Story of Change Uraibu wa Ponografia

Jade_

Senior Member
Apr 19, 2015
153
225
`Kuna mtu hapa Jamii Forum alielezea kisa chake na kwamba anaweza kujifungia ndani akiangalia video za ngono huku akipiga punyeto kwa masaa hata 12. Kuna watu walifikiri hii ni “chai” (uongo) lakini watu wanapata sana hizi shida ila hawawezi kuongea kwa kuwa ni aibu kwenye jamii. Unaweza kukuta kundi la vijana limeinamia simu ukafikiri wanafanya kitu cha maana kumbe wanaangalia ponografia. Siku hizi hata watoto wanakutana na hizi video mtandaoni na zinawaharibu mapema sana. Rejea uzi wangu wa jinsi mtoto anavyoathiriwa na elimu anayopata akiwa mdogo sana.

Watu wengi sana wameingia katika dimbwi la uraibu wa video za ngono za mtandaoni, na wanatafunwa taratibu bila wao wenyewe kujijua. Uraibu huu ni mbaya sana kuliko uraibu wa madawa au pombe na madhara yake ni kama ya kulevya. Familia zinaangamia, vizazi na vizazi hurithishana tabia hizi na watu wanabaki na maumivu makali sana kwenye nafsi zao. Rejea uzi wangu kuhusu uraibu wa ngono kiujumla. Uraibu huu unasababisha magonjwa mengi ya kisaikolojia kama vile sonona, kuharibu ubongo kibayolojia, kuumwa mwili na kwa wanaume zinapunguza nguvu za kiume na hata kupelekea uhanisi. Mtu atalalamika sana, atazunguka hospitali zote na kwa waganga wote kutafuta tiba ya ugonjwa wa nguvu za kiume lakini tiba inaweza kuwa kuacha kuangalia video za ngono. Uraibu huu unaambatana na uraibu wa kupiga punyeto.

Dalili za uraibu wa video za ngono ni kukaa muda mwingi sana mtandaoni unatafuta video hizi. Yaani kama upo nyumbani unaanza kwanza taratibu kusaka video ambazo zinaweza kukidhi mahitaji yako huku unapiga punyeto na ukikaribia kufikia mshindo unaacha kwanza unaendelea kutafuta video nyingine tena. Mwingine akiona tu tarakinishi tayari anapata hamu anatamani aende tu kwenye video hizo. Mtu kama huyu, kwa sababu waigizaji kwenye sinema hizi wanafanyia plastic surgery sehemu zao za siri (wanawake) na wanachukuliwa wale wenye maungo makubwa (wanaume) basi anatamani tu kulala na watu wa aina hii. Anakuwa hana hamu na watu wa kawaida, na kwa wanaume atajiona amepungukiwa nguvu za kiume.

Dalili nyingine ni kwamba mtu huyu anaanza kuwa na tamaa nyingine ambazo hakuwahi kuwa nazo kama vile mapenzi ya jinsia moja, kupitia mtaroni, mapenzi na watoto, mapenzi na wanyama au mapenzi na ndugu. Anataka kufanya staili za kila namna akiona kwenye video hizi na kifo cha mende kinaonekana ni ushamba. Hii ni kwa sababu ponografia hushtusha na hisia za kushtuka na za kupata hamu zinafanana sana (moyo unadunda kwa haraka zaidi, unaanza kusikia joto nk). Hivyo basi unaufundisha ubongo kwamba ili upate raha inabidi uangalie na kufanya makubwa zaidi vitakavyokushtua. Utaanza na video za ngono za kawaida lakini kadiri unavyoendelea kuzoea utatafuta zinazokushtua ambazo si za kawaida na mwishowe utajikuta ambako ukuwahi kutarajia kuwepo. Dalili zipo nyingi na chache za kuongezea ni mtu kupoteza mahusiano mazuri aliyowahi kuwa nayo kama ya ndugu jamaa na marafiki, kutokufanya vizuri shuleni na kazini, kubadilika hulka ghafla bila sababu ya msingi nk.

Video za ngono za mtandaoni kiukweli ni aina ya udhalilishaji kwa wanawake. Hata wanawake wanaocheza hizi video wanakuwa tayari wana matatizo ya kisaikolojia (aidha waliwahi kudhalilishwa kingono au walilelewa kwenye mazingira hatarishi) kwa hiyo wanakuwa na chuki binafsi. Mwanamke mwenye uraibu wa kuangalia video hizi atataka kufanyiwa kama wanawake kwenye hizi video wanavyofanyiwa (matendo ya aibu) na bila ya yeye kudhalilishwa anaona kama hajapata raha.

Kwa wanaume wao ni mwendo wakudhalilisha. Asilimia kubwa ya video kwenye tovuti za ponografia zinahamasisha kutoka na watoto, kutoka na ndugu, kufanya mapenzi ya jinsia moja, kubaka, kufanya unyanyasaji wa kingono nk. Hii inajionyesha moja kwa moja kwenye jamii, mtu anaona kama kumvunjia au kuvunjiwa heshima ndio mapenzi yenyewe. Kitu ambacho si kweli na husababishia watu vidonda visivyotibika.

Kama una uraibu huu lazima ufanye kila namna uache kuangalia video za ngono. Kufanya hivi ni ngumu mno lakini ni kitu kinachowezekana. Kama mtu anavyoanza kuacha madawa ni lazima kwanza uanze kupunguza kuangalia video hizi. Siku za mwanzoni utajisikia vibaya sana, unaweza hata kuumwa lakini ni muhimu ujikaze na usikate tamaa. Unatakiwa kupunguza taratibu mpaka uje kuacha kabisa. Wewe mwenyewe utashangaa jinsi maisha yako yatakavyobadilika na pia hata matatizo madogo (kuumwa, uchovu, kukosa hamu ya kula, kutoweza kufikiri au kutumia ubongo kwa kina nk.) yatapotea kwenye maisha yako. Watu wengi wanafikiria kwamba wamelogwa lakini yote haya ni madhara ya ponografia. Video za ngono si za kuangalia mara mojamoja, bali ni kitu cha kutoangalia kabisa.

Kitabu cha Your Brain on Porn: Internet Pornography and the Emerging Science of Addiction cha Gary Wilson kinaongelea kwa ukubwa na kwa undani zaidi kuhusu uraibu huu.
 
Upvote 24

hermanthegreat

Senior Member
Mar 2, 2021
166
500
No you read and study more. And on top of that brainstorm and start thinking for yourself. Maybe even try to find people with a porn addiction (if you don't have one) to get their experience.
The problem is not your mind, it's your mindset!.
 
Hardbody

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
2,401
2,000
Andiko zuri na linafundisha. I was once addicted but now nashkuru Mungu nimeanza kuzisahau
 
Jade_

Senior Member
Apr 19, 2015
153
225
Andiko zuri na linafundisha. I was once addicted but now nashkuru Mungu nimeanza kuzisahau
Ahsante na hongera mkuu. Unaweza kutushirikisha kisa chako ili kama kuna mtu atapitia huu uzi aweze kujifunza kitu?
 
agudev

Member
Apr 5, 2016
43
125
`Kuna mtu hapa Jamii Forum alielezea kisa chake na kwamba anaweza kujifungia ndani akiangalia video za ngono huku akipiga punyeto kwa masaa hata 12. Kuna watu walifikiri hii ni “chai” (uongo) lakini watu wanapata sana hizi shida ila hawawezi kuongea kwa kuwa ni aibu kwenye jamii. Unaweza kukuta kundi la vijana limeinamia simu ukafikiri wanafanya kitu cha maana kumbe wanaangalia ponografia. Siku hizi hata watoto wanakutana na hizi video mtandaoni na zinawaharibu mapema sana. Rejea uzi wangu wa jinsi mtoto anavyoathiriwa na elimu anayopata akiwa mdogo sana.

Watu wengi sana wameingia katika dimbwi la uraibu wa video za ngono za mtandaoni, na wanatafunwa taratibu bila wao wenyewe kujijua. Uraibu huu ni mbaya sana kuliko uraibu wa madawa au pombe na madhara yake ni kama ya kulevya. Familia zinaangamia, vizazi na vizazi hurithishana tabia hizi na watu wanabaki na maumivu makali sana kwenye nafsi zao. Rejea uzi wangu kuhusu uraibu wa ngono kiujumla. Uraibu huu unasababisha magonjwa mengi ya kisaikolojia kama vile sonona, kuharibu ubongo kibayolojia, kuumwa mwili na kwa wanaume zinapunguza nguvu za kiume na hata kupelekea uhanisi. Mtu atalalamika sana, atazunguka hospitali zote na kwa waganga wote kutafuta tiba ya ugonjwa wa nguvu za kiume lakini tiba inaweza kuwa kuacha kuangalia video za ngono. Uraibu huu unaambatana na uraibu wa kupiga punyeto.

Dalili za uraibu wa video za ngono ni kukaa muda mwingi sana mtandaoni unatafuta video hizi. Yaani kama upo nyumbani unaanza kwanza taratibu kusaka video ambazo zinaweza kukidhi mahitaji yako huku unapiga punyeto na ukikaribia kufikia mshindo unaacha kwanza unaendelea kutafuta video nyingine tena. Mwingine akiona tu tarakinishi tayari anapata hamu anatamani aende tu kwenye video hizo. Mtu kama huyu, kwa sababu waigizaji kwenye sinema hizi wanafanyia plastic surgery sehemu zao za siri (wanawake) na wanachukuliwa wale wenye maungo makubwa (wanaume) basi anatamani tu kulala na watu wa aina hii. Anakuwa hana hamu na watu wa kawaida, na kwa wanaume atajiona amepungukiwa nguvu za kiume.

Dalili nyingine ni kwamba mtu huyu anaanza kuwa na tamaa nyingine ambazo hakuwahi kuwa nazo kama vile mapenzi ya jinsia moja, kupitia mtaroni, mapenzi na watoto, mapenzi na wanyama au mapenzi na ndugu. Anataka kufanya staili za kila namna akiona kwenye video hizi na kifo cha mende kinaonekana ni ushamba. Hii ni kwa sababu ponografia hushtusha na hisia za kushtuka na za kupata hamu zinafanana sana (moyo unadunda kwa haraka zaidi, unaanza kusikia joto nk). Hivyo basi unaufundisha ubongo kwamba ili upate raha inabidi uangalie na kufanya makubwa zaidi vitakavyokushtua. Utaanza na video za ngono za kawaida lakini kadiri unavyoendelea kuzoea utatafuta zinazokushtua ambazo si za kawaida na mwishowe utajikuta ambako ukuwahi kutarajia kuwepo. Dalili zipo nyingi na chache za kuongezea ni mtu kupoteza mahusiano mazuri aliyowahi kuwa nayo kama ya ndugu jamaa na marafiki, kutokufanya vizuri shuleni na kazini, kubadilika hulka ghafla bila sababu ya msingi nk.

Video za ngono za mtandaoni kiukweli ni aina ya udhalilishaji kwa wanawake. Hata wanawake wanaocheza hizi video wanakuwa tayari wana matatizo ya kisaikolojia (aidha waliwahi kudhalilishwa kingono au walilelewa kwenye mazingira hatarishi) kwa hiyo wanakuwa na chuki binafsi. Mwanamke mwenye uraibu wa kuangalia video hizi atataka kufanyiwa kama wanawake kwenye hizi video wanavyofanyiwa (matendo ya aibu) na bila ya yeye kudhalilishwa anaona kama hajapata raha.

Kwa wanaume wao ni mwendo wakudhalilisha. Asilimia kubwa ya video kwenye tovuti za ponografia zinahamasisha kutoka na watoto, kutoka na ndugu, kufanya mapenzi ya jinsia moja, kubaka, kufanya unyanyasaji wa kingono nk. Hii inajionyesha moja kwa moja kwenye jamii, mtu anaona kama kumvunjia au kuvunjiwa heshima ndio mapenzi yenyewe. Kitu ambacho si kweli na husababishia watu vidonda visivyotibika.

Kama una uraibu huu lazima ufanye kila namna uache kuangalia video za ngono. Kufanya hivi ni ngumu mno lakini ni kitu kinachowezekana. Kama mtu anavyoanza kuacha madawa ni lazima kwanza uanze kupunguza kuangalia video hizi. Siku za mwanzoni utajisikia vibaya sana, unaweza hata kuumwa lakini ni muhimu ujikaze na usikate tamaa. Unatakiwa kupunguza taratibu mpaka uje kuacha kabisa. Wewe mwenyewe utashangaa jinsi maisha yako yatakavyobadilika na pia hata matatizo madogo (kuumwa, uchovu, kukosa hamu ya kula, kutoweza kufikiri au kutumia ubongo kwa kina nk.) yatapotea kwenye maisha yako. Watu wengi wanafikiria kwamba wamelogwa lakini yote haya ni madhara ya ponografia. Video za ngono si za kuangalia mara mojamoja, bali ni kitu cha kutoangalia kabisa.

Kitabu cha Your Brain on Porn: Internet Pornography and the Emerging Science of Addiction cha Gary Wilson kinaongelea kwa ukubwa na kwa undani zaidi kuhusu uraibu huu.
Nakubaliana 100% na post yako kuhusu hii hoja mkuu, uraibu huu watu wengi wanaogopa kuuongelea kutokana na aibu ya kuonekana mdahifu wa kushindwa kucontrol hisia zake mwenyewe na hii inasabisha mtu kuugulia kwa ndani na ingawa mara nyingine hutamani msaada anashindwa kuuomba na hii husababisha kukata tamaa zaidi na kurudi pale pale kama njia pekee ya kujiliwaza, hii inaingia na kuharibu sehemu mbalimbali za maisha ya mtu mwenye uraibu huu, hutumia hii kama njia ya kupunguza mawazo na kufanya mwili urelax na kuondoa stress na hii husaidia mara nyingi mtu akijumuisha na tendo la punyeto kwani mwili hutoa vichocheo mbalimbali hasa "dopamine" ambayo inafanya kazi kumfanya mtu ajisikie raha na utulivu, kichocheo hiki cha "dopamine" ndicho kinachochangia sana mtu kujenga tabia, ubongo kila muda unakuwa unatamani kile kitu chenye kuweza kutoa dopamine nyingi zaidi na kwa jinsi miili yetu ilivyo, hisia ya tendo la ndoa na kufika kileleni ni mojawapo ya vitu ambayo vinatoa "dopamine" nyingi na hivyo kuwa rahisi kwa mtu mwenye huu uraibu kutamani mara kwa mara.

Ingawa watu wengi wanapenda kujidanganya kwamba tendo hili halina utofauti wowote na ponografia/punyeto, ukweli ni kwamba tendo la ndoa linahitaji mtu kufanya "effort" kutafuta mwenzi na kumuandaa na vitu vingine vingi hapo katikati ndipo mwisho wa siku uweze kupata hiyo "dopamine" tofauti na ponografia na punyeto ambayo ni kitendo cha kubofya tu, tayari kila kitu unapata kiganjani 😉, "dopamine" ya jinsi hii naifananisha na ile ya chakula cha kawaida cha wanga (mf. ugali, wali n.k) na chakula chenye sukari nyingi (mf. ice cream, keki, chocolate), mwisho wa siku vitu vyote hivi vinavunjwa kuwa sukari rahisi ("glucose") lakini kimoja hutoa sukari nyingi zaidi na kwa uharaka kuliko kingine na kuwa na uwezo mkubwa wa kusababisha uraibu.

Wanasayansi wanasema "dopamine" ni mojawapo ya kichocheo kinachofanya mtu awe na hamu ya kufanya kitu fulani, vitu kama vile hobby, kula chakula, kuchangamana na watu n.k huwa vinafanya mtu apate kiasi fulani cha hii "dopamine" na humfanya ajisikie vizuri. Ubaya wa ponographia (na punyeto) ni kwamba kinafanya kichocheo hiki kitoke kwa wingi sana zaidi ya vile ambavyo mwili ungeitoa na urahisi na kificho cha tendo hili huwa kama njia shortcut ya kuweza kupata "dopamine" bila kushughulika sana, matokeo yake mwili unakuwa umezoeshwa kupata dozi nyingi ya hiki kichocheo na vitu vingine vya kawaida vinavyotoa "dopamine" pungufu vinakuwa havina mashiko tena, hivyo mtu anakuwa anapoteza hamu katika mambo mengi ya msingi ambayo yanahitaji ushughulishe mwili na akili kwanza kabla ya kupata hyo "dopamine" na badala yake kung'ang'ania hapa hapa anapoweza kupata furaha ya muda mfupi bila ya gharama na usumbufu wowote.

Kama mtu una muda unaweza kupitia forums kama "NoFap" kwenye reddit r/NoFap au NoFap® kuona jinsi gani watu mbalimbali duniani wanavyopambana na vitu hivi ili upate experience ya moja kwa moja ya wahusika, kiukweli wapo watu wengi wanateseka kwa siri na hili janga.

Vijana wenzangu wanaume kwa wanawake tujitahidi tupambane na huu "ugonjwa" kwani unatuua chini chini bila ya sisi kujua, ile raha na uchangamfu tunayoipata kwa muda mfupi inatufanya tusiweze kupambana kuweza kufikia level ambazo tungeweza kufikia kama tusingekuwa waraibu wa hili janga.

Nawatakia mapambano mema.
 
Ahsante mkuu kwa mchango wako. Hizo subreddits nilizipitia nilipokuwa nafanyia utafiti huu uzi. Wahanga wakipitia huko kutawasaidia sana.
Dopamine ni double edged sword, ikizidi sana unakua sugu, mwili unapata shida zaidi kuiproduce hivyo kusababisha depression.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom