Urais sio rahisi mnafahamu wanajamii forum? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urais sio rahisi mnafahamu wanajamii forum?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mkatamiti, Oct 26, 2010.

 1. M

  Mkatamiti Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DHANA YA KWAMBA URAIS NI RAHISI NI KUWATANIA WATANZANIA!

  • Wapinzani wakiongozwa na Chadema wanachotaka ni Urais basi!
  • Tena Urais wa kipindi kimoja tu cha miaka mitano!
  • Halafu wawapishe wenyewe waliowatuma ndio maana yake!
  • Suala la kuleta nafuu kwa maisha ni ghilba ambayo itaishia kupigiwa makofi kwenye viwanja vya kampeni halafu Watanzania wataachwa na ujaka wao kama sio solemba!
  • Ahadi za CCM ni za uhakika zinatekelezwa katika mchakato unaoeleweka,’ wahenga wanasema kawia ufike!


  Ninapoandika makala hii najisikia vibaya na kujiuliza inakuwaje wanasiasa kwa namna moja au nyingine waliowahi kuwa Wabunge katika Bunge la Jamhuri watakuwa mabingwa wa kutumia falsafa ya kulenga kufikia malengo ya kisiasa kwa njia yoyote hata kama itasambaratisha amani na utangamano wa nchi.

  Kitu gani hasa kimewakumba je ni uchungu kweli wa kutaka kuwahudumia Watanzania vyema zaidi au njama za kuwataka kuwatumia kama ngazi ya kupata madaraka kiurahisi tu!


  Kama uchungu kweli kwa nini wasifuate utaratibu wa kawaida kwa kutumia lugha za kistaarabu waliozozoweya Watanzania. Kule Kenya ukiwa baa unapiga mluzi fyee..! au unaita kwa makeke ..’ weye muhudumu lete kinywaji..’ na lazima alete! Lakini Mtanzania atasema..’ tafadhali muhudumu naomba unipatie kinywaji fulani! Kwa hiyo basi tuwakane na tusiwape kura zetu Wapinzani wanaopiga miluzi ya uchochezi, makwenzi, mapanga na bakora na kulazimisha tuwape kura zetu! Sasa lugha za kebehi , dharau na uchochezi lengo nini kama si ushawishi wa watu wapigane na kuvunja amani hapa uzalendo wa hawa Wapinzani bila ya shaka una mushkeli tena mkubwa na tahadhari ichukulie haraka! Wanasema akumulikaye mchana usiku atakuunguza! Mfano halisi kilichotokea kule Maswa hawa jamaa wamekusudia na kwa maana nyingine hii ni changamoto ya wazi kwa Vyombo vyetu vya Usalama visiwalazie damu! Mzaha mzaha mwisho utatumbuka usaha!

  Ahadi zinazovutia za Mgombea wa Chadema za kutoa elimu bure na kupunguza gharama za vifaa ujenzi zinaweza kutekelezeka kwa mikakati ya muda mrefu kama ya CCM na sio kipindi cha miaka 5 hii dhahiri huyu Mzee anawafanya Watanzania mabwege mtozeni na mazumbukuku , jamani tumsitukieni! Tunajua kwa rasilimali zinazokuwa chini ya uangalizi wa Rais Mgombea a upinzani akipata bingo hiyo kwa miaka 5 ataweza kukidhi uchu wa utajiri na kuwaondolea umasikini jamaa zake na wale waliomuunga mkono kuipata nafasi hiyo tu lakini sio Watanzania zaidi ya milioni 40! Awadanganye wale wanaotaka kudanganywa lakini ukeli unabakia hivyo maendeleo ya nchi ni mchakato wa muda mrefu sana hadi leo taifa tajrii la Marekani lina zaidi ya miaka 234 asilimia 11 ya raia wake ni masikini kuliko Watanzania sasa kwa miaka zaidi ya 234 Marekani haijaweza kufuta umasikini sasa huyu Mnafiki anasema ataweza kufanya hivyo kwa miaka mitano anamdanganya nani? Na hakika watanzania makini somo wamehslielwa msimamo Wapinzania warejeshwe darasani wakajifunze kutengeneza mtandao wa kisiasa kuandaa viongozi wenye maadali na wajidunze lugha ya staha, kutumia nguvu za hoja na kuwa sera zinazotekelezeka na endelevu! Huu utani wa mwaka huu uchukuliwe kama utani ambao mahala pake mwafaka ni katika vipindi vya ’ ze orijino komedi! Wakati fulani nilimsikia Mgombea wa rais wa Chadema anajigamba atapambana na EPA kwa nguvu zake zote lakini labda tumkumbushe huko nyuma wakati akiwa katika utumishi wa kiroho alikumbana na kashfa zinazofanana na EPA EPA hali iliyomfanya aache uchungaji wa kondoo wa Bwana bila ya kupenda , swali kama EPA katika utumishi wa Mungu ilimshinda ataweza kweli kushindana na EPA ya kidunia ama anatakuwa kuwa mshiriki wake kinamna na hasa anaposema atatua matatizo yetu kwa kasi ya ajabu ndan ya kipindi kifupi cha miaka mitano tu! Watanzania mambo hayo!

  Gharama za kutoa elimu bora, ujenzi wa miundombinu yake na kuwa na fungu la kutoa motisha kwa walimu ni mipango ya muda mrefu haiwezi kukamilika kwa kipindi kifupi cha miaka 5! Halikadhalika mpango wa viwanda vya kuzalisha vifaa vya ujenzi ni wa muda mrefu pia.

  Mchakato wa kubadilisha katiba sio lelema tunawasifia jirani zetu Kenya walioisimika hivi karibuni , ukweli mchakato wa kuiasisi na kuiandika katiba hiyo na kujiadili kwa kina umechukua takriban miaka 20 ya vute ni kuvute! Sasa huyu Mwenzetu anasema ataifanya kwa siku 100 hali hii na ahadi nyingine ndio zinazoleta dhana kuwa Urais ni rahisi jambo ambalo sio kweli hata kidogo!
  Mgombea huyu Watanzania anataka kutuuza tena kwa mkopo. Ukichunguza anataka kuweka rehani tunu zetu kuu yaani Amani , Utulivu, Usalama na Mshikamano! Tusithubutu kufanyia mzaha tunu zetu hizo kama ule msemo ‘bura yangu sibadili na rehani! Hata ulichonacho kinaonekana ni hafifu ni bora mara 100 kuliko pepo ya ahadi isio na ithibati!

  Halafu ahadi ya muungwana ndio ya kuenziwa kwa sababu kwa muungwana ahadi ni deni kama nilivyosema katika makala zilizopita Kwa kumnukuu hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa Mgombea Bora wa Urais nchini atatoka CCM kwa sababu ya umakini na bila ya shaka yeyote huyu ndio Muungwana tunaye mtafuta na ahadi zake anaziheshimu! Katika mikutano Mgombea wake amerejea zile ahadi zilizomo katika Ilani ya 2005 zilizotekelezwa na zile zinazoendelea kutekelezwa na hizi mpya za Ilani ya 2010! Hoja kwa wale wasiofahamu ahadi za 2005 utekelezaji wake ni endelevu kama ilivyo jamii ni dainamiki haisimami kama nukta sasa ni dhahiri Ilani ya 2010 inaendeleza utekelezaji wa Ilani ya 2005 kwa maana hakuna mpaka wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni kama mto unaotiririka maji! Sio ajabu katika ahadi za Mgombea wa Upinzani anakuja na dhana ya kubeza kwa hiyo ana nia ya kusitisha harakati za maendeleo halafu wasimike mauzauza yao! Watanzania wapenzi tusithubutu kubadilsha rubani wakati ndege ya maendeleo ikiwa angani atatubwaga huyu na imeshatokea katika nchi kadhaa duniani na hivi sasa wanajuta kuzaliwa!

  Kuna msemo kabla hujafa haujaumbika! Methali ambayo ina tafsiri nyingi mojawapo ni kuwa usicheke kilichomkuta mwenzio huenda kabla hujafa na wewe kikakukuta! Kumetokea dhihaka kutoka takriban kwa wasomi, Asasi za kuetetea wanawake na baadhi ya vyombo vya habari kujizuia kutoona mkanganyiko wa kimaadili kwa mgombea wa Chadema ambaye bila ya kuwa na haya wala soni ! Hata baada ya mwenye mke kujitokeza mimi nilifikiri kuwa kingelikuwa kitendo cha uungwana Mgombea huyu angejitokeza hadharani na kuungama na kisha kuomba msamaha kwa Watanzania na pia kwa Mume halisi wa ‘mchumba’ wake!( na mambo yangeisha hapo!) Lakini kama jogoo amekuwa akiranda na huyu shemeji yetu nchi nzima! Hapa tumepata somo gani na kwa wale wanaoshabikia au kufumbia macho ahli hiyo kweli ni haki hiyo! Kwa zile asasi za kutetea haki na vyombo vya habari vimejidhihirisha ndumila kuwili kwamba pale maslahi yataathirika kwa ‘Mgombea’ wao wako tayari kuwa kinyonga na kujifanya wameghaflika na kugeuza kichwa na kuangalia pembeni! Kwa Hali halisi lazima Watanzania wafahamu kama tutafanya makosa sio ajabu tukajikuta wake zetu na wapenzi wetu wako hatarini kuporwa! Maana kama hivi sasa Mheshimiwa huyu hajakuwa Rais anapora namna hii bila woga fikiria akichanganya na nguvu za dola tutakuwa tumekwisha!

  Shime Watanzania tusipandikize hofu katika jamii yetu ya kuporwa wake zetu na wapenzi wetu na kutapeliwa tusipate hata kidogo tunachopata sasa na wakati huo huo tusije kupata dhahama ya kukabiliwa na vipigo na kuuawa kupitia vyombo vya dola! ( Bila ya shaka Wasaidizi wa Mheshimiwa nao wataiga tabia ya bosi wao ya kuporapora na ndio itakuwa kasheshe kweli Tanzania)!
  Hivi sasa katika kampeni hawa jamaa wanatembeza kipigo na mauaji kama kazi je wakipata dola tutakuwa tumekwisha. Nawasihi Watanzania tusibahatishe tuchague chama makini ambaco ni CCM!

  Tathmini ya kawaidia inadhihirisha wapinzani wanacheza na hisia za watanzania na huu ni utapeli wa kisiasa wa aina yake Kuna msemo wa busara zimwi likujualo halikuli likakwisha. Hawa wapinzani chondechonde wataumaliza moja kwa moja, ya dhana ya uzimwi maana yake ni yale mapungufu ya utekelezaji ilani ambayo huweko sababu kadhaa mojawapo ni kwamba Watanzania ni binaadamu ambao hawajakamilika na pia huuchagua madiwani wa vyama tofauti hatimaye halmashauri zinatumia muda mrefu kulumbana! Sasa ili kuipa nafasi CCM kutimiza ahadi zao nzuri wapatieni uwezo usiokuwa na mashaka yaani mafiga matatu Rais , Wabunge na Madiwani kutoka CCM. Bila ya kusahau tamko la Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuwa abadan Rais bora Tanzania bila shaka yeyote atatoka kutoka Chama cha Mapinduzi ! Na kwa mantiki hiyo basi wabunge na Madiwani bora watatoka CCM. Chagua Amani, Utulivu , Usalama, Mshikamano na Maendeleo , chagua CCM!

  Mungu Ibariki Tanzania !
  Mungu Ibariki Afrika!
   
 2. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  haya,kaoge ukalalee mtoto mzuri.
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
 4. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Umeshajua kuwachokoza wenzio, unajua fika kitakachofuata kwenye thread hii.
   
 5. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  we crapist.. acha vilio kama vya kitoto kilichopata tohara, kitu gani kitafuatia?
   
 6. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Too late!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,109
  Trophy Points: 280
  Kumbe ameandika nini vile....sijui sijamwelewa au hajaeleweka. Kwahiyo??
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,109
  Trophy Points: 280
  wa lini huyu naye jamani, kaja lini huyu, katokea wapi vile naomba mnikumbushe>
   
 9. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  kinachofuatia ni kama hiki ulichoandika.
   
 10. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Wewe unaonekana ni mtoto wa kuotaota ndota na maluwe luwe!! pambafu
   
 11. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,109
  Trophy Points: 280
  Yamekuwa haya tena?? kwa heri
   
 12. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Tatizo la kuandika post ukiwa unajinyea ndo hilo.

  Pole sana.

  Katawadhe ndugu.
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,109
  Trophy Points: 280
  tusiwajibu vibaya, twende nao taratiiiiibbbbbbbbbuuuuuuuuuuu kama speech ya Dokta wa Ukweli
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kwanza karibu sana jamii forum pili unapoandika hii makala sijui unakuwa umetumwa au kueneza propaganda. Mosi lugha za uchochezi na kebehi zimeanza kwa CCM kuanza kusema mdahalo ni kwa watu wasio na elimu (watu wa kariakoo ukikumbuka statement za katibu mkuu wa CCM).


  Pili ukija katika hoja ya Slaa ni mnafiki na akipata urais atajitajirisha yeye na familia yake kwani CCM wanafanya nini? Mara nyingi mwenye kuona mwenzie mgoni au mwizi utakuta yeye ndie mwizi mwenyewe kwanini usiseme tutashirikiana na slaa kuondoa umaskini?

  Nakutakia kila la kheri na propaganda zako lakini humpati mtu
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Asante sana ! nilikuwa sijasoma Pumba muda mrefu
   
 16. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hata mimi nakubali urais si "rais",nikiangalia na kutafakali jinsi jk alivyouchukulia ki-"urais"na namna alivyoelemewa na ahadi na ahadi 83,ili awetena "rais".........!!! Sipati picha kamili.
   
 17. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  kipi hicho crapist?
   
 18. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli Urais si rahisi umemshinda Kiwete
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Another mythomaniacs !
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  @ Mkatamti... unfortunately nakubaliana na wewe... but probably tunatofautiana kitu kimoja, upinzani lazima uwepo na regardless at what level, presidency ndio core ya upinzani kwa sasa kwani at grass-root level hakuna plain level field

  Its a good start kwa sasa na in 2015 movement will spread to the lower levels
   
Loading...