Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Hizi habari za Membe naona zimekuwa nyingi ,ni either watu wake wanapima upepo au kambi ya maadui wanafanya kitu inaitwa pre-empty. Ila ukimya wa Membe unaweza kuwa na kishindo kikubwa,kikatikisa kusini adi kaskazini,mashariki adi magharibi.
 
Niwazi kuwa kuna watu watatoka mapovu kwa ushauri huu, lakini hakuna jinsi dawa hata kama ni chungu ili tupone hatuna budi kuimeza, ukweli ni kwamba mh B C Membe ni mwanadiplomasia aliye bobea sana katika nchi yetu , ni kiongozi anayeweza kurudisha heshima yetu kama watanzania katika sura yake ile ya zamani.
Kulingana na hali ilivyo na hakuna asiyejua kuwa wananchi wana mhitaji MTU atakaye waletea faraja na kuwafuta machozi ambayo kila mmoja Amelia kwa njia zake wengine sasa imebaki na michirizi mashavuni mwao huku wakiwa wamekata tamaa kwani haijui hatma ya kesho yao, bomoa bomoa imeliza wengi , wanafunzi katika vyuo vikuu wamebaguliwa kwenye mikopo, ajira imekuwa nikilio kisicho koma kila kukicha, wakulima ndo usiseme hawajui hatma yao nini ukianzia kwenye pembejeo hadi kwenye masoko kwao ni giza tu, wafugaji hawana maskani katika nchi yao kila wanapo hamia kwa ajili ya kulisha mifugo wanaonekana kuwa maadui wanafukuzwa wamebaki kutanga tanga ndani ya nchi yao,wavuvi ndo usiseme nyavu zimechomwa kwa kile kinacho itwa nyavu haramu bila ya kuonyesha mkakati wa kuzileta hizo nyavu bora, wafanyakazi wamesha nyanyaswa mpaka basi, mishahara haipandi , madaraja hawapandishwi, wafanya biashara ndo usiseme wamebanwa na mfumo wa kodi usio kuwa rafiki na biashara zao. Yapo mengi sana.
Na ndio maana mwanadiplomasia makini kama Membe ana hitajika, awe ndani ya CCM au hata nje ya CCM , umefika muda muafaka sasa jitokeze 2020 watanzania wakupe kura za kutosha na bado nasema Membe unatosha sasa kuingia ndani ya gari letu ,funga mkanda, shika usukani, washa gari safari mpya ianzwe.
Unamwitaji WEWE PEKE YAKO
 
Rais anatoka kwenye baraza la mawaziri..
Hatujawai kuwa Rais kutoka nafasi ya uwaziri mkuu .
Ni mapema sana kuanza kumzushia mzee wa watu habari kama hizi. Yuko busy na uandishi wa kitabu chake.

Si December wala Camillius..!
 
Hata sasa mfanye awe rais wa familia yako. Ukishakunywa ukalewa unaanza kuongea mataka taka.... Yaani membe naye awe rais?mitanzania sijui imerogwa na nani...inakosa akili hata ndogo tu za uelewa... Mnataka kutuletea matakataka mengine ikulu? Mnaleta kichefu chefu kwenye mambo ya msingi...hovyo kabisa .. awe rais na mumeo kbisa.wewe na familia yako.umetutukana sana
 
Back
Top Bottom