Uchaguzi 2020 Urais ni taasisi na cheo cha hadhi kubwa sana, hatuwezi kukigawa kwa huruma wala kwa muongo

Jan 12, 2019
40
125
Tundu Lissu ni moja ya wagombea wanaoendelea kujinadi maeneo mbalimbali kwa Watanzania akitaka achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Namfuatilia sana Ndugu Lissu kwenye kila mikutano yake anayonadi Sera zake lakini sidhani kama kwa kiwango cha nafasi ya Urais anachokitaka kinaendana na kariba yake, hadhi ya cheo chenyewe cha Urais kama taasisi ya heshima kubwa kabisa.

Kiongozi wa nafasi kubwa kama ya Rais ni lazima apimwe kwa mienendo yake mbalimbali ya vitendo, kauli na ukweli ndani yake. Anayoyanadi kwenye mikutano yake ndio aina na mwelekeo wa kiongozi huyo hata akipata madaraka. Kiongozi muongo ni dhahili anatia doa na hofu ya uwezo wake kwenye nafasi hii inayomtaka mtu mchamungu na mkweli sana.

Lissu kwenye mikutano yake amekuwa akilaani vikali na kupinga kitendo cha Serikali kununua ndege kwa kuhoji faida ya ndege hizo. Baada ya kauli yake hiyo anayoitaja kila mahali na kuifanya kama ajenda yake nilitarajia na kutegemea kwamba Lissu angetumia magari kote huko apitako kwasababu ndege hazina faida lakini cha ajabu nimeshangazwa na kumuona Lissu huyuhuyu anayeponda na kupinga ununuzi wa ndege kumuona na yeye akipanda ndege hizo. Hii inatoa picha na somo kwa Watanzania juu ya aina ya Ndugu Lissu.

Kwenye mikutano ndege hazina faida lakini baada ya mkutano anapanda hizohizo. Huu ni unafiki kwa mtu anayetaka cheo cha ngazi kubwa kama ya Urais.

Lissu akiwa Shinyanga alinukuliwa akisema yeye akiwa Rais ataruhusu wafugaji kufugia kwenye hifadhi zetu za wanyama bila bughudha yeyote ile. Sasa jaman Watanzania wenzangu tujiulize kidogo hivi mbuga za wanyama zinazotuingia Mabillion ya pesa na kuwa Sekta ya pili kwa kuchangia pato la Taifa Lissu anasema ataiharibu na kwa kuwaruhusu wafugaji na watu kufanya wanachokitaka. Hii mlisikia wapi?

Hapo hujazungumzia huruma ambayo amekuwa akiitia kwa Watanzania kila siku kwa tukio lake la kupigwa risasi. Yan leo Lissu aende Ikulu kwasababu ya risasi alizopigwa. Wakati Watanzania wakitaka kusikia Sera zinazogusa maisha yao kwenye maji, elimu, barabara, afya na ustawi wao yeye stori na Sera kwa Watanzania ni risasi. Yani hii ndo Sera kuu ya Lissu. Yaani dhamana nyeti kama ya Urais mtu achaguliwe kwasababu ya Sera ya kupigwa risasi. Yani tutakuwa nchi ya ajabu sana duniani.

Zaidi Lissu ameendelea kuwakanyaga wamachinga na wajasiriamali wadogo kwa kudanganya sana. Jana pale Dodoma Lissu alipinga hadharani utaratibu wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo. Hivi kwenye nchi hii nani asiyejua namna wamachinga walivyosumbuliwa kila mahali nchi nzima kwa kutozwa makodi ya ajabu ajabu na kufukuzwa kila mahali.

Utaratibu wa kuwalinda watu hawa ili wafanye biashara zao bila bughudha na mtu yoyote kwa kuwapatia vitambulisho maalum na kulipa elfu 20 tu kwa mwaka badala ya hela walizokuwa wanatozwa kila siku Leo Lissu anaponda. Tunaweza kuwa tofauti kwenye itikadi na imani zetu kisiasa lakini linapokuja suala linalogusa maisha na maslahi ya watu siasa ni lazima ijitenge na uhalisia.

Uongozi ni dhamana na matendo na mienendo mizuri sasa ukiona mtu anayeomba Urais anakuwa na tabia za namna hii kwakweli inashangaza na kutia wasiwasi sana. Watanzania mnalo jukumu la kwenda kufanya maamuzi Oktoba 28.
 

mwajuma270

Member
Sep 5, 2020
6
45
Watanzania tujipange kuwapima wagombea wetu kwa hoja na tufanye maamuzi ya busara tarehe 28/10/2020 ya kumchagua kiongozi atakae tuletea maendeleo pamoja na kuliweka taifa letu katika hali ya amani na utulivu wakati wote.Hakuna kiongozi kutoka nje ya tanzania atakae tuongozea nchi yetu.Tuwe makini na vibaraka na mifano mizuri tunayo tuwaangalie wenzetu wa libya leo wanajuta kwa maamuzi waliyo yafanya ya kumuondoa kiongozi hodari alikua mzalendo wa taifa lake.Kila nchi ifanye maamuzi yake binafsi na hakuna mwenye haki ya kuingilia uhuru wa taifa lingine.kazi kwenu watanzania Tarehe 28/10/2020 mtaharibu au mtatengeneza?
 

sylver5

Member
Jul 22, 2013
8
45
Rais hata awe ana tabia zipi litmus test ya kama anafaa kuongoza nchi ni wananchi wenyewe provided he/she is of sound mind
Hamna taasisi au mamlaka inaweza ikatengua maamuzi ya wananchi pale waamuapo (ikiwa tu vigezo vya kikatiba vimezingatiwa)
All in all upinzani ukajipange; waliteke bunge la wananchi kwanza na mengine kama urais yatafuata
 

Makani_evarist

Senior Member
Sep 5, 2020
191
250
Lissu Ni tahira Kama matahira wengine. Huwezi kukisema kitu kibaya halafu at the same time unakitumia baada ya mkutano. Ndo maana hata kwenye mikutano watu hawaji.

IMG-20200913-WA0078.jpg
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,021
2,000
Na tunajua tukichagua Chadema wataanzisha vita Tanzania na sisi tuna ndugu zetu wazee wengine wagonjwa tutakimbilia wapi?
Huyu anayeteka na kuuwa watu je? Huyu mshamba na limbukeni anatukana watu kama mbwa. Anafaa huyu dikteta?
 

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
6,961
2,000
Mbona kiti hicho kimekaliwa na mtu mshamba sana anaetembea huku anatafuna mahindi barabarani!? Mwenye roho mbaya, katili, aliejaa kiburi na muuaji?

Tumuondie nduli huyu kwanza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom