Urais 2030: Dkt. Mwigullu Nchemba na January Makamba wana nafasi nzuri kuliko Dkt. Hamis Kigwangalla

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,763
Ikumbukwe hawa vijana wadogo watatu Mwigulu, January na Kigwangalla waligombea urais 2015 japo safari yao iliishia kwenye kura za maoni.

Niliwapa jina la Three the Hard Way.

Safari inaendelea japo naona Dkt. Kigwangalla ameachwa nyuma kidogo lakini kwenye Marathon ushindi ni mbinu na ujanja so lolote linaweza kutokea 2030.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Yan Kigwangalla umuweke katika wanaoutaka Uraisi? Tanzania iongozwe na Kigwangalla?

Rais wa Tanzania Mwaka 2030 hatakuwa mtu maarufu na Tanzania hii mtu aliyetabiriwa urais akawa ni mmoja tu Jakaya Kikwete wengine woote waliangukia pua kila aloibuka hakuwa akitegemewa

Nakuuliza swali Ungemuuliza mtu mwaka 2014 tu kwamba akutajie maraisi wajao angekutajia Kina Lowassa au Membe na Kina Sitta Ila sasa akaja Kundenge!

Hapo sasa ungemuuliza mtu mwaka jana kwamba Rais baada ya Magufuli ni nani angekwambia Bashiru au Makamba Lakin ni SAMIA na hamuamini 😂. Sasa kitakachowakuta ninyi unashangaa akina Byabato au Nauye ndo wanakuwa Marais ninyi mko kwa ngonjera
 
Hivi hii nchi imekuwa ya kugawa urais sio? Ndio maana waafrika tuko nyuma umasikini kila kona sababu ya kuacha watu wajinga wasiokuwa serious kupewa urais, Yani mwigulu? Makamba? Seriously? Anyways 2030 bado sana. Labda watatokea watu wenye akili upinzani.
 
Kama tunahitaji Tanzania tule maziwa na asali tunahitaji dictator kuliko JMP, Raisi anatakiwa aendane na Hitler kidogo ilitutoboe.... kati ya hao hakuna hata mmoja mwenye caliber hizo hao labda nafasi za uwaziri ndio zinawafaa ..tuwe serious kidogo watanzania jabali ni gumu sana kutoboa tunahitaji kidume chenye uthubutu....vita ya uchumi inahitaji serious people....
 
Nchi tunampa Mtaka.
====
Nadhani unapima upepo....na mimi nimeweka ukuta kumkinga Rais wetu wakati huo.
 
Inasikitisha watanzania kuwa tushajiwekea kuwa ni watu wa kundi fulani tu ndio wanapaswa kuwa viongozi/maraisi. Imekuwa kama vile ni wao pekee ndio wenye uwezo wa kutawala na wengine hawafai/hawawezi.
 
January is back in the game....Mwigulu ataanza kukosa usingizi. 2025 au 2030 cheche zitaruka.
 
Back
Top Bottom