Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Jul 25, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,334
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Mara baada ya mazishi ya Mhe. Regia, (RIP), on route back to Dar, nilibahatika kukutana mahali na Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wibroad Slaa akiwa na wife wake, Fina, tuliendesha mazungumzo mafupi, informal, na miongoni mwa maswali niyomuuliza, ni hili la iwapo atagombea tena nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi wa 2015!.

  Nayakumbuka vizuri sana majibu ya Dr. Slaa kuhusu swali hilo!. Kwa vile mazungumzo yale hayakuwa rasmi, kuna uwezekano mkubwa, Dr. Slaa alizungumza "off the record", sio busara kuyaleta mazungumzo ya "off the record" kwenye public na kuyaweka "on the record" bila "idhini" ya msemaji.

  Kwa vile msimamo wa "Dr. Slaa kuhusu kugombea urais 2015, mimi naujua!, nawashauri, wale wote wanaumlaumu au kumshutumu Zitto, kuonyesha nia ya kuwania urais wa 2015 kwa tiketi ya Chadema, kwa kujenga mazingira "impliedly" not "expressly"!, wasimlaumu bali wamsupport!.

  Hivi kuna ubaya gani, kuonyesha nia ya kuwania the highest office?. Wote wanaoutaka urais, huitwa "presidential hopeful", hivi kuna ubaya wowote to aim high?!.

  My Take.
  Kwa vile mchakato wa kuwania urais wa 2015 bado haujaanza rasmi kwa vyama vyovyote, lakini tunashuhudia "presidential hopefuls" wa vyama mbalimbali wakijenga mazingira kupitia mikakati mbalimbali, nawaombeni wapenda demokrasia ya kweli, tuwe open minded kuhusu watu hawa, tusianze kuwanyooshea vidole vya kuwashutumu na kuwakatisha tamaa, bali tunapaswa kuwaunga mkono kwa nguvu zote ili at the end of the day, tumpate mgombea bora kabisa miongoni mwao!,

  Mfano hakuna ubishi kuhusu uwezo wa Zitto katika masuala ya organization na mass mobilization!, hakuna ubishi kuhusu nguvu ya Zitto katika ushawishi na kujenga hoja na kusimamia utekelezaji. Kama ni kweli Zitto ni "presidential hopeful" ndani ya Chadema na sasa anajenga mtandao wa kuandaa mazingira hayo, this is very healthy kwa Chadema, kwa sababu by the time muda wa mchakato rasmi unawadia, Chadema iwe na pool ya wagombea wenye sifa za urais, na ikampitisha Dr. Slaa kupeperusha tena bendera ya Chadema, huo mtandao wa Zitto ndio utakuwa an added advantage kwa ushindi wa kishindo wa Chadema, na Zitto ndio atafaa zaidi kwa post ya Waziri Mkuu, kama alivyofanya Obama na Hillary Clinton!.

  Kufuatia mimi kuufahamu msimamo wa Dr. Slaa, lets support Zitto or anybody else!,

  Mhe. Zitto, just follow your dreams, "Sky is the limit!".

  I wish Zitto all the best!.

  Wasalaam.

  Pasco. (wa jf).

  NB. Pasco wa jf, sio mwanachama, mshabiki au mkereketwa wa chama chochoite cha siasa, bali ni muumini wa demokrasia ya kweli.

  Update 1.

  Kufuatia hoja nyingi ambazo zimeibuliwa na uzi huu, sitaweza kuzijibu zote, bali nazijinu kiujumla jumla humu

  Wakuu kwanza lazima nikiri wazi kuwa baadhi ya wapenzi wa Chadema mliojibu uzii huu uu miongoni mwa hazina kubwa ndani ya Chadema kutokana na genuinity na objectivity ya majibu yenu makini kwenye hoja hii.

  Niliwahi kusema humui kuwa chadema-haijajipanga nilishambuliwa sana. Wapenzi wa Chadema hawakusoma hoja zangu wakaishia kumjadili mtoa hoja!.

  Kuna siku nilisema humu jinsi ccm imechokwa mpaka basi!, nikimaanisha there is an opportunity to be seized!.

  Siku nyingine niliwaambia chadema, 2015 Ikulu njia nyeupe ila mjipange!, ni wachache waliojibu kwa makini!.

  Hiyo siku nilipokaa na Dr. Slaa, nilimweleza reservations zangu kuhusu sio tuu mgombea urais wa Chadema, bali nilieleza kuhusu udhaifu mkubwa wa Chadema katika kuwapata viongozi wake na wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uongozi wa ndani ya chama, na nje ya chama, kama serikali za mtaa, ubunge na udiwani.

  Nilimshauri Dr, Chadema ianze kuwa na succession plan ya kuwatayarisha viongozi wake, kwenye kila posti kuanzia nafasi za uongozi ndani ya chama, hadi nafasi za kugombea serikali za mitaa, udiwani, ubunge hadi urais, badala ya kuwategemea wanaotemwa CCM na kuwadaka tuu. Yes japo wanaotemwa tayari ni mtaji, lakini lazima lazima iwe na timu yake, ili kufika mahali hao wanaotemwa kupimwa streghts na waliopo, kama aliyepo ni stronger, huyo anayetemwa CCM, hapati nafasi Chadema.

  Na ili kujenga Chadema imara, chadema pia lazima kiwe na internal mechanism yake ya kufanya vetting kwa viongozi wake, vinginevyo inaweza kujikuta ina mapandikizi ya waliotemwa CCM na kuhama kwa hasira za kemwa, lakini mapenzi yao yako bado yako CCM, hivyo wanakuja Chadema ili kupata tuu, wakikosa, mtawashuhudia wakirejea CCM!.

  Pia ili kupata a dedicated team ya viongozi imara, Chadema ianzishe mfumo wa succession plan, kuwatarisha viongozi wake wa kesho by headhunting recruitment of committed leaders, iwafanyie grooming, iwapike, waive, ndipo ije iwape uongozi, mfano sasa hapo ilipo, tayari Freeman Mbowe ameisha overstay as Chairman, Chadema ianze maandalizi ya kuwapika viongozi wake kwa uenyekiti kwa kumuandaa nani atapokea Mbowe uenyekiti, ili kujenga succession plan bila makundi ili kujenga ssustainability ya chama chochote sustainable.

  Kwenye Chadema haijajipanga niliwaambia kuwa kuna baadhi ya maeneo, watu wameichoka CCM mpaka basi kiasi kwamba hata kama Chadema ingesimamisha jiwe, hilo jiwe lingepita!. Hii inamaanisha kama Chadema ingesimamisha wagombea kila jimbo, saa hizi mngekuwa na wabunge wengi zaidi ya hawa waliopo!.

  Miongoni mwa ushauri wangu kwa Dr. Slaa, Chadema isishobokee wagombea maarufu wala kusubiria makapi ya CCM!, good leaders are made and not born!. Nikashauri, Chadema ifanye incouragement kwa wanachama wake wenye nia mbalimbali za kugombea, wajitanabaishe tangu sasa ili wawe groomed kuja kugombea mara wakati utakapo wadia na sio kusubiria kipenga cha NEC kipulizwe, the time left will be too little too late!.

  Nikatolea mfano wa jimbo la Kinondoni, linashikiliwa na CCM miaka nenda, miaka rudi. Mgombea wa CCM tayari anajulikana, weaknesess zake zinajulikana, kama mimi ni mwana Chadema na nina nia ya kugombea Kinondoni come 2015, nitasema sasa na wote wenye nia wajitangaze ili miongoni mwetu, sote tujue nani ni best kutuletea ushindi, ndipo tumgroom tayari kwa kuiteka Kinondoni na sio kusubiri, CCM itamsimamisha nani!.

  Mfano kwa Mwaka 2015, Jimbo Ubungo, CCM huenda itampeleka Nape, Jimbo la Kawe, CCM itamrudisha Kippi, na majimbo yote yanayoshikiliwa na wapinzani, CCM itapeleka watu makini, na very strong, hivyo kama mimi ni mwana Chadema, najijua uwezo wangu kuiletea Chadema ushindi kwa jimbo Fulani ni mkubwa kuliko mbunge aliyepo, mfano jimbo la Kawe ni mkubwa kuliko uwezo wa Halima Mdee kulitetea jimbo la Kawe, nitaonyesha nia sasa kwa kujenga mtandao wa mazingira ya ushindi. Muda kuchukua fomu ukifika, mimi nitachukua fomu kwa jimbo la Kawe, na Halima Mdee nae atachukua fumu, Ben Saanane nae atajaza na Mzee Mwanakijiji pia atajaza, Chadema kitatupima wote, ni nani mwenye uwezo Zaidi na chances kubwa za ushindi, kinampitisha kupeperusha bendera ya Chadema, kama sio Halima, then Halima Mdee anakuwa ndio mhamasishaji mkuu wa mgombea mpya wa Chadema Kawe. Baada ya kumuengua Charles Mwera Tarime, niliwaambia makosa yenu na jimbo mlilitoa sadaka bure kabisa kwa kukosa busara!.

  Kwa sisi wapenzi wa demokrasia ya kweli ambao hatuna vyama, tunaamini hakuna mwana Chadema yoyote, mwenye hakimiliki ya kuhodhi nafasi yoyote ya uongozi kuanzia chini hadi uenyekiti. Nafasi zote za uongozi ndani ya chama na nje ya chama, ni haki ya kila mwanachama mwenye sifa, vigezo na uwezo!. Kama Zitto anazo sifa, vigezo na uwezo, kwanini azuiliwe asigombee?.

  Kwenye ule uzi wangu wa Chadema Hamjajipanga, niliwaambia Chadema kinakabiliwa na tuhuma za "udini" na "Ukaskazini", japo tuhuma hizi sio za kweli, likini zipo na sio za kupuuzwa!. Nikawashauri ili Chadema kiaminiwe na Watanzania wote, wa dini zote na maeneo yote, lazima hilo koti lenye harufu ya udini na ukaskazini, livuliwe!. Nikawashauri Zitto ni mtaji mkubwa sana kwenye kwenye kuondoa dhana hizo potofu, utumieni vizuri mtaji mlio nao kujiongezea mavuno!.

  Japo haikuandikwa popote, wagombea wa urais kwa CCM, wanapokezana, Muislamu na Mkristo!. Alianza Nyerere, Mkristo, akaja Mwinyi, Muislamu, akafuatia Ben Mkapa Mkristo, sasa ni JK, Muislamu, anayefuatia is more likely, Mkiristo (not necesarily). Prof. Lipumba, aligombea kama boya tuu ili kuhakikisha kura za Waislamu wasioipenda CCM, zisiende Chadema!. Kama 2015 CCM itamsimamisha mgombea Mkristo na Chadema ikamsimamisha Zitto ambaye ni Muislamu, Prof. Lipumba, hatathubuti kutia pua, maanayake boya halitaweza kufanya chochote!. Chadema itajivunia kura zote za ukanda wa Pwani zilizokwenda CUF!. Chadema itavuna kura za Waislamu wote wenye msimamo mkali walioko CCM, Chadema itavuna kura zote za Watanzania walioichoka CCM, Kundi kubwa la vijana, waliokata tamaa na kuamua kutopiga kura klwa sababu ya watu wale wale, chama kile kile na mambo yale yale, wakimuona Kijana mwenzao Zitto, anapeperusha bendera kuelekea magogoni, kwanza watajitokeza kujiandikisha kwa wingi, na watapiga kura kwa vingi kiasi cha CCM kuanguka chali, sio tuu kwa kifo cha mende, bali kipigo cha mbwa mwizi!. Hivi hizi opportunities zote za Zitto nyie wenzangu hamzioni?!.

  Kwa vile nilishazema toka juzi, jana, leo na kesho nitasema tena, mimi Pasco wa jf, sina chama!. Lakini kiukweli, CCM ndicho chama tawala kilichoko madarakani, namfagilia sana EL kama atakuwa ndie mgombea wa CCM, na nikasema kama afya yake ni mgogoro kuhimili pilika pilika za uchaguzi wa 2015, then the second best candidate kwa CCM ni Membe!, sio nawafangilie ili washinde, bali CCM iwasimamishe ili muwatumie kama pace makers wenu!.

  Mwenye masikio na asikie!.

  Pasco.
  12:24 am
   
 2. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hatukatai mtu kuonyesha matamanio,hapa suala linakojua ni mbinu unazozitumia,na timing pia.Yeye anataka kwa kuharibu na si kujenga.
   
 3. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Well said.
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  huu ndio upuuzi tusioutaka humu ndan...wewe peke yako ndio unajua ukweli juu ya dr slaa na hutaki kuusema hapa na wakati huo huo unasema kwa kuwa unaujua ukweli wa dr slaa juu ya hatima ya urais basi tumsapot zitto bila kutwambia hicho unachokijua juu ya dr slaa!!!!......sasa kwa nini umeleta uzi huu hapa? unataka kutuaminisha nini?.....halafu usinikumbush kabisa siku ya mazishi ya regia mtema maana uliharibu kaburi lake kwa kupanda juu eti ukitafuta kupiga picha kama dr slaa atashikana na mkono na kikwete wakati wa kusalmiana.....

  wewe ulishasema kuwa uko kwenye Eliairline na juzi hapa membe aliosema ana maadui 11 na watahamia kenya 2016 kama ataoteshwa na wewe ulionekana kumuunga mkono kama ataoteshwa...sasa unakuja na matango pori tena juu ya zitto......huyu zitto tunamdai video aliyosema ataweka humu tangu jana..sasa na wewe usitichanganyie habari sisi...wewe na ramadhani semtawa mko kundi moja!!!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ooh boy!! mbona umezunguka sana kusema hicho.
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CDM haina mambo ya mitandao.Hayo ya mitandao yapo CCM.By the way wewe msimamo wako unajulikana kwamba unamuunga mkono Edward Lowassa kwa hiyo unataka mitandao CDM ili isambaratishe chama mtu wako Lowassa apenye kirahisi.Umechemsha.
   
 7. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Mwambie Zitto aoe kwanza ndo aje kutangaza nia, Hatutaruhusu Rais kapera.
   
 8. makusanya

  makusanya JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Hamna Kitu
   
 9. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 730
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Zitto kutaka kugombea Uraisi sio tatizo wala sio kosa.. Dr. Slaa kwa maono yangu naona it is better hata yupo kimya on the matter sababu cha ajabu mengi ambayo yanazungumziwa kuhusu Uraisi in relation na Zitto (whether ni kweli ama ni uongo); kimsingi yalitakiwa yajadiliwe ndani ya CDM.

  Hili silent tiff lilitakiwa liwe resolved kwa njia za kujenga - In the sense ingekuwa ndani ya CDM wao wangeyajadili then mmoja wao ambae ni muwakilishi aje awakilishe msimamo wao juu ya habari za Zitto na Uraisi in relation na akina Nassari, Mdee et al.

  Kosa ambalo kwa wengine linaweza lisiwe apparent ni kitendo cha Zitto kutowa tamko ambalo linakuwa kama linawakandamiza wanachama wenzie... Kwa mtu mwenye akili ni lazima ujiulize huyu mtu ana nia gani? Unakuwa na mashaka kuwa yawezekana zile rumors juu yake za kuvuruga chama ni kweli? Haeleweki kabisa niya hasa na madhumuni yake.

  Kwa muktadha huo hata wana CCM ambao wanajua FIKA kuwa CCM ipo ulikingoni mwa maisha yake watataka Zitto ndio asimame kama raisi kuiwakilisha CDM...
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Damn!! Who da hell are you???
   
 11. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160

  Mzee salaam.......wala usipate taabu.....

  Composition is an art of which if supported with knowledge and courage then the result will obvious be the expected impact delivered from the content......and if one is not lucky enough to have all these qualities and yet s/he believes to be famous and strong then behind the very brain the thinking is that the later will replace the former pre-requisite.......

  Oooh poor believer.....!!!!!!!

  Si wote maarufu ni weledi kama wao wanavyopenda kueleweka
   
 12. GreenCity

  GreenCity JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 4,652
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  sasa kama unakiri mchakato bado, ya nini mtu kuanza kujijengea awareness kwa watu wakati utaratibu wa CDM kupata mgombea unafahamika? Zitto, kama ipo, ipo tu lakini mnayofanya sasa ni kama yale ya MAGAMBA na akina SHIBUDA. just keep silent and wait for the procedure.!
   
 13. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,492
  Likes Received: 5,591
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pasco,

  Tofautisha nidhamu ya NIA ya Zitto na nidhamu ya NIA ya Dr Slaa! mpaka sasa nidhamu gani yenye afya kwa chama?
   
 14. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,492
  Likes Received: 5,591
  Trophy Points: 280
  Pasco wa jf, sio mwanachama, mshabiki au mkereketwa wa chama chochoite cha siasa, bali ni muumini wa demokrasia ya kweli. Haaaaa wapi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 15. m

  mamajack JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ni kweli kabisa,sio kosa mtu kutaka kuwa kiongozi wa nchi hii.lakini pia naona kama mh. zitto anapaswa akae chini atulie and ajifanyie tathimini mwentewe.binafsi zito ni mwakilishi mzuri wa wananchi andamekuwa akifanya vizuri kazi zake.chaajabu,ni njinsi jammii anayoiongoza ilivyokuwa na mtazamo hasi(-) kwake.mie namshauri zitto atulie maana jinsi siku zinavyoendelea,amekuwa akihusishwa na tuhuma kibao ambazo sio nzuri,ajiulize ni wapi anakosea maana asipotulia magamba watamtumia and mwisho wa kuwa tegemeo kwa wananchi utafika.zitto skando zimekuwa nyingi sana bana,utadhani msanii kumbe kiongozi na mwakilishi wa wananchi.
  zito wa zamani anapotea anaelekea kuwa zito mambo leo.tafadhali mh.turejeshee yule zito mwenye uchungu na nchi hii anayefanya kazi yenye maslahi kwa wote.hivyo vya urais mie sitaki kuviongelea maana maamuzi yapo kwa wanachama wenzio.
   
 16. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Pasco umenena! wasiwasi wangu ni tabia mpya ya kukanusha iliyojengwa na viongozi wa cdm
   
 17. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Hii kauli pro-cdm hawataifurahia
   
 18. fyddell

  fyddell JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 2,082
  Likes Received: 769
  Trophy Points: 280
  Tunasubili video aliyotuahidi. Na kwanini aanze kujenga uadui na wenzake kina Mdee na Nasari kama kweli nia yao yote ni moja ya kukijenga chama.
   
 19. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kwani kuna kuna uhusiano gani kati ya ugombeaji wa Slaa na wa Zitto au mwanachama mwingine? Kwamba kuna watu wanataka Slaa kwanza akatae ndio wengine waruhusiwe? Kwani CHADEMA wanapeana nafasi, au ni mchakato wa mchujo? Naona hapo umeandika kama Ponda wa sensa!
   
 20. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Oops Pasco, msalimie "Iron man" Lowassa.
   
Loading...