye siasa, maana hata platform ya kuongea baada ya kumegewa kipande cha keki na CCM hana. We will never allow our president to come from armipit of Tanganyika. Zanzibar ni kiwapa cha mkono wa kulia wa Tanganyika. Kikwapa (Zanzibar) kinanuka tunakivumia tu kwani ni cha kwetu, subirini hiki kizazi cha vizee kiondoke, sisi tutawanyoa bila nyembe mpaka mkome... ebo!
 
seif umeshaona kwamba Tg, ni koloni mlilo rithishwa na babu zenu ehee!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom