Urais 2015 hatari - UCHAGUZI WA UVCCM, WAZAZI VITA MPYA CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urais 2015 hatari - UCHAGUZI WA UVCCM, WAZAZI VITA MPYA CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 12, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]• UCHAGUZI WA UVCCM, WAZAZI VITA MPYA CCM

  na Martin Malera
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  HARAKATI za kuwania urais mwaka 2015 ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), zimefika hatua mbaya ya watu wanaotajwa kuwa katika orodha ya wagombea na wapambe wao kuingiwa na hofu ya kudhuriana na kuombeana mabaya, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

  Hofu hiyo imeongezeka zaidi hasa kutokana na ugonjwa wa ajabu anaougua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ambao taarifa zisizo rasmi zinauhusisha na kuwapo kwa mikono ya watu.

  Ingawa hadi sasa si Mwakyembe mwenyewe au mamlaka yoyote ya umma aliyetoa taarifa rasmi ya nini hasa anaugua mwanasiasa huyo, lakini kauli ambazo alizitoa siku chache zilizopita zinaongeza chumvi katika mashaka hayo.


  Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Mwakyembe aliyerejea kutoka katika matibabu nchini India alisema hana sababu ya kulipiza kisasi na kwamba anamwachia Mungu.


  Kauli hiyo imeibua maneno mengi miongoni mwa wanasiasa ambao baadhi wamekuwa wakiitafsiri kuwa inayothibitisha wasiwasi uliotanda kwamba huenda mwanasiasa huyo anaugua kutokana na kudhuriwa na wanasiasa washindani wake.


  Wakati ugonjwa anaougua Mwakyembe ukiwa bado unazusha mashaka, kuugua kwa muda mrefu kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya nako kuliibua maneno mengi.


  Habari ambazo zilimkariri Mwandosya mwenyewe na watu walio karibu naye zinaeleza kwamba, ugonjwa wake ulisababisha baadhi ya wanasiasa ndani ya CCM kumchulia kifo kutokana na maradhi hayo.


  Kabla na baada ya kurejea nchini kutoka katika matibabu yake nchini India, Mwandosya alikaririwa akisema watu waliokuwa wakimchulia kifo, walitakiwa kutambua kwamba watalazimika kusubiri kwa muda mrefu kabla ya hilo (kifo) kumfika.


  Wakati hali ikiwa hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa, kumekuwa na hali ya kutoaminiana na kutiliana sana mashaka miongoni mwa makada maarufu ndani ya CCM ambayo yote inahusishwa na mchakato wa urais ndani ya chama hicho mwaka 2015.


  Kada mmoja maarufu wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima Jumatano amesema wamefikia hatua ya kujilinda kwa kuwa waangalifu katika matembezi na sehemu wanazokula chakula kwa sababu hizo hizo.


  Kwa mujibu wa kada huyo, wanasiasa takriban wote wanaotajwa kuwa wanatarajia kugombea urais kupitia chama hicho wamefikia hatua ya kujilinda kwa silaha za moto na wengine kutumia mafuta maalum yanayoaminika kuzuia sumu.


  "Tumefika pabaya, hali ni ngumu sana. Sasa hivi watu wamegawana hata maeneo ya kutembelea. Kwa mfano kama kundi fulani lina kawaida ya kupata bia kwenye baa au hoteli fulani, makada wa kundi lingine hawafiki.


  "Ikitokea mmekutana kwa bahati mbaya, mmoja lazima aondoke," alisema mmoja wa makada wanaotajwa kuwania urais.


  Kiongozi mmoja mstaafu anayetajwa kuwa miongoni mwa wagombea urais naye anaelezwa kwamba amelazimika kuchukua hatua kadha wa kadha za kujilinda ili kuepukana na hatari ya kudhuriwa na washindani wake wa kisiasa ndani ya CCM.


  "Hivi sasa tumefika mahali tunasafiri kwa tahadhari kubwa na kwa kutumia usafiri ambao baadhi ya watu wanaotulenga hawawezi kututambua kama njia ya kukabiliana na hatari ambayo inahusishwa na urais wa mwaka 2015," amekaririwa akisema mwanasiasa huyo mstaafu.


  Wakati hayo yakitokea kumbukumbu zinaonyesha kwamba kwa nyakati tofauti wanasiasa wawili, akiwamo Mwakyembe mwenyewe na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta wamepata kutoa taarifa za maisha yao kutishiwa.


  Sitta ambaye duru za kisiasa zinamtaja kuwa mmoja wa wanaofikiria urais, amepata kukaririwa kwamba amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa kupitia simu yake ya mkononi kwa njia ya ujumbe mfupi na watu asiowajua.


  Mgombea mwingine ambaye jina lake nalo limehusishwa na tishio la maisha yake ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.


  Gazeti moja la kila wiki (siyo Tanzania Daima) lilipata kumkariri mtoto wa mwanasiasa huyo akilalamika kuhusu kuwapo kwa tishio la maisha ya mzazi wake huyo.


  Ingawa wenyewe hawajatamka rasmi, baadhi ya makada wengine wanaotajwa kufukuzana kurithi nafasi ya Rais Jakaya Kikwete mwaka 2015 ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Dk. Emmanuel Nchimbi, Hussein Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda.


  Majina ya wanasiasa wengine wanaotajwa ni pamoja na Mathias Chikawe, John Magufuli, William Ngeleja, Lazaro Nyalandu na Ezekiel Maige.


  Katika hatua nyingine, wakati Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), unatarajiwa kufanyika mwaka huu, chama hicho kimejikuta kikiingia kwenye vita mpya ya kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee na ile ya Umoja wa Vijana (UVCCM).


  Ugumu wa uchaguzi huo, unatokana na makundi yanayowania urais ndani ya CCM mwaka 2015 kufanya kila iwezalo kuhakikisha inamwingiza mtu wake ambaye atapata nafasi ya kuingia kwenye vikao muhimu vya maamuzi, yaani Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC).


  Tayari makundi hayo ya urais yameshaanza harakati za kuhakikisha yanashika nafasi hizo nyeti kwa gharama yoyote ile.


  Kiti cha Mwenyekiti wa Wazazi CCM, kimeachwa wazi baada ya aliyekuwa kiongozi wa nafasi hiyo kufariki wiki iliyopita wakati nafasi ya umoja wa vijana iko wazi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Masauni Masauni, kuamua kujiuzulu kutokana na kashfa ya kughushi umri wake.  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  sioni jipya,ni yaleyale tuliyokwishayasikia
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Uandishi wa kijinga na kipumbavu hakuna habari hapa! Tanzania Daima ina boa
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  CCM wagonjwa watapiana ngwala nasubiri UWT nataka mama Simba aanguke
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Mama noninooo muda wake umeisha maana yeye siasa zake za kukurupuka na za fitna kwa sasa hizo siasa zilipita na wakati na mtandao mpya hana nafasi tena yeye alipewa kazi ya kuwaumbua wanafiki wenzake kwenye ule mtandao wa mwanzo...sasa siasa zimempiga teke muda si wake!!!
   
 6. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,134
  Trophy Points: 280
  UVCCM is only relevant kama asilimia 70 watanzania ambao takwimu show kwamba wao ndio 70% ya population, as watanzania wenye umri chini ya miaka 30, will make it relevant. Otherwise, kama CCM ina jumla ya wanachama milioni sita leo hii, kati ya jumla watanzania karibia milioni 45, what the hell is UVCCM? Tafakari.
   
 7. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  That's very true, as far as politics is concerned in this country, UVCCM is totally irrelevant. Ni genge la VIFISADI vinavyojiandaa kuwa MAFISADI.

  Walipaswa kuwa link kati ya Chama na vijana, lakini hawataki hata kukutana na vijana. Wakati BAVICHA wakiandaa makongamano ya vijana wa vyuo vikuu, wao ni kupigana vikumbo kuhusu nani atakuwa rais 2015.
   
 8. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,827
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  Hizo habari za magamba tumezichoka, tunachotaka kusikia ni kwamba wameuana kabisa sio hisia za vifo kila siku. Wauane tu makaburi yapo tele
   
Loading...