Urais hali tete....presha inapanda presha inashuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urais hali tete....presha inapanda presha inashuka

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Halisi, Nov 1, 2010.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  KATIKA historia ya chaguzi zote, mikoa yenye idadi kubwa ya watu ya Kanda ya ziwa, kanda ya Nyanda za Juu kusini na mkoa wa Dar es Salaam ndipo ambako chama tawala kimekua kikipata ushindi wa kishindo. Kwa uchaguzi wa mwaka huu, mambo yamekua tofauti.

  Pamoja na kuwa kuna utata wa ajabu katika baadhi ya majimbo (mfano Hai na Iringa) ambako kura zimejichanganya (mfano Mbowe 118 Kikwete 118, Fuya 77, Slaa 75) bado Chadema imejikita na kufanya vyema katika mikoa ya kanda ya ziwa, ya Mwanza, Kagera, Mara na Shinyanga na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ya Mbeya na Iringa na kugawana kura na CCM mikoa ya Ruvuma, Kigoma na Rukwa huku CCM ikipata ushindi mkubwa katika mikoa ya Pwani, Tanga, sehemu ya Dar es Salaam (wanakogawana na Chadema na CUF) na mikoa ya Lindi na Mtwara (wanakogawana na CUF), mikoa ambayo ina idadi ndogo ya watu, pamoja na mikoa ya Zanzibar na Pemba ambako nako CCM na CUF wanagawana.

  Mikoa mingine yenye idadi ndogo ya watu ya Morogoro, Singida na Dodoma nako CCM imefanya vizuri lakini Chadema nako imeambulia kura, kama vile jimbo la Singida Mjini ambako ni ngome kuu ya CCM, JK amepata kura zaidi ya 19,000 na Chadema kuyra 5,000, hizo si haba kabisa ukilinganisha na matokeo ya kanda ya ziwa na Nyanda za Juu Kusini.

  Ukiangalia matokeo yanayotangazwa na NEC utaona wamechukua kwa kiasi kikubwa matokeo ya mikoa ya Zanzibar na Pemba, na mikoa ambayo CCM imefanya vizuri. Jambo la ajabu sana hata Arusha na MWanza ambako wametangaza matokeo ya Ubunge, wanaruka kutangaza matokeo ya Urais.

  Katika majimbo ya Ubungo na Kawe, wamezidi kuchelewesha kama walivyofanya Arushwa, Nyamagana na Ilemela na Hananga matokeo yanachanganya ambako Mary Nagu anaelezwa kwamba ameshinda kwa tofauti ya kuyra 45 kama ilivyo matokeo tata ya Kigoma Mjini, ambako Peter Serukamba, yamewachanganya watu wa Kigoma.

  Kwa uchambuzi huo, hali si shwari kabisa na kama MWanza, Arusha, Ubungo na Kawe wamekuwa wagumu kukubali matokeo, haijulikani hali ikoje kwenye matokeo ya Urais wa Muungano na kule Zanzibar.
   
 2. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Haya mambo ya recount ndiyo yanaharibu kila kitu kwa kura za upinzani. CCM wamepoteza uraisi (na au kama wakishinda ni kwa margin ndogo sana) ila hawataki kukubali hili.
   
 3. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  unanamana Nagu kashinda mkuu....inaniuma kishenzi kam ndivyo
   
 4. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu watabana weeee mwishowe wataachia,inasaidia pia kwa jk kuaacha ngazi maana hana mawaziri
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Nov 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Habari zote ambazo inteligentsia ya ka-nzi inadokeza ni kuwa ilibidi watoe matokeo hayo ya Urais ili kudemoralize mashabiki wa Chadema kuonesha a massive win for JK. It was a psychological trick which seems to backfire kwani matokeo yanavyozidi kukusanywa kutoka kwa majimbo.. mshindi wetu anaweza akawa chini ya 55% hivyo majimbo ya Mbeya, Songea, Mwanza, Shinyanga n.k yanawasumbua sana..

  Watu wasikate tamaa au kuanza kugive up na kukubali kura zimechakachuliwa. Nilisema mapema hapa kuwa ni vigumu sana kuiba kura na kwenye urais itakuwa ni ngumu zaidi.. Endapo Dr. Slaa ataamua kujitokeza kesho Jiji la Dar litalipuka kwa matumaini.. lakini hawawezi kabisa kulazimisha ushindi kama walivyoahidi.

  Tayari CCM imepata pigo kubwa kabisa katika historia ya chama hicho chini ya utawala wa Rais Kikwete, hili ni pigo linaloacha mwangwi! Lakini heshima yake yote sasa imebakia katika kushughulikia kura za urais.
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Jamani hali ni tete
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Nov 1, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  yaaah niuchaguzi wa kihistoria, Mwanakiji ndani ya masaa 30 yaliyopita vijana hapa mwanza wamelala masaa chini ya sita, wakiapa kulinda na kusimamia kila hatua ya zoezi zima la upigaji kura, na kisha wakaamua kuwaonesha Tume kuwa ninini maana ya nguvu ya umma, pale walipoamua kwa vitendo kutaka kuingia ndani ya majengo yanayotumika kutangazia kura, ili kuwashinikiza watangaze matokeo, WATU WAMEBADILIKA, NCHI IMEBADILIKA SANA.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,947
  Trophy Points: 280
  vijana wa mwanza wameilinda vizuri haki hao walijitokeza kwa wingi jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye historia ya vyama vingi,
  natumai hawa nec pamoja na mizengwe ya lakini itakuwa ngumu kuuzima moto uliokwisha kuwaka sasa hivi wanacheza na mind za watu na waliogundua huu mchezo nadhani bado ni wachache sana
   
 9. O

  Obama08 Senior Member

  #9
  Nov 1, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ndio mkuu, Mwanakijiji, mm nilishaona hilo, kila mtu amesema wanaanza na kule CCM iliposhinda ili kuwapumbaza, kuwahadaa kisaikolojia, ili watu wkate tamaa, hata Zenj walifanya hivyo hivyo, mahala ambapo CHADEMA wameshinda wana kataa kutaja kabisa hadi ghasia already started, look Arusha, Mwanza, Ubungo, Kawe nk ila wamekiona wabunge, Urais nasema ni hatihati,
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Kwa mtu asiyejua maana hawezi kuambiwa maana. Tulipiga kelele sana warekebishe mambo wakadharau na kutuona wadaku. Leo hii wanavuna walichopanda and that is the universal law which no one can violate including our politicians.
   
 11. k

  king ndeshi Senior Member

  #11
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sio kama nauburi udini no.! ila sehemu nyingi alizo kimbiza jk zina idadi kubwa ya vibarakashee na madira,na ndo maana ukicheki utakuta wana gawana vibarakashee na CUF,next TIME siangalii sera ni IMANI MKAZI. FAAAKI PISI.:israel:
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Trick ya NEC niliigundua mapema sana ila wamechemsha
   
 13. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ninakubaliana na Mwanakijiji kwa asilimia 100. Matokeo ya mwaka huu ni pigo kubwa sana kwa ccm na wanaharakati tunatakiwa kutovunjika moyo kabisa kwani ukombozi hufanywa hatua kwa hatua. Mimi ninapendekeza baada ya purukushani hizi za uchaguzi wanaharakati tukae na kufanya uchambuzi wa kina hatimaye tu-define roadmap mpya kuelekea ukombozi kamili mwaka 2015. lundo la ahadi za kufikirika alizotoa jk kwa watanzania ni mojawapo ya silaha za maangamizi zitakazotumika kubomoa ngome ya mafisadi.

  Nina mengi ya kuongea kuhusu mwelekeo mpya wa harakati lakini nadhani kwa sasa siyo wakati wake.

  Pipoooooooooooooooooooz ..........................
   
 14. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM have nothing to celebrate even if NEC declares them to have won over 100%. Watanzania walifanya kazi nzuri na huwezi kutegemea zaidi ya hapo katika uchaguzi ambao mtawala ndiye refa wakati huo huo akiwa mshindani. Naomba Slaa ajiandae kujenga Imani ya watu hawa na kuwapa matumaini ya ushindi. Katika fair ground CCM ni chali ya mende. Najivunia watu wa Maswa, meatu, shinyanga, Musoma na nyanda za juu kusini kwa kazi nzuri sana waliyofanya. Kwa kweli Bunge halitatosha. Aluta continua
   
 15. coby

  coby JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  WanJF aliyekaribu na wabunge wateule kwenye majimbo yote ambaya chadema imeshinda muwahimize wasiridhike wakaingia mtaani kusherehekea huku wakiacha nyuma yao jamaa wanachakachua matokeo ya Dr. Slaa kwani nimenotice jamaa wanawachelewesha ili wakiwaachia msherehekee sana huku wao wakifanya mambo.
   
 16. nzitunga

  nzitunga Senior Member

  #16
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni hatari sana. Iringa ilibidi wananchi watishie kuingia ndani, ilibidi wananchi watishie kuvamia ofisi za manispaa. Hii ni hatari kwa chama tawala kutumia mabavu. Check this video from Iringa. [video=facebook;109262512473616]http://www.facebook.com/video/video.php?v=109262512473616[/video]
   
 17. k

  king ndeshi Senior Member

  #17
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sio kama nauburi udini no.! ila sehemu nyingi alizo kimbiza jk zina idadi kubwa ya vibarakashee na madira,na ndo maana ukicheki utakuta wana gawana vibarakashee na CUF,next TIME siangalii sera ni IMANI MKAZI. FAAAKI PISI:A S angry:
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Someni bandiko la Hutaki Unaacha kwingineko kwenye JF hii
   
 19. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #19
  Nov 1, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
Loading...