Urais bila majority bungeni una faida? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urais bila majority bungeni una faida?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Jun 23, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Leo kuna mdau hapa JF kasema kitu ikanifanya nifikirie hili swala. Je ikatokea chama kimoja kika shika serikali na kingine kikawa na idadi kubwa zaidi ya wabunge ina faida? Mimi naona hapa yatatokea moja kati ya haya.

  1. Kutakuwa na uwiano mzuri wa madaraka yani checks and balances. Kwa maana hiyo chama kinaacho shikiria serikali haiweza kufanya ndivyo sivyo ikijua wabunge wao wata pitisha tu agenda yoyote watakayo ipeleka bungeni. Kwa maana hiyo hapa itailazima serikali kupeleka hoja bungeni ambazo zinaonekana wazi ni kwa manufaa ya taifa ambalo bunge lenyewe ni lazima lipitishe.

  2. Shughulu za serikali zitasimama na uendeshaji wa serikali utakuwa wa tabu zaidi. Kwa maana hiyo kunakuwa na deadlock. Hii itatokana kama chama chenye wabunge wengi zaidi kikiamua kususia hoja mbali mbali za serikali makusudi ili serikali ionekana imeshindwa kutimiza wajibu wake.

  Swali langu ni je kama hali hii ikitokea Tanzania lipi kati ya haya mawili lina nafasi kubwa la kutokea? Kwa hali yetu ya kisiasa je itatokea sababu namba moja au itatokea sababu namba mbili? Je kuna uwezekano wa kutokea scenerio tofauti na hizi mbili? Ni scenerio ipi hiyo nyingine inayoweza kutokea?
   
 2. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Hii unajua kuwa haiwezi kutokea labda kwa generation yako ya tatu. Amka, acha kuota ndoto za majinamizi mchana kweupe!
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Jun 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,054
  Trophy Points: 280
  ..Katiba yetu inaelekeza kwamba Waziri Mkuu atateuliwa miongoni mwa wabunge wa chama chenye majority bungeni.

  ..pia Raisi atateua baraza la mawaziri kwa kushauriana na Waziri Mkuu.

  ..kwa kifupi chama chenye majority bungeni ndiyo chenye madaraka ya kuunda serikali/baraza la mawaziri.

  ..i believe there will be more checks and balance in our country if the President does not belong to the party that has a majority in the parliament.
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu unajua maana ya "what if"? Unajua maana ya hypothetical wuestion? Mimi nimeuliza kama if this was to happen je itakua bora ama la? Inaelekea lugha tabu. Anyway asant kwa your opinion?
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  O.K. mkuu nimekupata. Ila unajua kwamba nchi nyingi zingine zenye parliament system watu hawachagui mtu kuwa raisi. Wana chagua chama halafu chama chenye majority kinamchagua mtu wao kuwa raisi. Sasa Tanzania watu mnaenda kuchagua raisi then pia mna chagua wabunge. Which means kuna possibility wabunge wa chama fulani kuwa wengi zaidi ya wabunge wa chama cha raisi. In that case what happens? Ni katika kutaka kujua zaidi mkuu.
   
 6. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Acha kuota ndoto za majinamizi!
  hakuna kitu kama hicho labda karne ya 22 au 23.
   
Loading...