Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,582
- Thread starter
- #101
Mkuu Mkandara, baada ya kuongea na Dr. Slaa, nilimwelewa vizuri sana ndio maana nawashauri watu humu, wasimbeze Zitto!.Pasco, mimi nakoma na vijana wa Chadema wakimkomalia mtu hadi utamwonea Huruma..Dr. Slaa amekuwa kikataa kugombea toka mwaka 2010 muda wote alikuwa akisema hatagombea, CCM wakauvaa wakidhani Mbowe wakarusha madongo sana tu mara walotegemea hayakuwa..Wakati wa uchaguzi Dr.Slaa yeye mwenyewe alisema ni rais wa awamu moja tu, na baada ya uchaguzi kasema hayo alosema ukayasikia wewe tu, lakini yote haya nakuhakikishia hakuna ukweli wowote. Anaweza fanya lolote kinyume maana sii kiapo bali tactics za kisiasa
Alisema hatagombea, akagombea angekuwa Zitto nchi nzima ingekuwa kiza kwa laana ambazo angezipata..jamani mweee.. Huu ni wakati muafaka wa wanaChadema kujitambua wao wamesimama wapi na kuna hatari gani za kisiasa ambazo nina hakika watakisambaratisha chama wenyewe kama ilivyokuwa kwa NCCR, CUF na sasa Chadema bila mkono wa CCM direct.. CCM anajua sana kuvimaliza vyama na Chadema iko hatarini kifupi naanza kuhofia kama itafika mwaka 2015 wakiwa pamoja..
Nyerere hakumtaka Mwinyi, alimtaka Dr. Salim!, Mwinyi akaambiwa tutakutaja halafu wewe ukatae, ili kumpisha Dr. Salim!. Mwinyi alipokuwa nominated, hapo hapo wabaya wa Salim, wakamshika sikio, usikubali kukataa!, Mwinyi aliposimama, akakubali!.
Wakati wa Ben Mkapa, Boys II Men ndio waliokuwa most favourate!. Ben akaambiwa na wewe nenda kachukue fomu!. Ben kwa kujipima na maarufu wale, akajiona hawezi!, akalazimishwa na fomu alaletewa!.
Nadhani hiyo ni spirit ya Dr. kuwa kugombea urais, mpaka uombwe ubebelezwe!. Huu ni ule mtindo wa aibu za kimila za Mwanamke wa Kitanzania, hata apende vipi, hawezi ku advance mpaka kwanza atongoz... na kujifanya kukataa ndipo hatimaye hukubali!.
Siasa za mtu kusubiri kutongo... zimepitwa na wakati!. Sasa ni siasa za ukweli, unajipima, unajiona unaweza, sifa unazo, uwezo unao, vigezo unavyo!, why not try!.
Umasikini mkumbwa wa Watanzania ni kukosa moyo wa kujaribu "darring heart", people don't dare!, zinatangazwa kazi internationa post, mijitu inasifa, haiombi!, tunaendelea kugawana umasikini wetu!. Wakijitokeza wenye sifa, tunawakatika tamaa!. Lipumba ndie mgombea wa kudumu wa CUF kwa urais wa muungano na Maalim Seif, urais wa Zanzibar!. Jee Chadema nayo, inataka kutengeneza wagombea wa kudumu?!.