Urais 2015 wamweka pabaya Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urais 2015 wamweka pabaya Rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Questt, Jun 28, 2010.

 1. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Imeandikwa na Sadick Mtulya

  VYOMBO vya dola nchini vinahaha jinsi ya kuua makundi ndani ya CCM ili kumtengenezea mazingira mazuri yatakayomuwezesha Rais Jakaya Kikwete kuongoza nchi bila ya matatizo na kupata mrithi wake mwaka 2015, Mwananchi imeelezwa.

  Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa harakati za kila kundi kutaka mtu wao ashike nchi mwaka 2015 zinazidi kuongezeka huku uhasama ukionekana dhahiri kuanza kuibuka, hali ambayo inaonekana kuwa itamuweka katika hali ngumu Rais Kikwete baada ya kuchaguliwa kumalizia ngwe ya miaka mitano.

  Hatua hiyo inakuja wakati ikielezwa kuwa vigogo wengi ndani ya CCM wamejipanga kujitokeza kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi ya urais wakati Kikwete atakapomaliza muda wake mwaka 2015 iwapo atashinda kwenye uchaguzi wa mwaka huu.


  Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, kila kundi ndani ya CCM linajiandaa kusimika mtandao wake mpya kwa ajili ya kushika nchi mwaka 2015 hali ambayo itamuweka rais kwenye hali mbaya kiutawala.


  “Mwaka huu hakuwezi kuwa na mpambano wala mvutano mkubwa ndani ya CCM katika nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani atakayejitokeza (kupambana na Kikwete) atakuwa amejimaliza kisiasa," alisema mpashaji habari wetu.


  “Vigogo wa makundi wanayotaka nafasi ya urais kupitia CCM wameelekeza nguvu kubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Kutokana na hali hii vyombo vya usalama vinahangaika jinsi ya kuweka mazingira mazuri ya utawala wa Rais Kikwete pamoja na kumpatia mrithi sahihi.”


  Habari zinasema vyombo vya usalama vimekwishaanza kazi hiyo ambayo lengo lake ni kuinusuru nchi isiweze kuingia katika machafuko kutokana na wengi wa wanaotarajiwa kujitokeza kugombea urais 2015 wanautaka kwa dhati na wana ushawishi mkubwa ndani ya chama na serikali na pia wana uwezo wa kifedha.


  Pia chanzo chetu kilisema vyombo hivyo vimeingilia suala hilo ili kunusuru mgawanyiko mkubwa unaoweza kujitokeza ndani ya CCM kutokana na kwamba tayari katika miaka mitano ya utawala wa Rais Kikwete kumekuwepo na hali ya kutoaminiana kwa baadhi ya vigogo na kusababisha mgawanyiko.


  Pamoja na mambo mengine, katika uwatala wa miaka mitano ya Rais Kikwete inayotarajiwa kuamlizika hivi karibuni, moja ya sauala ambalo haliwezi kusahaulika ni kuibuka kwa makundi mawili hasimu yanayopingana, huku moja likijinadi kupambana na vitendo vya ufisadi na lingine likipinga vita hiyo.


  Chanzo chetu kilisema kutokana na kuwepo kwa hali ya kutoaminiana, kila kundi linapigania kushika madaraka ifikapo 2015 ili liweze kusimika mtandao wake.


  Hata hivyo, habari zimesema mbali na vyombo vya dola kuhaha tayari kuna mpango maalumu ulioanza kutekelezwa wa kuyaweka pamoja makundi hasimu ili yaondokane na siasa za chuki.


  Sehemu ya mpango huo unaelezwa kutekelezwa ni kuwakutanisha pamoja na kuwasifia baadhi ya viongozi wenye nguvu kutoka katika makundi hasimu katika mikutano na vikao mbalimbali vinavyofanywa ndani ya chama na serikalini.


  “Kama utafuatilia kwa umakini katika mikutano na vikao mbalimbali inayoendelea, utasikia viongozi kadhaa wakisifiwa na kupongezwa kutokana na mambo mazuri waliyoyafanya katika uongozi wao,” alisema chanzo.


  Chanzo: Mwananchi
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ama kweli Miafrika ndivyo tulivyo... sasa hawa Mwananchi badala ya kuzungumzia ya mwaka 2010 wanaenda hadi mwaka 2015.. Dalili ya kukata tamaa kabisa kisha ati kuna watu wanaamini JK atashindwa uchaguzi huu..CCM hakuna makundi, kuna Unafiki tu wakimsifia JK anapokuwa nao kisha kumbeza anapowapa kisogo. Hii ndio tabia ya Miafrika lakini hakuna mkweli baina yao.

  Kama wangekuwa wakweli vikao vya kamati kuu na mkutano mkuu uliopita usingefikia muafaka baina ya viongozi wa makundi haya..Nilisha sema as long as Sitta na Wapiganaji walikubali kusuluhishwa na Mafisadi (shake hand with devil) they have no case against JK..
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  kundi lingine la wana ccm linataka kuja kuifisadi tanzania 2015,watu wanaangalia maslahi yao binafsi na sio maslahi ya taifa.

  siku hipo Mungu atajibu kilio cha watanzania wanyonge wanaoteseka kupitia uongozi mbovu.
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani hapa mimi ndiyo nachoka kabisa!
   
 5. m

  matambo JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  it looks mere hearsay than truth

  what kind of scribing is this????

  no wonder uncle ben used to despise nyie waandishi!!!!
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu MS,

  Sasa ndo unataka kusemaje.....
  Mbona uko kundi lisilokuhusu?
   
 7. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Lete source...........
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  naomba kuuliza huyu mtulya na yule wa sauti ya ujerumani ni watoto wa Idris Mtulya?
   
Loading...